Ijumaa, 29 Rabi' al-thani 1446 | 2024/11/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kunusurika kwa Trump na Mashtaka ni kwa Sababu Kura Zinaheshimiwa Zaidi kuliko Ukweli nchini Amerika

Na: Dr Abdullah Robin*

Mashtaka ya Trump yameigawanya Amerika. Baadhi wamesema kwamba katiba ya Amerika imepasuliwa, na katika ishara za kuonesha upinzani, na saa kadhaa baada ya Seneti kumuacha huru Trump, msemaji wa Bunge la Wawakilishi, Nancy Pelosi, alitoa ishara ya kushangaza kwa umma moja kwa moja kupitia runinga. Ilitokea wakati Trump alipomaliza kutoa hotuba yake ya mwaka kwa taifa kuhusu “Hali ya Nchi’’ katika Bunge la Wawakilishi. Aliposimama juu ya minbari kutoa hotuba, alipeana nakala iliyoandikwa kwa Nancy Pelosi kama ilivyo desturi, lakini kiutata hakumpa mkono Pelosi. Naye Pelosi akakataa kumtambulisha kama ilivyo tamaduni, “Wanachama wa Bunge, niko na sharafa na heshima kwa kuwaletea Rais wa Amerika” na badala yake alisema, “Wanachama wa Bunge, Rais wa Amerika.” Trump alikuwa na kiburi na kusifu ufanisi wake katika hotuba yake na Pelosi akatoa ishara ya hila usoni nyuma ya Trump alipokuwa akihutubia na Pelosi akamalizia upinzani wake kwa kusimama na kupasuapasua hotuba yake wakati Trump alipogeuka kuondoka juu ya minbari.

Kulikua na vipengee viwili vya mashtaka dhidi ya Rais Trump: matumizi mabaya ya madaraka kwa kuishinikiza Ukraine kuzindua uchunguzi kwa wapinzani wake wa kisiasa, na kuweka kizuizi kwa Bunge kwa kukataa kuwakubalia wafanyikazi wa Ikulu na Vitengo vya Serikali kutoa ushahidi. Katika mashtaka yote, maseneta wote wa chama cha Democrat walimtangaza Trump kuwa na hatia. Katika shtaka la pili maseneta wote wa chama cha Republican walimtangaza Trump kutokuwa na hatia, wakati katika shtaka la kwanza seneta mmoja pekee wa chama cha Republican alipiga kura dhidi ya Trump. Kwa kuwa chama Cha Republican kina wanachama wengi, Trump alipatikana hana hatia.

Trump na adui wake wa chama cha Democrat, Nancy Pelosi wamekuwa wakirushiana maneno makali. Pelosi alisema, “Trump amepasua ukweli katika hotuba yake, amepasua katiba na tabia yake, na nimepasua hotuba yake inayoashiria hali ya akili yake,” katika njia ya kuzungusha maneno kuhusu hotuba ya Trump yenye anwani ‘Hali ya Nchi. Trump alisema kwamba wanachama wa Democrat ni ‘waovu’ na “wanataka kuiharibu nchi”.

Vyumba viwili vya Bunge la Amerika vinahitajika kuuwajibisha utendaji wa afisi ya Rais kwa msingi wa ‘utengaji nguvu’. Hii ndio kanuni msingi ya uongozi katika nadharia ya demokrasia ambayo imeingizwa katika katiba ya Amerika kwa lengo la kuzuia matumizi mabaya ya mamlaka na dhulma. Hata hivyo Rais Trump hajawajibiswa kwa matendo yake, kwani kura za kuunga au dhidi ya makosa ya Trump zilikuwa na uhusiano wa vyama. Hata kabla kesi kuanza katika Seneti, kiongozi wa chama cha Republican, Mitch McConnell, alisema kwamba, “Hakuna nafasi ya kuwa Rais ataondolewa katika mamlaka.” Ni kesi ya kuajabisha iwapo hakimu atapeana uamuzi kabla kesi haijaanza. Wanachama wa Republican walikataa kuita shahidi yeyote, lakini wanachama wa Democrat walitaka kuwaita wengi, na hili swala lilijadiliwa na kupigiwa kura hata kabla kesi kuanza. Aliyekuwa mshauri wa maswala ya Usalama nchini, John Bolton, alitangaza katika vyombo vya habari, kwamba anakaribia kuchapisha kitabu kuthibitisha kuwa Trump alizuilia msaada kwa Ukraine ili kuwashinikiza na waende kwa matakwa ya Trump ya kufanya udadisi kwa wapinzani wake wa kisiasa, na wanachama wa Democrat walimtaka Trump atoe ushahid katika kesi. Kura zilipigwa kwa mujibu wa Chama na wala sio msingi, kwa hivyo kesi ilifanyika bila Bolton ama mashahidi wengine! Hakika hii ndio kesi dhalili kabisa ulimwenguni.

Kesi ya Rais kupelekwa wa mujibu wa umaarufu badala ya ukweli sio geni. Rais wa zamani Clinton alishtakiwa baada ya kashfa ya Monica Lewinsky na wengi miongoni mwa wanachma wa Democrat walikua dhidi ya kesi hiyo, na wengi miongoni mwa wanachama wa Republican waliunga mkona kesi hiyo. Kesi ilifanyika katika Seneti, pia na mashtaka mawili, hakuna hata mwanachama mmoja wa Democrat alipiga kura kuwa Rais yuko na hatia. Katika upande wa Republican, kumi kati ya 55 walipiga kura kuwa Rais hana hatia katika kesi ya kwanza na watano walimtangaza hana hatia katika kesi ya pili. Hivyo basi kesi zote mbili, matokeo yaliamuliwa kwa mujibu wa uhusiano wa mrengo wa kisiasa. Kwa maana nyingine, unawezafanya chochote ikiwa watu wengi wako nyuma yako, unawezafanya unacho kipenda ikiwa wewe ni rais wa Amerika, kama ambavyo Trump alivyokuwa akisema! Miezi sita iliyopita alitangaza, “Kisha niko na Kipengee cha 2, ambapo niko na haki ya kufanya kile nitakacho kama rais.”

Hata hivyo, upinzani kwa Trump unaendelea. Kiongozi wa Wachache katika Seneti Chuck Schumer amesema kwamba kuwachwa huru kwa Trump ni, “kutokuwa na thamani” na ilikuwa kwa sababu ya “kufinikwa kwa ajabu kwa haki katika historia ya nchi.” Kiongozi wa Wengi katika Seneti, Mitch McConnell, ambaye alikuwa kiongozi wa Republican amesema, “Tulipiga kura. Hakuna kura iliyozuiliwa. Hakuna mjadala uliyozuiliwa. Hawa watu hawakuwa na kura … Hawa watu wangeshinda mara nyingi kama wangeshinda chaguzi zaidi na wako na nafasi ya kufanya hivyo mwaka huu.” Kwa hivyo kushinda kesi ya kisheria ni kuhusiana na kura, sio ukweli ndani ya Amerika, na Rais kiukweli yuko juu ya sheria maadamu chama chake kiko na imani kwamba wapiga kura wako na furaha.

*Imeandikwa kwa ajili ya Gazeti la Ar-Rayah - Toleo 273

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 28 Machi 2020 08:35

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu