Jumamosi, 25 Shawwal 1445 | 2024/05/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  22 Jumada I 1445 Na: BN/S 1445 / 09
M.  Jumatano, 06 Disemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali Vibaraka Zinalipa Uhai Umbile la Mayahudi. Usaliti wa Siri sasa Umekuwa wa Dhahiri!
(Imetafsiriwa)

Chini ya kichwa, "Kuendesha daraja la ardhini kati ya bandari za Haifa na Dubai, kupita Saudi Arabia na Jordan, kuvipita vitisho vya Mahouthi," wavuti ya arabi21.com uliripoti, ukitoa mfano wa Vyombo vya habari vya Kiebrania, kwamba, "Imarati (UAE ) na dola inayokalia kimabavu zilitia saini makubaliano ya kuendesha daraja la ardhini, kati ya bandari za Dubai na Haifa, likipitia katika eneo la Saudia na Jordan, kwa lengo la kuvipita vitisho vya Mahouthi vya kufunga njia za kupitia meli. Tovuti za Kiebrania ziliripoti kwamba "Kampuni ya Israel" Traknet ilikuwa imeanza kuendesha daraja la ardhini kutoka bandari ya Dubai, kupitia Saudi Arabia na Jordan, hadi bandari ya Haifa, ili kuondokana na vitisho vya biashara ya baharini katika Bahari Nyekundu."

Maelezo ya usaliti, licha ya uhalisia wake, hayatoshi tena kuelezea msimamo wa serikali vibaraka kwa Palestina, watu wake, na yote yanayotokea ndani yake. Na kwa usaliti huja njama. Usaliti ulikuwa wa siri. Sasa umekuwa dhahiri. Hizo ndizo serikali za uhaini. zinakwea usaliti kama huo, badala ya kunyosha mkono wa misaada na nusra kwa watu wa Palestina, hata wakati wanakabiliwa na uhalifu na mauaji ya halaiki mikononi mwa umbile la Kiyahudi. Wanafanya hivyo, badala ya kukata bahari, ardhi, na anga za ulimwengu, kuzuia usambazaji wa mafuta, na kutumia nguvu zao zote kuzuia umwagaji damu, wakati wanao uwezo wa kufanya hivyo. Isipokuwa majeshi ya Waislamu yasonge, wakati meli za Magharibi zimeshaingia kulisaidia umbile la Kiyahudi, serikali hizi badala yake zinalipa uhai njia umbile la Mayahudi ili kupata biashara yake, na barabara ya ardhini, inayokwepa njia za bahari zilizotishiwa, kwa njia ya usambazaji, kupitia daraja la ardhini, kutoka UAE hadi bandari ya Haifa.

Katika wakati ambapo mzingiro unaimarishwa pambizoni mwa Gaza, huku ikikabiliwa na uharibifu, kwa kukatwa kwa maji na vyakula kwa Gaza, serikali za wasaliti zinatafuta kupata njia mpya ya kulisambazia umbile dhaifu linaloporomoka la Kiyahudi. Hii ni kama walivyohakikisha njia za uhai kwa umbile la Kiyahudi hapo awali, wakati walipounda ngao ya kinga pambizoni mwake, kama kikwazo dhidi ya watoto wa Ummah wa Kiislamu, ili wasiweze kuuondoa uvamizi huo. Serikali hizi zinapambana na watoto wa Ummah wenyewe, kuzuia mikono yao, na kuwafungia ndani ya mipaka ya kitaifa. Leo, wanahakikisha kuendelea kuwa hai kwa umbile la Kiyahudi, na hata kuliunga mkono katika kutekeleza uhalifu wake dhidi ya watu wa Palestina. Kutojali kwa serikali hizi damu ya Waislamu kumefikia kilele chake. Hawana tena msitari mwekundu, isipokuwa kwa kubakia hai viti vyao vibovu vya enzi, vilivyolaaniwa.

Serikali hizi zote zinahusika katika uhaini, kuhakikisha kutawala kwa umbile la Mayahudi juu ya watu wa Palestina. Hakuna tofauti kati ya serikali ya Misri inayoizunguka Gaza, na serikali ya Uturuki inayolisambazia umbile la Mayahudi na mafuta na chakula. Hakuna tofauti kati ya serikali zinazotafuta kulilinda umbile la Kiyahudi kwa daraja la ardhini, kuanzia serikali ya Imarati ambayo inampiga vita Mwenyezi Mungu (swt), Dini yake, na waumini, kupitia serikali ya uasherati katika Ardhi ya Misikiti miwili mitakatifu, na kumalizikia na serikali ya Jordan, serikali iliyoundwa na Waingereza ili kuwa kaka mapacha wa umbile la Kiyahudi, kama mlinzi wa mipaka yake pamoja nalo, katika historia ndefu ya kujisalimisha, usaliti, ushirikiano na njama.

Enyi Waislamu, Enyi Maafisa, na Enyi Watu wa Nguvu katika Ummah:

Sio siri tena kwenu kwamba serikali hizi na umbile la Mayahudi zote gora moja, katika msaada wa pamoja. Uhai wake ni sehemu ya uhai wao. Kufariki kwake ni sehemu ya kufariki kwao. Serikali hizi zinamsaliti Mwenyezi Mungu (swt), Dini yake, na Mtume wake (saw). Ni waaminifu kwa watu wenye uadui zaidi, ya watu wote, kwa waumini. Haya yote hayaliokoi umbile la Mayahudi kutokana na hatima yake isiyoweza kuepukika. Badala yake, haya yote yalinalaani wenyewe kwa maangamivu yake wenyewe, pamoja na maangamivu yao. Hii ni kwa sababu ufisadi na uhalifu wake unahesabiwa kama wao. Hii ni kama vile ufisadi wao unahesabiwa kama ufisadi wake. Ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) inakuja kutimizwa, kuhusu wale wanaowafuata Mayahudi na Manaswara hadi akawa mmoja wao, na akashirikiana pamoja nao, kama vile serikali hizi zinavyofanya sasa. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَى أَن تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ فَعَسَى اللهُ أَن يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِّنْ عِندِهِ فَيُصْبِحُوا عَلَى مَا أَسَرُّوا فِي أَنفُسِهِمْ نَادِمِينَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. * Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo kwake wakawa wenye kujuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao.” [Surah Al-Maaidah 5:51- 52].

Basi kuweni wafuasi wa Answar wa Mwenyezi Mungu (swt), na mkono wa haki unaoivunja batili. Wapindueni watawala hawa wasaliti. Jikomboe ili muikomboe ardhi ya Isra ya Mtume wenu (saw). Wapeni nusra ndugu zenu, huku Mwenyezi Mungu (swt) yuko pamoja nanyi na hatayapitisha patupu matendo yenu mema.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu