Ijumaa, 24 Shawwal 1445 | 2024/05/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Matembezo ya Ukombozi “Enyi Majeshi ya Waislamu: Qur'an Yenu Inakuamuruni Mutaharaki ili Kuinusuru Gaza.”

Mbele ya ushujaa ulioonyeshwa na mujahidina mashujaa katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) chini ya kauli mbiu (Kimbunga cha Al-Aqsa) dhidi ya umbile la Kiyahudi linaloendelea na kushambulia Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa, uzingiraji wake na upigaji mabomu wake unaoendelea kwa miaka 17 kwenye Ukanda wa Gaza, na mbele ya mauaji ya kikatili yaliyofanywa na umbile hili halifu katika mwezi uliopita kwa Waislamu waliotengwa katika Ukanda wa Gaza, ambayo yalisababisha kuuawa na kujeruhiwa zaidi ya wanaume na wanawake elfu 71 wa Kiislamu, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia, iliandaa "Matembezi ya Ukombozi" kwa kichwa“Enyi Majeshi ya Waislamu: Qur'an Yenu Inakuamuruni Mutaharaki ili Kuinusuru Gaza.”kwa ajili ya kuyataka majeshi ya Waislamu yataharaki kuwanusuru Waislamu wanyonge katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) na kukomboa Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa na Palestina yote inayokaliwa kimabavu kuanzia mto wake hadi bahari yake kutokana na makucha ya Mayahudi wahalifu wauwaji.

Mnamo siku ya Ijumaa, Disemba 22, baada ya swala ya Ijumaa (1:00 adhuhuri), kuanzia Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu hadi Barabara ya Al-Thawra.

Basi kuweni pamoja nasi na mushiriki katika ujira na Mwenyezi Mungu atatunusuru hata kama ni baada ya muda.

Ijumaa, 09 Jumada Al-Thani 1445 H sawia na 22 Disemba 2023 M

- Video ya Ualishi wa Matembezi -

- Alama Ishara za Amali hii -

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

#ArmiesToAqsa

#AqsaCallsArmies

Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu