Ijumaa, 24 Shawwal 1445 | 2024/05/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  13 Rajab 1445 Na: 1445 / 19
M.  Alhamisi, 25 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali Iliyofeli katika Kila Kitu Isipokuwa katika Usababishaji Umaskini na Ukusanyaji Pesa za Haramu!
(Imetafsiriwa)

Waziri wa Fedha Jibril Ibrahim, kwa mara ya tano mfululizo, aliongeza kwa ujasiri bei ya dolari ya forodha, ambayo ilianza kuongezeka mnamo Juni 2021, kutoka pauni 28 hadi pauni 370, kisha hadi pauni 445, kisha hadi pauni 564, kisha hadi pauni 650. Hatimaye, hadi pauni 950!! Sababu ya kwanza ya hatua hiyo ilikuwa ni mojawapo ya mahitaji ya mageuzi ya kiuchumi, kuongeza mapato, na kuleta utulivu wa kiwango cha ubadilishaji wa pauni ya Sudan dhidi ya dolari ya Marekani. Uzoefu wa kivitendo ulithibitisha kutofaulu kwa sera hii. Hali ya uchumi haikuimarika, wala kiwango cha ubadilishaji fedha hakikutengemaa. Badala yake, kinyume kabisa ndicho kilichotokea. Kiwango cha ubadilishaji wa dolari kiliongezeka kutoka pauni 47 hadi kufikia pauni 600 kabla ya vita, na sasa imezidi pauni laki tatu na moja.

Ufisadi wa tawala hizi za vibaraka umedhihirika, ambao uliifanya Sudan, ambayo ni tajiri kwa utajiri wake wa dhahiri na uliofichika, ukiporwa na wakoloni wa makafiri kupitia mikopo iliyoharamishwa ya riba na kile kinachoitwa uwekezaji wa kigeni, hivyo kuwafukarisha wananchi. Kisha vita hivi vya laana vikawasshwa katika utekelezaji wa ajenda ya kafiri mkoloni Magharibi.

Serikali hii iliyofeli imefeli kwa kila kitu isipokuwa kusababisha umaskini na kukusanya fedha haramu. Ilishindwa kutekeleza wajibu wake wa kulinda usalama wa watu na kuwakabidhi kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka, hali iliyosababisha umwagaji damu, ukiukaji wa heshima, wizi wa fedha na uharibifu wa mali, yote hayo na mengine mengi yaliathiri watu wasio na hatia na wasio na ulinzi wa Sudan.

Kuongeza zaidi mateso ya watu waliochoshwa na vita, serikali inapandisha bei ya bidhaa za kimkakati. Kwa kuongeza bei ya dolari ya forodha, ambayo iliakisiwa moja kwa moja katika kupandisha bei ya unga wa mkate, na bei ya mtungi wa gesi ya kupikia imepanda mara tatu, na hakuna faraja kwa watu wa Sudan!

Kupandisha bei ya dolari ya forodha, pamoja na kuongeza mateso ya watu, ni haramu kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, kwani Uislamu umeharamisha ‘sahib maks’, maana yake ni mtu anayetoza watu ushuru, (forodha). Mtume (saw) amesema: «لَا يَدْخُلُ الْجَنَّةَ صَاحِبُ مَكْسٍ» “Haingii Peponi mtoza ushuru.”

Hakuna wokovu kwetu isipokuwa kwa kuwaondoa hawa mabepari vibaraka na kusimamisha jengo kubwa la Uislamu. Khilafah Rashidah ya pili kwa Njia ya Utume, ili maisha salama na yenye utulivu yarudi.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal 8:24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu