Jumapili, 11 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  16 Jumada I 1445 Na: 1445/07 H
M.  Alhamisi, 30 Novemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mfumo wa Kibepari: Janga Juu ya Majanga

(Imetafsiriwa)

Makumi ya maelfu ya watu kote nchini wameathiriwa na mvua kubwa, mafuriko na maporomoko ya ardhi. Kenya, ikiwa ni pamoja na Pembe ya Afrika imekumbwa na mvua kubwa inayohusishwa na hali ya hewa ya El Nino katika wiki za hivi karibuni iliyosababisha vifo vya makumi ya watu, ikiwa ni pamoja na zaidi ya 100 katika maeneo mbalimbali ya Kenya. Uharibifu mkubwa wa nyumba na barabara umetokea. Hizb ut Tahrir / Kenya ingependa kutaja yafuatayo:-

Tunahuzunishwa na vifo vya watu na uharibifu wa mali na kwa haya tunatoa wito kwa jamii nzima ya Kenya na hasa Waislamu kuweza kutoa misaada kwa wahanga kwani hili ni miongoni mwa mambo yanayohimizwa na Uislamu. Mtume Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie alisema:

«مَنْ فَرَّجَ عَنْ مُسْلِمٍ كُرْبَةً، فَرَّجَ اللَّهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرُبَاتِ يَوْمِ القِيَامَةِ »

“Yoyote atakayemuondoshea Muislamu dhiki yoyote ile basi Mwenyezi Mungu atamuondoshea dhiki miongoni mwa dhiki za siku ya Qiyama.”

Majanga kama haya yanapotokea, hutulazimisha kutambua udhaifu wa wanadamu na kuthibitisha uwezo wa Mwenyezi Mungu (swt) Muumbaji wa Mwanadamu, Uhai na Ulimwengu. Huu ni ushahidi wenye nguvu wa kuthibitisha kwamba kimaumbile mwanadamu, mwenye mipaka yuko chini ya nguvu zilizo nje ya uwezo wake hivyo huhitajika na kuwa na mwongozo wa Muumba wake Mwenyezi Mungu unaosimamia mambo yake yote maishani utakaomdhaminia ufanisi mkubwa.

Mafuriko hayo yameonyesha wazi kushindwa kwa uhandisi wa miundombinu kutokana na ufisadi wa kisiasa ambao umeathiri kabisa ujenzi huo. Kwa muktadha huu, idadi ya watu kwa ujumla itabeba mzigo maradufu wa ushuru na ujenzi duni kutokana na ufisadi.

Mara nyingi majanga hayo yanapotokea, hudhihirisha hali halisi ya itikadi ya kimatata ya kibepari na mifumo yake ya utawala ya kutopeana kipaumbele kwa maslahi ya umma. Lakini la ajabu kwenye michakato ya kuwania madaraka, wanasiasa wa kibepari huzunguka nchi nzima kwa helikopta kutafuta kura huku kwenye mafuriko wanakodolea macho televisheni raia wanapo kufa maji!  Hii ndiyo taswira halisi ya ubepari na viongozi wao wanaothamini maslahi yao kibinafsi na kutojali maisha ya maskini.

Mwisho wa yote ni kwamba serikali ndio inayopaswa kunyoshewa kidole cha lawama kwa kutepetea juu ya usalama wa watu kwani ilipaswa kuchukua hatua za tahadhari kwa kuweka taratibu maalum kama njia ya kupunguza athari hizo za maafa pamoja na hatua za haraka za kuwaokoa watu.

Uislamu kama mfumo kamili wa kimaisha umeanisha kwamba jukumu la kusimamia mambo ya umma kimsingi ni la serikali na wala sio kwa raia au mashirika ya kibinafsi. Mtume Muhammad Rehema na Amani Zimshukie alisema:

«الإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»

“Imamu/ Kiongozi ni mchungaji na ni mwenye kuulizwa juu ya wale anaowachunga.”

Kuhusu majanga kama mafuriko, Uislamu umemuamuru kiongozi kutumia fedha kutoka hazina (Baitul Mal) kuwahudumia raia walioathirika na hili ni jukumu lake juu yao wala sio fadhila kwao. Ikitokea hakuna fedha kwenye hazina ya serikali, basi kiongozi analazimika kuwatoza tajiri kiasi maalum cha kodi ili kufidia hali hiyo. Na hivi ndivyo Khilafah inavyotazamiwa kusimamia maslahi ya raia wake Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi Kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu