Jumamosi, 10 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  1 Muharram 1440 Na: 1440/01
M.  Jumanne, 11 Septemba 2018

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wacha Mwaka Mpya wa Kiislamu Utushajiishe Zaidi Katika Majukumu Yetu

Tunatoa pongezi zetu za dhati kwa Ummah wetu mtukufu kwa kuwasili kwa mwaka mpya wa Kiislamu wa 1440 Hijri. Lakini, hali ,mbaya na ya uchungu ya Ummah wetu ulio barikiwa bado haijabadilika, hata inazidi kuwa mbaya.

Ummah wetu unamwagika mito ya damu nchini Yemen, Burma, Afghanistan, Palestina, Somalia, Syria nk. Ambapo kwa hivi sasa, nchini Syria katika mkoa wa Idlib mauwaji mabaya ya kikatili yanaendelea kutokana na njama za Uturuki na Iran, zikijumuisha Urusi.

Huku maangamivu haya yakiendelea watawala wa ulimwengu wa Kiislamu, kama ilivyo tarajiwa, wamefungia macho pasi na mipango yoyote kabambe ya kuzuia janga hili.

Kadhia ya kuanza kwa mwaka mpya wa Kiislamu inapaswa kuunganishwa na wajibu wetu na kubeba majukumu yetu barabara kama ilivyo hapa chini:

1. Utumizi barabara wa maisha ya dunia: Uislamu kama mfumo kamili na mpana haupuuzi maisha ya dunia, bali umeweka hukmu maalumu za kuamiliana nayo. Kwa kuanza kwa mwaka mpya ni wakati wa kupanga, kutenda na kukabiliana na changamoto kwa njia nzuri na kuboresha hali nzuri zaidi ikilinganishwa na mwaka jana. Mtu mwenye akili huifanya hali yake ya sasa kuwa nzuri zaidi kuliko iliyo pita.

2. Kujitayarisha kwa maisha ya Akhera: Kuanza kwa mwaka mpya yamaanisha kuwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa rehma zake ameturuzuku fadhila ya muda zaidi hapa duniani. Hivyo basi, tunapaswa kuitumia vizuri zaidi sehemu hii ya maisha haya ya muda kupitia kujifunga na maamrisho Yake na kujiweka mbali na makatazo Yake ili kumridhisha Yeye pekee kwa matarajio ya Pepo. Tunapaswa kuutumia muda vizuri hadi pumzi yetu ya mwisho, kwa kuwa pindi wakati unapo kwenda hauwezi kurudishwa.

3. Kubeba Ulinganizi (Da'wah) wa Kiislamu: Wakati wa Khilafah ya Umar ibn al-Khattwab katika mwaka wa 16 Hijri, Maswahaba (ra) wote kwa pamoja walikubaliana (Ijmaa) juu ya kulichagua tukio la hijra kama nukta kianzilishi ya mwaka wa kwanza wa Kiislamu, licha ya kuwepo kwa matukio mengi matukufu mengineyo yaliyo muhimu vilevile. Hii ni kwa sababu Hijra ni tukio la kipekee ambalo kwalo Uislamu ulihamishwa kutoka hatua ya kinadharia hadi hatua ya kutabikishwa kivitendo kupitia kuasisiwa Dola ya Kwanza ya Kiislamu mjini Madina, na dola hiyo iliendelea kutawala kwa makarne kwa mafanikio makubwa, hadi kuvunjwa kwake 1924 kupitia Uingereza kwa kushirikiana na usaidizi wa makhaini miongoni mwa Waturuki na Waarabu.

Ijmaa ya maswahaba ya kuchagua tukio la hijra kama nukta kianzilishi cha kalenda ya Kiislamu yaonyesha waziwazi kuwa ukombozi wa kihakika wa Ummah wetu utapatikana kupitia dola ya Kiislamu pekee. Kuanza kwa mwaka mpya kunapasa kuushajiisha Ummah wetu zaidi katika wajibu wetu mtukufu na kadhia nyeti ya kusimamisha tena Khilafah, ikianzia katika biladi kuu za Waislamu, kisha kueneza uongofu, nuru na uadilifu wake kwa wanadamu wote bila ya kuzingatia mataifa yao, rangi, dini au makabila. 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ﴿

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu