Ijumaa, 24 Shawwal 1445 | 2024/05/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  21 Rajab 1445 Na: 1445 / 11
M.  Ijumaa, 02 Februari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Muungano wa Tawala za Kiarabu... Ushirikiano katika Dhambi, Uvamizi na Usaliti hayatasababisha Kubakia Hai kwa umbile la Kiyahudi wala kwa Wakoloni Makafiri wa Kimagharibi
(Imetafsiriwa)

Haikutarajiwa kwamba tawala za Waarabu zingewanusuru pasi na shaka watu wa Gaza kwa majeshi yao yaliyowekwa kambini, na labda hilo ni bora zaidi. Huenda Mwenyezi Mungu anachukia kutaharaki kwao, basi akawazuia. Lau wangetoka wasinge wazidishia chochote mujahidina kati umadhubuti na ushujaa isipokuwa kuchanganyikiwa. Wangefanya kula njama na washirika wao, Mayahudi na Wakristo, wakitaka kuzusha fitna baina yao. Au pengine, wangetafuta hisa katika ushindi uliofikiwa na watu thabiti na imara wa Gaza, nyuma ya wapiganaji wa Mwenyezi Mungu wenye ikhlasi. Tunawachukulia kuwa hivyo. Shaka ingetokea kuhusu kuanguka kwa watawala hawa madhalimu mikononi mwa maadui zao.

Tawala hizi dhaifu na za wasaliti zilikaa kimya, mithili ya wafu, mbele ya mambo ya kutisha ambayo yalichochea hisia za watu kote ulimwenguni. Hata hivyo, ilitarajiwa na kubakia kuwa ni wajibu kwamba fahari na adhama ndani ya majeshi ya Ummah vinapaswa kusonga na kushinda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wao, kupigana sako kwa bako na watu wa Gaza.

Badala yake, tawala hizi hufanya mikutano ya hadhara na ya siri na viongozi wa Kimagharibi wa Kimarekani na wa Ulaya. Wanakutana kwa mazungumzo ya diplomasia kwa kuihudumia Marekani na Ulaya, wakijadili jinsi ya kuwatawala watu wa Palestina, kutatua kadhia ya Palestina, kulipa nguvu umbile la Kiyahudi, licha ya ukatili na uhalifu wake, na kufikia maslahi ya kisiasa, kijeshi, usalama na kiuchumi ya dola za kikafiri za kikoloni za Kimagharibi - Marekani, Uingereza, na Ulaya. Wanalenga kutilia nguvu ushawishi wao na uungaji mkono kwa umbile la Kiyahudi.

Kwa hivyo, miungano na mikutano kati ya viongozi wa nchi za Kiarabu na mawaziri wao, iwe ya pande mbili au ya pande nyingi, katika Mashariki ya Kati hutokea mara kwa mara na kufifia. Miungano hii mara nyingi inaundwa na kuamuliwa na ushindani wa kikanda, uingiliaji kati wa kimataifa, na mapambano makali ya ushawishi kati ya dola zenye nguvu za kikoloni za Kimagharibi, zikiongozwa na Marekani, Uingereza, na Ufaransa. Mahusiano baina ya nchi za kibepari yameegemezwa kwenye mapato na maslahi, na yalichukua mkondo mkubwa baada ya vita vya Gaza kuzusha hisia na machafuko katika misimamo ya nchi hizi, ambayo haikuwa sehemu ya mapato yao ya kisiasa ya ulaji njama dhidi ya Umma. Mipango hii hapo awali ililenga usalama, kukabiliana na ugaidi, usalama wa kawi, ushirikiano wa viwanda, biashara, na ujenzi, yote yakilenga kuiwezesha Marekani, washirika wake, na umbile la Kiyahudi.

Tovuti ya habari ya Axios ilifichua mkutano wa siri wa maafisa wakuu wa usalama wa kitaifa kutoka Saudi Arabia, Jordan, Misri na Palestina jijini Riyadh siku kumi zilizopita. Mkutano huo ulilenga kuratibu mipango ya siku moja baada ya kumalizika kwa uvamizi wa Gaza, kujadili njia za kuishirikisha Mamlaka ya Palestina katika utawala. Vyanzo hivyo viliiambia tovuti hiyo kuwa "mkutano huo jijini Riyadh uliandaliwa na Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Saudia Dkt. Musaed bin Mohammed Al-Aiban." Washiriki wengine ni pamoja na Majed Faraj, Mkuu wa Huduma ya Ujasusi ya Palestina, mwenzake wa Misri Abbas Kamel, na Meja Jenerali wa Jordan Ahmad Husni. Chanzo kimoja kilitaja kwamba "Wasaudi, Wamisri na Wajordan walimjulisha Faraj kwamba Mamlaka ya Palestina inahitaji kufanya mageuzi makubwa ili kuhuisha uongozi wake wa kisiasa." Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Saudia alisisitiza wakati wa mkutano huo kwamba "Ufalme huu unasalia na nia ya kusonga mbele katika uhalalishaji mahusiano na 'Israeli'."

Katika mkutano mwingine, Mkurugenzi wa Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA), William Burns, alifanya mazungumzo katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, na Waziri Mkuu wa Qatar, Mohammed bin Abdulrahman, na mkuu wa upelelezi wa Misri, Abbas Kamel. Mkutano huo pia ulihusisha mkuu wa Mossad. Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar alisema kuwa dori ya Qatar ni upatanishi, si kutia shinikizo kwa pande husika, akisisitiza kuwa Qatar haina ushawishi juu ya mtu yeyote.

Katika ilani nyingine, New Arab (Al-Araby Al-Jadeed) iliangazia mkutano mmoja uliofanyika mnamo Jumatatu jioni kati ya maafisa wakuu kutoka Idara ya Ujasusi ya Misri na viongozi wa Hamas ambao wamekuwa Cairo kwa siku kadhaa. Madhumuni ya mkutano huo yalikuwa ni kukabidhi makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa Paris kwa ujumbe wa Hamas na kujadili maoni ya awali ya harakati hiyo.

Mkutano wa hivi majuzi wa pande tatu kati ya Misri, Jordan na Palestina ulifanyika katika mji wa Aqaba, ukilenga kutafuta mbinu ya kivitendo ya kutatua mgogoro wa Gaza. Mkutano huo ulisisitiza kukataliwa kwa watu kuyahama makaazi yao, na kutaka kusitishwa kwa mapigano, na kutaka kuwezesha kupitishwa kwa misaada. Mfalme Abdullah alizuru Misri mara tatu baada ya vita vya Gaza na kuwakaribisha Rais Sisi na Abbas katika kile kinachojulikana kama Mkutano wa Aqaba.

Mawasiliano na ziara nyingi za wanasiasa wa Marekani, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Blinken, Waziri wa Ulinzi Austin, na Mshauri wa Usalama wa Kitaifa, zimefanyika Mashariki ya Kati na umbile la Kiyahudi. Ziara hizi ni sehemu ya msaada usio na kikomo wa kijeshi kwa umbile hilo. Hata hivyo, pia zinahusisha shinikizo la kisiasa kwa viongozi wa mrengo wa kulia katika serikali ya Netanyahu, kwenda sambamba na maagizo ya Marekani kwa viongozi wa kanda hiyo ndani ya mfumo wa suluhisho la dola mbili na kudumisha usalama wa kudhalilisha, jeshi, na msaada wa vifaa kwa umbile hilo lililoshindwa.

Kuhusiana na mikutano, miungano, na ziara hizi za tawala za Kiarabu, nukta zifuatazo zinaweza kuangaziwa:

- Kuegemea kwa tawala za Kiarabu juu ya ushirikiano wao na Marekani na Ulaya ni udanganyifu na uhadaifu. Itawageukia wao na umbile la Kiyahudi kwa maangamivu na kuvunjwa moyo, kutokana na mwamko wa Ummah na kuwafahamu kwake maadui zake. Wakati umekaribia ambapo watatoweka, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

- Miungano hii haitatoa suluhu za utiifu katika kusuluhisha suala la Palestina au kuanzisha suluhisho dhahania la dola mbili. Wala haitasababisha makubaliano yoyote baina ya nchi mbili au ya kikanda kati ya Mayahudi, Magharibi, na serikali zinazoshirikiana nazo, iwe ya kuhalalisha mahusiano, ya kiuchumi, kijeshi, au makubaliano ya usalama.

- Miungano na mikutano hii haijawahi kuwa kwa maslahi ya watu wa tawala hizi dhaifu na haitakuwa ya msaada kwa watu wa Gaza katika makabiliano yao ya kishujaa. Tawala hizi zinakula njama ya kuwafilisi ili kutumikia mashini ya vita ya ‘Israel’. Misri inafunga kivuko cha Rafah ili kuzuia misaada, na kuvuka kunahitaji kulipa maelfu ya dolari kwa makampuni ya kijasusi ya Misri. Jordan inashirikiana na Dola za Ghuba na Saudi Arabia kulisaidia umbile la Kiyahudi, kutoa njia mbadala kwa bidhaa kupitia Dubai, Makka, na maeneo ya Jordan na Palestina yanayokaliwa kwa mabavu.

Zaidi ya hayo, Jordan hupokea shehena za silaha za Kimarekani zilizokusudiwa Mayahudi na kuwasambazia mboga na matunda, nk.

- Kushindwa kwa umbile la fedheha la Kiyahudi mnamo Oktoba 7, 2023, na kushindwa kwake baadaye na mujahidina mashujaa kumeacha alama ya kudumu kwenye dhamiri ya taifa zima. Litafutiliwa mbali tu kupitia vita vya mwisho katika kulitokomeza kutoka kwenye mizizi yake.

- Marekani na Ulaya, na wale wanaozunguka mzunguko wao kwa madhambi yao, uchokozi, na matamko yao, ndio maadui wakubwa wa Umma wa Kiislamu. Hili liko imara katika akili za watu na uhusiano wowote nao utakuwa tu hali ya vita. Askari wao na kambi zao zimetawanyika katika ardhi za Kiislamu havitawanufaisha, kwani kambi hizi zilianzishwa kupitia kushirikiana na watawala wa Waislamu.

- Watawala wa Waislamu wenyewe wanang’ang’ana kubakia hai, na muungano wao na maadui wa Ummah na mikutano yao ya mara kwa mara ni thibitisho la ukubwa wa hofu yao na kutikiswa kwa viti vyao vya utawala ambao wanaamini kimakosa kwamba Mayahudi na Magharibi wanawazuia kutokana na kuanguka kwao kanako karibia, na wanashindwa kujifunza kutoka kwa wale walioanguka kabla yao.

- Ulimwengu mzima umeinuka dhidi ya vitendo viovu vya Mayahudi na misimamo mibaya ya Marekani na Ulaya. Yale yanayoitwa mashirika ya kimataifa na taasisi halali zinatamani sana mabadiliko katika mfumo huu mbovu na wa kishetani wa kimataifa. Mabadiliko pekee ya kweli yatakuwa ni kwa njia ya kuregea kwa fikra msingi katika Uislamu, Dini iliyoteremshwa na Mola wa walimwengu wote, yenye kupangilia maisha ya mwanadamu kwa mujibu wake.

- Licha ya kuporomoka kwa ubepari mbovu na demokrasia ya uwongo kutoka katika akili na nyoyo za watu kote duniani, lazima ziwepo juhudi za kuregesha Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume, ili kusimamisha Dini kama Mtume (saw) alivyofanya mjini Madina Al-Munawwara. Dola kandamizi za kikafiri zinahitaji dola kama hasimu ili kuzipindua na kubadilisha mfumo wa kilimwengu kuwa ule unaofikia uadilifu na usawa.

Huku usaliti wa watawala hawa makhaini unavyodhihirika, matumaini ya Umma leo yapo kwa watu wake wenye nguvu na uwezo na yanajifunga kwa kila mwanajeshi wake. Ni lazima wachukue hatua ya kupigana na Mayahudi huko Gaza na Palestina, kwani wamepitiliza katika ufisadi, mauaji, na uharibifu huko. Kuweni washirika wa Mwenyezi Mungu na kuweni mithili ya mashujaa miongoni mwa Maswahaba, na mashujaa wa Umma, kama Salah al-Din, Qutuz, na Baybars.

[إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ]

“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi” [Ghafir:51]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu