Jumatatu, 27 Shawwal 1445 | 2024/05/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  9 Muharram 1444 Na: 1444 / 01
M.  Jumapili, 07 Agosti 2022

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
Mheshimiwa Al-Hajj Muhammed Naeem Muhammed Hasan (Abu Usamah Zukarnah) Mmoja wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir

(Imetafsiriwa)

Kwa nyoyo zenye subira na matarajia mema, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Jordan inamuomboleza mbebaji da’wah, mmoja wa Mashababu wake wema, safi na mchamungu, na wala hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu, kutoka kizazi cha kwanza cha Hizb ut Tahrir, Al-Ustadh mwema:

Al-Hajj Muhammad Naeem Hasan (Abu Usamah Zakranah)

Ambaye aliregea kwenye rehma za Mwenyezi Mungu Mtukufu mnamo Jumapili asubuhi, 09 Muharram 1444 H sawia na tarehe 7 Agosti 2022 M, ambaye alitumia maisha yake kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah kwa bidii na subira, kwa ahadi na kubeba ulinganizi, licha ya madhara na dhiki aliyokumbana nayo.

Mwenyezi Mungu amrehemu muheshimiwa ndugu Abu Usamah. Alikuwa mpole, mpenda dawah na Mashababu wake, mtenda kazi mwaminifu, mwenye msimamo juu ya haki, na akiifurahia ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amsamehe na amrehemu na amkusanye pamoja na Manabii, wakweli, mashahidi na watu wema katika Pepo za neema, na hao ndio marafiki bora zaidi, na tunamuomba Mwenyezi Mungu aijaaliye familia yake subira, utulivu na faraja njema.

Ewe Mwenyezi Mungu, mrehemu ndugu yetu Abu Usamah, yakirimu makaazi yake, panua mlango wake, na umweke makaazi mazuri zaidi kuliko makaazi yake, na familia bora zaidi kuliko familia yake, na utukusanye sisi na yeye chini ya bendera ya Mtume wako Siku ya Kiyama.

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

- Kalima ya Ustadh Bilal Al-Qasrawi katika mazishi ya Haji Abu Osama Zakarneh, Mwenyezi Mungu amrehemu -

- Kalima ya Dkt Hassan Abu Abed katika Kikao cha Tanzia ya Hajj Abu Osama Zakarneh, Mwenyezi Mungu amrehemu -

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu