Ijumaa, 24 Shawwal 1445 | 2024/05/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  6 Shawwal 1445 Na: 1445 / 07
M.  Jumatatu, 15 Aprili 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mafuriko ya Rufiji Yametengenezwa

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir Tanzania kwa unyenyekevu mkubwa inatoa mkono wa rambi rambi na kuwafariji wahanga wote wa mafuriko yaliyotokea katika wilaya za Rufiji na Kibiti, mkoani Pwani.

Kufuatia balaa la mafuriko hayo yalioathiri uhai, kuharibu makaazi 23,000, kuangamiza ekari 33,930.24 za mazao, kuleta wahanga 88,000 wanaohitaji misaada muhimu na zaidi kusambaratisha shughuli za kijamii na kiuchumi, upande wetu Hizb ut Tahrir Tanzania tungependa kuweka bayana yafuatayo:

a. Mafuriko haya ni ya kutengezwa kutokana na mapungufu ya mfumo wa kiufundi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere. Lakini kunaambatana na hali ya uzembe na utovu wa uwajibikaji wa wanasiasa. Kwa kuwa ndani ya mwezi Machi 2024 bwawa lilikuwa limeshajaza maji kiwango cha 164.8 cubic meters sawa na lita 14.6 milioni, katika hali ambayo bwawa halikuwa na uwezo tena kubeba maji katika hifadhi yake, matokeo yake likalazimika kuyamwaga maji ziada, hali iliyopelekea Mto Rufiji kutapika na kupelekea mafuriko kwa wakaazi wa pembezoni mwake. Ama uzembe na utovu wa uwajibikaji, haya yanadhihirika, kwa kuwa jopo la ufundi wa bwawa hilo lilionya awali juu ya ujio wa balaa la mafuriko. Walichokifanya wanasiasa ni kusubiria kutoa huduma za misaada, badala ya kuchukua hatua za kuzuia au kuhamisha watu.

b. Mafuriko haya ni kielelezo cha wazi kwamba chini ya mfumo wa ubepari, miradi hususan mikubwa haipo kwa ajili ya kutumikia maslahi mapana ya raia, bali ipo kwa ajili ya maslahi ya mabepari na wanasiasa waroho, wakikosa kushughulishwa na chochote katika maisha ya raia. Mradi huu mkubwa na mingine mfano wake ambayo imepachikwa jina kuwa ni ‘miradi ya kimkakati’ ati ikilengwa kuwasaidia watu. Cha kushangaza! hata kabla ya mradi kuanza kazi, tayari umeshaangamiza maisha ya watu, mali zao, na kuvuruga kabisa shughuli zao za kilimo cha ‘kijungu mwiko’ (cha kimaskini).

c. Mataifa yanayoendelea, licha ya kudai yako huru, ukweli ni kuwa katika miamala yao bado yanaogelea mle mle katika nyayo za wakoloni. Miradi ya kikoloni haikuwa ikilengwa kwa ajili ya maslahi ya wenyeji na maeneo yaliyoizunguka, bali ililengwa kufikia maslahi ya kiuchumi ya wakoloni.

d. Rasilmali zilizokosa uoni mpana wa kimfumo haziwezi kamwe kuleta tija kwa ajili ya ustawi mpana wa maisha ya watu. Afrika ina hazina kubwa ya rasilmali zinazoweza kuboresha maisha ya watu kijamii na kiuchumi, lakini kwa kukosekana mfumo huru, rasilmali hizo zinamalizia kuporwa na unyonyaji wa mabepari wa Kimagharibi, na makombo kuingia katika mifuko ya wanasiasa waroho. Mto Rufiji una hazina kubwa ya maji, ukirefuka kwa masafa ya kilomita 600, na bwawa lake ni la tatu kwa ukubwa ndani ya Afrika, kwa masikitiko hata halijaanza kazi iliyokusudiwa tayari limeshaleta maangamizi.

Mfumo wa ubepari kimaumbile umefeli katika msingi wake na nidhamu zake. Na ajenda yake kubwa ni maslahi na sio kujali na kuwatumikia watu. Ni Uislamu tu chini ya dola yake ya Khilafah ndio unaweza kwa dhati kuyasimamia mambo ya Ummah. Hii ni kwa sababu una nishati yenye nguvu ya kiroho iliyojengwa kufungamanisha matendo yote ya mwanadamu hapa duniani na maisha yajayo ya Akhera.

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi: Sultan Said

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu