Jumamosi, 25 Shawwal 1445 | 2024/05/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 14/02/2024

Maoni ya habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli… Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, irudishe ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahuma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 04 Sha’aban 1445 H sawia na 14 Februari 2024 M

Usaidizi Usioyumba kwa Waislamu wa Kashmir pasi na Kuhamasisha Wanajeshi wa Pakistan ni Usaliti

Waziri mkuu wa muda na mkuu wa jeshi walionyesha "msaada wao usioyumba" kwa watu wa Kashmir, katika Siku ya Mshikamano wa Kashmir, 5 Februari. Waislamu wa Kashmir inayokaliwa kwa mabavu wako chini ya uvamizi wa kikatili wa Dola ya Kibaniani. Ni kwa kuandaa Jihad pekee kupitia vikosi vya jeshi la Pakistan ndio inaweza kuikomboa Kashmir. "Msaada usioyumba" hauna maana bila uhamasishaji wa jeshi la Pakistan. “Msaada kama huo usioyumba” hauwatii motisha Waislamu. Badala yake, unaitia motisha Dola ya Kibaniani kuumakinisha ukaliaji wake wa kimabavu, kwa kuwakandamiza wanawake, watoto na wazee wetu. Kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu ﷻ, Khilafah kwa Njia ya Utume itayahamasisha majeshi ya Pakistan. "Msaada wake usioyumba" utapelekea Takbira za ushindi na utekelezaji Swalah ndani ya Jamia Masjid huko Srinagar kupitia askari washindi.

27 Rajab 1445 H - 08 Februari 2024 M

Ongezeko la Bei ya Gesi kwa Mahitaji ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, lazidi kubimbirisha Moto

Kwa matakwa ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, Mamlaka ya Udhibiti wa Mafuta na Gesi imeongeza bei ya gesi kwa wastani wa 23% hadi Rupia 1,590 kwa kila mmbtu. Hili ni ongezeko la pili la bei katika kipindi cha miezi minne. Serikali iliongeza bei ikidai gharama za michezo za kampuni za gesi, gharama za upotezaji wa kesi, na kuweka vikomo vipya kwa hasara za laini. Mikutano ya hadhara ilidhibitiwa. Katika Khilafah kwa Njia ya Utume, dola itasimamia sekta ya kawi, sio taasisi za kikoloni. Kusudi lake sio kukusanya ushuru usio wa moja kwa moja au kuwaadhibu watu kwa usimamizi mbaya na uzembe wa serikali. Ni kuwapatia wananchi gesi kwa bei nzuri.

28 Rajab 1445 H - 09 Februari 2024 M

Hata Baada ya Uchaguzi, Hakutakuwa na Mabadiliko. Uchaguzi haubadilishi Mfumo

Sokomoko ya uchaguzi hatimaye imekwisha. Utawala wa ukoloni juu ya serikali unabaki kama ilivyokuwa kabla ya uchaguzi. Uchaguzi ni zoezi la kutafuta mtu wa kuendesha muundo wa uliopo. Matokeo yanabainishwa katika wizi wa kura kabla ya upigaji kura. Matokeo ya siku ya uchaguzi kwa kawaida hayaleti tofauti kubwa, isipokuwa marekebisho madogo. Wakati umefika kwa Waislamu wa Pakistan kujitahidi pamoja na Hizb ut Tahrir, kwa ajili ya kusimamisha Khilafah, kwa ajili ya mabadiliko ya kweli. Waislamu lazima wawatake maafisa wa Jeshi la Pakistan kuung'oa mfumo wa sasa na kutoa Nusrah kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah. Hizb ut Tahrir imejitayarisha kikamilifu kuleta mabadiliko, na mpango kamili wa Kiislamu.

29 Rajab 1445 H - 10 Februari 2024 M

Damu ya Mashahidi inalilia Salahuddin wa Leo

Vikosi vinavyokalia kwa mabavu vya umbile la Kiyahudi vinawauwa kwa njaa na kuwachinja wanawake na watoto wasio na hatia ndani ya gereza la wazi la Gaza. Jumuiya ya kimataifa inatazama kwa ukimya, huku mauaji ya halaiki yakiendelea kwa zaidi ya miezi minne. Chombo cha wakoloni, Mahakama ya Kimataifa ya Haki, kinasalia kuwa tasa, wakati viongozi wa Magharibi, pamoja na vibaraka wanyakuzi ndani ya Ardhi za Kiislamu, wanafanya kazi kwa kuliunga mkono umbile la Kiyahudi. Watu madhulumu wa Palestina wanatamani Salahudin mpya ili kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina kutokana na wavamizi katili. Wakati umefika kwa majeshi ya Waislamu kukusanyika ili kunusuru Waislamu na Uislamu. Kwa hivyo je, mtazingatia, enyi maafisa wanyoofu katika jeshi la Pakistan?

01 Sha’aban 1445 H – 11 Februari 2024 M

Watu Hupata Hasara, Haijalishi ni Chama Gani Kitashinda Katika Uchaguzi wa Kidemokrasia

Mtu yeyote anayesema kuwa mabadiliko ya kweli yanawezekana kupitia chaguzi za kidemokrasia, kwa kujua au kutojua, anadanganya wananchi. Uchaguzi ni utaratibu wa kuhifadhi mfumo uliopo, sio kuubadilisha. Katika Demokrasia, uchaguzi huwa kama valvu ya shinikizo ambayo huondoa mfadhaiko kwa watu, kwa kubadilisha tu nyuso. Hii inaweka udhibiti mikononi mwa wakoloni na vibaraka waliowachagua, huku ni nyuso pekee zinazoendesha mabadiliko ya Demokrasia. Je, sivyo ilivyotokea katika chaguzi za hivi majuzi? Hivyo, kwa nini tusikatae munkari muovu wa demokrasia na kukamata maroof njema ya Khilafah kwa Njia ya Utume, kwa mikono miwili? Hakika, hilo ni bora kwetu Duniani na Akhera.

02 Sha’aban 1445 H - 12 Februari 2024 M

Marekani Huchagua Nyuso Muhimu za Serikali katika Ulimwengu wa Kiislamu

Baada ya uchaguzi nchini Pakistan, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alitangaza mnamo tarehe 9 Februari, "Sasa tunatazamia kwa wakati unaofaa, matokeo kamili ambayo yanaakisi matakwa ya watu wa Pakistan." Kuanzia Morocco hadi Indonesia, uchaguzi unaakisi matakwa ya wakoloni, sio watu. Mstari mwekundu ni chochote wanachotaka wakoloni, na huyo anayeitwa mtawala yuko pale tu ili kutoa hakikisho. Katika Ulimwengu wa Kiislamu, mtawala halisi ndiye mkuu wa jeshi, au amiri jeshi mkuu, huku kamishna halisi wa uchaguzi ndiye mkuu wa ujasusi. Sasa ameshughulishwa na kupanga ziara za kuwatembelea wagombeaji wa uchaguzi, kwa kutumia hongo na vitisho, ili kuamua nyuso za serikali. Hakutakuwa na mabadiliko kutoka ndani ya mfumo huu. Unahitaji kung'olewa na kubadilishwa na Khilafah kwa Njia ya Utume.

03 Sha’aban H - 13 Februari 2024 M

Dola yenye Nyuklia Haipaswi Kuinamia Mfumo wa Kilimwengu Unaoporomoka

Mfumo wa kilimwengu unaoongozwa na Marekani umefeli katika nyanja zote. Licha ya kuungwa mkono kikamilifu na utawala wa Kizayuni, hauwezi kudai ushindi huko Gaza. Jeshi la Marekani bado linaendelea kuramba majeraha yake baada ya kushindwa nchini Afghanistan. Marekani imegawanyika sana kisiasa. Uchumi wa Marekani ni dhaifu. Dola zengine kubwa zinatafuta kukwepa utawala wa sarafu ya Marekani, dolari. Katika hali hii, kwa nini dola ya nyuklia itegemee taasisi za mfumo huu wa kilimwengu unaoporomoka, iwe Mfuko wa Fedha wa Kimataifa au Umoja wa Mataifa? Enyi maafisa wanyoofu katika Jeshi la Pakistan! Changamkieni fursa hii! Ipeni Nusrah yenu Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah, na muuzike mfumo huu wa kilimwengu uliovunjika milele in sha Allah.

04 Sha’aban H – 14 Februari 2024 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu