Jumapili, 11 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  8 Ramadan 1445 Na: Afg. 1445 H / 11
M.  Jumatatu, 18 Machi 2024

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
UNAMA ni Chombo cha Kisiasa na Wakala wa Ujasusi wa Dola za Magharibi; Kazi yake nchini Afghanistan Lazima Ikomeshwe Mara Moja!
(Imetafsiriwa)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja liliidhinisha azimio la kuongeza muda wa Misheni ya Usaidizi ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA) kwa mwaka mwingine. Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa alitaja kuregeshwa kwa uwepo wa UNAMA nchini Afghanistan kuwa ni "muhimu" na kusema kwamba jumuiya ya kimataifa inataka "kuzidisha maingiliano na kujenga imani" na Taliban.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Afghanistan inalaani kuongezwa kwa muda wa UNAMA na inaichukulia kuwa misheni ovu na chafu - ambayo mwendelezo wake ni hatari kwa watu wa Afghanistan unaolenga kuwapurukusha watawala wa sasa kutokana na utabikishaji kamili wa Uislamu.

Kazi ya UNAMA kwa hakika inahusishwa na uvamizi na sera za dola kuu nchini Afghanistan. Wakati nchi hiyo ilipokuwa chini ya udhibiti wa Marekani, kazi ya UNAMA iliidhinishwa na Baraza la Usalama mwaka 2002 kwa lengo la kuleta mageuzi ya kisiasa, kiuchumi na 'yenye msingi wa thamani' nchini Afghanistan. Kwa hakika, UNAMA imekuwa tawi la kisiasa na kithaqafa la ukoloni katika kipindi cha miaka 20 iliyopita ya Jamhuri ambayo imefanya juhudi kubwa kuongoza ajenda za usekula na mageuzi ya kisiasa kwa msingi wa demokrasia huku ikidhoofisha maadili ya Kiislamu nchini. Baada ya kuondoka kwa aibu kwa vikosi vya Marekani na NATO, mashirika ya kisiasa na kitamaduni na misheni ya uvamizi huo pia yalipaswa kuondolewa kutoka kwa uso wa Afghanistan. Lakini sio tu kwamba misheni hii hatari iliendelea, leo UNAMA inafanya kazi kama mwavuli mkubwa unaojumuisha mashirika 20, fedha na programu zinazolenga kukuza maadili ya kiliberali na mageuzi ya kisiasa ya kidemokrasia chini ya pazia la misaada ya kibinadamu.

Kilichotuletea majuto na wasiwasi zaidi ni kwamba msemaji rasmi wa serikali ya Afghanistan amekaribisha kuongezwa muda kwa mamlaka ya UNAMA. Alisema katika Televisheni ya Taifa ya Afghanistan inayomilikiwa na Serikali: "InShaAllah (Mungu akipenda), itakuwa kwa manufaa ya Afghanistan kwa sababu Afghanistan inahitaji kuwasiliana na nchi na mashirika. Katika suala hili, UNAMA inaweza kuwa kama kichocheo cha kuimarisha uhusiano." Kwa hakika Umoja wa Mataifa, misheni na mashirika yake ni mashirika ya kijasusi na vyombo vya kisiasa vya dola za Magharibi ambayo shughuli zake hazina taathira nyingine isipokuwa uovu na masaibu. Kudumisha uhusiano wowote na kuwa na mtazamo chanya kwa Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kimataifa ni kosa kubwa la kisiasa lenye matokeo hatari.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِنْ دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ إِنْ كُنْتُمْ تَعْقِلُونَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.” [Aali-Imran: 118]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu