Jumatano, 15 Shawwal 1445 | 2024/04/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Je, Ramadhan itaweka Taqwa katika Nyoyo zenu Kusimama kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina?

Hizb ut Tahrir / Kenya kwa furaha, inawapongeza Waislamu nchini na kote duniani kwa ujumla kwa kuwasili kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je, Ramadhan itaweka Taqwa katika Nyoyo zenu Kusimama kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina?

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Kenya kwa furaha, inawapongeza Waislamu nchini na kote duniani kwa ujumla kwa kuwasili kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Tunapoingia katika mwezi huu wa rehema, msamaha na kukombolewa na Moto wa Jahannam, tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atujaalie nguvu na afya ya kutekeleza amali adhimu ya saumu ambayo si wajibu tu bali ni moja ya nguzo tano za Uislamu.

Ramadhan hii inakuja huku ulimwengu ukishuhudia mgongano kati ya matakwa ya Umma wa Kiislamu ya kushikamana na Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na matakwa ya ukafiri wa Magharibi. Umma umeonyesha uaminifu wake kwa Uislamu na unatamani kwa dhati ushindi wa Mwenyezi Mungu. Ulimwengu unashuhudia kufilisika kiakhlaqi kwa maadili ya Magharibi huku wakiunga mkono mashambulizi ya kikatili ya ‘Israel’ huko Gaza. Dola na vyombo vya habari vya Magharibi vinaonyesha rangi zao halisi za unafiki na ubaguzi wa rangi.

Cha kusikitisha ni kwamba, unyama unaofanywa na majeshi ya Kiyahudi dhidi ya ndugu zetu wa Gaza bado haujachemsha nyoyo wala mishipa ya viongozi wa Kiislamu na majeshi yao! Enyi viongozi! Je, saumu yenu itaweka taqwa katika nyoyo zenu na kukata mahusiano na umbile la Kiyahudi? Enyi majeshi, je Ramadhan itawapeni taqwa ya kuwapuuza watawala wenu waliomfanyia khiyana Mwenyezi Mungu, Mtume wake na waumini ili muanze kuandamana kwenda Palestina na kupigana na jeshi la Mayahudi?

Katika historia yote, Ramadhan imekuwa ni mwezi wa ukombozi na ushindi. Historia hii angavu kwa hakika itahuisha ushindi katika Vita vya Badr, Qadisiyyah na Ein Jalut. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atukubalie amali zetu na aujaalie Ummah huu mlinzi na ngao Khilafah kwa njia ya Utume. Khilafah ambayo itakusanya majeshi ya Waislamu ili kuling'oa umbile uaji la Kiyahudi na kukomboa sio tu Palestina inayokaliwa kwa mabavu bali ardhi zote za Waislamu.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya

Soma zaidi...

Sera ya Afya bila Afya

Wizara ya Afya imefichua kuwa Ksh.20 bilioni zimepotea kupitia mpango wa Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF) kupitia madai fidia za kirongo na upasuaji ghushi, miongoni mwa shughuli nyingine za ulaghai zinazofanywa na vituo vya afya.

Soma zaidi...

Mfumo wa Kibepari: Janga Juu ya Majanga

Makumi ya maelfu ya watu kote nchini wameathiriwa na mvua kubwa, mafuriko na maporomoko ya ardhi. Kenya, ikiwa ni pamoja na Pembe ya Afrika imekumbwa na mvua kubwa inayohusishwa na hali ya hewa ya El Nino katika wiki za hivi karibuni iliyosababisha vifo vya makumi ya watu, ikiwa ni pamoja na zaidi ya 100 katika maeneo mbalimbali ya Kenya.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir Kenya yafanya Maandamano baridi kutoa mwito kwa Majeshi ya Kiislamu Wakomboe Al-Aqsa kutoka kwa Makucha ya Umbile la Kiyahudi

Kufuatia mauaji ya halaiki yanayoendelea kufanywa na serikali ya kinyama ya kizayuni dhidi ya watu wa Ghaza, Hizb ut Tahrir Kenya iliweza kufanya maandamano baridi mnamo siku ya Ijumaa Oktoba 20,2023 katika miji ya Nairobi na Mombasa sambamba na miji mengine ya pwani.

Soma zaidi...

Wala Msifanye Uvivu Kuwafuatia Maadui kama Mumepata Maumivu Basi Wao Pia Watapata. Na Nyinyi Mnatumai Kwa Mwenyezi Mungu Yale Wasiyoyatumainia

Jumamosi tarehe saba Oktoba mwaka 2023, mashujaa wa ukanda wa Gaza walivuka mipaka ya umbile la Kiyahudi. Walishambulia ngome za adui na hivyo kufanya nyuso zao kuwa nyeusi. Shambulizi hili dhidi ya Jeshi la Kiyahudi limekashifiwa kote duniani ikiwemo Afrika.

Soma zaidi...

Hali Ngumu ya Kiuchumi: Matunda ya Mti Mouvu wa Mfumo wa Kiuchumi wa Kibepari Uliong’olewa Ardhini

Mwaka mmoja baada ya serikali ya Kenya Kwanza kuchukua hatamu za uongozi, hali ya kiuchumi na maisha ya raia wa kawaida imezidi kuwa mbaya. Ni dhahiri shahiri kwamba matarajio makubwa ya wananchi kurahisishiwa gharama za maisha na utawala ulioko mamlakani sambamba na kuondokewa na malimbikizi ya deni la taifa, yamegeuka kuwa mangati/mazigazi.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu