Jumamosi, 10 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  23 Shawwal 1444 Na: HTY- 1444 / 23
M.  Jumamosi, 13 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mamlaka za Mahouthi Zaendelea na Ukamataji wao wa Kidhulma dhidi ya Wabebaji Dawah ya kuregesha tena mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu katika Mashababu wa Hizb ut Tahrir
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Jumamosi, tarehe 16 Shawwal 1444 H sawia na 6/5/2023 M, mamlaka za Mahouthi zilimkamata Mhandisi Shafiq Khamis, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, mbele ya nyumba yake katika mji mkuu, Sana'a, bila ya mashtaka yoyote isipokuwa uanachama wake na Hizb ut Tahrir, ambayo inafanya kazi ya kurudisha tena mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu baada ya kutoweka kwake katika maisha ya Waislamu. Leo hii Waislamu wamegawanyika na kutawaliwa na tawala zinazoungwa mkono na nchi za Magharibi, huku wakikabiliwa na adhabu kali na kutawaliwa na mifumo ya kisekula. Kwa hivyo mamlaka za Mahouthi zatangaza kuendelea kwa vita vyao dhidi ya Dawah ya Kiislamu na wabebaji wake katika Mashababu wa Hizb, kwani hapo awali walimteka nyara Ndugu Abdullah Al-Qadi mnamo tarehe 27 Ramadhan 1444 H sawia na 18/4/2023 M, ambaye bado anazuiliwa nao hadi wakati huu. Tumefikia uhalisia ambapo wasaliti, maadui wa Umma wa Kiislamu, na wapotovu wa fikra na tabia wanaheshimiwa, huku watu wema wakifungwa jela.

Hizb ut Tahrir ni chama mashuhuri ambacho kilianzishwa mwaka 1372 H - 1953 M huko Al-Quds na Sheikh Taqiuddin al-Nabhani, Mwenyezi Mungu amrehemu, Amiri wake wa kwanza, na Amiri wake wa sasa ni mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah. Lengo kuu la Hizb ni kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, ili hukmu irejee kwa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu. Njia ya kubeba Dawah inatokana na hukmu za Shariah, kufuata njia ya Mtume (saw) katika kubeba Dawah yake, kwani ni wajibu kufuata. Hizb haipigii debe mbinu za kisilaha katika njia yake; bali inalenga kuhuisha Ummah kwa fikra angavu na inajitahidi kuuregesha kwenye izza yake ya awali, ambapo inachukua hatua miongoni mwa mataifa na watu, na dola ya kwanza duniani, kama ilivyokuwa, inayotawaliwa kwa mujibu wa hukmu za Uislamu. Hizb imeandika mbinu na njia na ruwaza yake kwa dola katika vitabu vyenye thamani, ambavyo inaviwasilisha kwa Ummah mchana na usiku, moja kwa moja na vinavyopatikana kwenye tovuti zake.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir na Mahouthi walikuwa ndani ya jela moja wakati wa utawala wa mwendazake Ali Abdullah Saleh, na leo hii, Mahouthi wanatekeleza dhulma ile ile waliyoifanya watawala waliotangulia! Hatima ya kila dikteta na dhalimu ni fedheha duniani na Akhera. Hivyo basi, ni wajibu kwa mamlaka za Kihouthi, ambao wanadai kuwa katika njia ya Qur'an, kufuta mifumo na sheria za Kikafiri nchini, badala ya kuwakamata Mashababu wa Hizb ut Tahrir!

Tunathibitisha kwamba sisi ni sehemu muhimu ya Ummah huu mtukufu, tunafanya kazi katika nchi hii na katika zaidi ya nchi 40 kote duniani. Ukamataji, kufunga jela na kunyanyasa hakutatuzuia kusonga mbele katika kufichua mipango ya wakoloni katika nchi za Kiislamu ikiwemo ardhi ya Yemen. Tunaendelea na njia yetu ya kufikia lengo na kuwafichua watawala wote wanaoshikilia mifumo hii maadamu hawaongozwi na sheria ya Mwenyezi Mungu, hata kama wanadai kinyume na hivyo, na tunapambana nao kwa misimamo yetu ya wazi dhidi ya kujiepusha kwao kutabikisha Shariah na kupuuza kwao mambo ya watu. Hizb itabaki kuwa chama kinachoongoza kisicho wadanganya watu wake na mlinzi mwaminifu wa Uislamu. Hivyo basi, tunawaalika wenye ikhlasi kufanya kazi nasi ili tupate izza hapa duniani na neema ya Akhera.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [Al-Nur: 55].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu