Jumapili, 11 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  6 Safar 1445 Na: 1445 / 06
M.  Jumanne, 22 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali Inachapisha Mabilioni ya Noti za Sarafu ambazo Zinachochea Moto wa Mfumko wa Bei, na Kisha Kumwaga Machozi ya Mamba huku Watu Wakichomeka ndani ya Moto wake!

(Imetafsiriwa)

Bei ya umeme imeongezeka kwa Rupia 18 kwa kila kipimo tangu Julai mwaka jana. Leo umeme, pamoja na ushuru, ni Rupia 50 kwa kila kipimo. Bei za petroli zinagusa Rupia 300 kwa lita. Kiwango cha mfumko wa bei kiko kiwango cha juu katika historia ya Pakistan. Dola ya Pakistani inahusika na kuchochea moto wa mfumko wa bei. Inakidhi upungufu wake wa bajeti kwa kuchapisha noti za sarafu. Ni kwa gharama ya watu kujiua, kuua watoto, njaa na umaskini, na pia kunyimwa afya na elimu.

Matumizi ya bajeti ya serikali ya majimbo ni bilioni 14500. Lakini, mapato ya bajeti ni bilioni 9200. Matokeo yake, Benki Kuu ya Serikali inachapisha noti za sarafu na inakopesha benki za biashara kwa riba. Serikali yenyewe inakopa kutoka mabenki, kwa kiwango cha juu cha riba. Hivi ndivyo upungufu wa bajeti unavyofadhiliwa. Huku benki zikifaidika, watu wanabeba athari ya miamala hii ya riba. Kutokana na uchakavu wa pesa, bidhaa na huduma sasa ni ghali zaidi. Mfumko wa bei ni wizi kutoka kwa mifuko ya watu.

Sarafu ya sasa ya karatasi ya Pakistan isiyo na maana na thamani ya dhati ni chombo tu ubadilishanaji. Haina thamani ya ndani yake. Kwa kuchapisha zaidi, hakuna ongezeko la utajiri halisi wa nchi. Utajiri wa halisi unatoka kwa bidhaa, uzalishaji na huduma. Ikiwa hizi hazitaongezwa, basi kuchapisha pesa utaongeza tu kiasi cha pesa. Bidhaa na huduma sasa zitanunuliwa kwa pesa zaidi na nchi itateseka kutokana na mfumko bei. Chini ya serikali ya PTI, deni liliongezeka kwa rupees trilioni 18 kutoka Agosti 2018 hadi Machi 2022. Chini ya serikali ya PDM, deni liliongezeka kwa trilioni 18.5 katika miezi 15 pekee. Katika kipindi hiki, ongezeko la pato la taifa halikuwa hata 15%. Kwa hivyo, ongezeko kubwa la sarafu limeunda dhoruba ya mfumko wa bei.

Uislamu huondoa nguvu ya serikali katika uchapishaji pesa wakati wowote inapotaka na kupata riba. Katika Uislamu, utoaji sarafu iliyoegemezwa kwa dhahabu na fedha sio chaguo, ni jukumu. Serikali haiwezi kutoa sarafu isipokuwa serikali iwe na kiasi sawa cha dhahabu au fedha. Kwa njia hii, mfumko wa bei unamalizika. Wizi wa mara kwa mara kutoka kwa mifuko ya watu hukoma. Utukufu wa mali ya watu unalindwa. Sarafu, bei na uchumi huwa thabiti.

Baada ya kusimamishwa kwake, Khilafah kwa Njia ya Utume itasitisha malipo yote ya riba. Haya yanajumuisha riba bilioni 7,500 juu ya mikopo ya shirikisho, mamia ya mabilioni ya riba juu ya deni la mviringo, riba juu ya mikopo iliyopatikana kwa ununuzi wa bidhaa na riba juu ya mikopo ya kigeni. Khilafah atapata ustawi kupitia mfumo wa kipekee wa ugavi wa rasilimali na kizazi cha utajiri ndani ya dola. Haitakabiliwa na nakisi yoyote ya kifedha. Haitalazimisha mzigo wowote usiofaa kwa watu. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Surah Taha 20:124].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu