Jumapili, 25 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/06/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Habari na Maoni
Ukombozi wa Wanawake Afrika: Uhuni wa Kikoloni kuhujumu Utulivu wa Jamii

Habari:


Mnamo Jumanne 16 Oktoba 2018, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alitaja baraza la mawaziri 20 huku wanawake wakichukua nusu ya vyeo sawa na wenzao wanaume. (The Star, 16/10/2018). Siku mbili baadaye mnamo Alhamisi 18 Oktoba 2018, Rais wa Rwanda Paul Kagame alitaja baraza la mawaziri 26 na wanawake wakichukua asilimia 50 ya baraza ikiwa ni 13 kati ya 26. (The New Times, 19/10/2018). Siku saba baadaye Alhamisi 25 Oktoba 2018, Bunge la Ethiopia lilimchagua SahleWork-Zewde kama rais wa tano na wa kwanza wakike tangu 1991 chama tawala cha Demokrasia cha Watu wa Mapinduzi wa Ethiopia (EPDRF). (Addis Standard, 25/10/2018)

Maoni:


Maamuzi yaliyochukuliwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ambaye ni Muislamu aliyeoa mke Mkristo; ni ya kimakusudi na yanayolenga kumakinisha mtizamo muovu wakimagharibi uliyokitwa juu ya mwito duni wa kisekula wa kirasilimali wa “Ukombozi wa Wanawake=Uhuru wa Wanawake” inayopigiwa debe na madola ya kisekula ya kikoloni ya kimagharibi na mashirika yao kama Umoja wa Mataifa (UN) na kikaragosi cha Muungano wa Afrika (AU) unaongozwa na vibaraka. Hivyo basi, matukio hayo yaligonga vichwa vya habari ulimwenguni huku vyombo vya habari vya kieneo na kimataifa vikiripoti kuhusiana na matukio hayo matatu kwa kinywa kipana. Waliangazia hususan kauli zilizotolewa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, “Wanawake wetu watatoa changamoto kwa msemo wa zamani kuwa wanawake hawawezi kuongoza. Maamuzi haya ni ya kwanza katika historia ya Ethiopia na labda Afrika” na Rais wa Rwanda Paul Kagame, “Idadi kubwa ya wanawake kuweko katika majukumu ya kufanya maamuzi imepelekea kupungua kwa ukandamizaji na uhalifu wa kijinsia.” (Independent, 16-20/10/2018).

Ukombozi wa wanawake na misemo yake hususan Usawa wa Kijinsia ni fikra ovu inayotokamana na dola za kimagharibi za kisekula za kirasilimali za kikoloni zinazolenga kuwafanya sawa wanaume na wanawake katika makujumu na haki zao ndani ya jamii. Ili kufikia lengo hilo, inapigia debe wanawake wapewe haki za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kielimu na kimahakama. Kwa kuwa Afrika ni shamba la kikoloni ambalo viongozi wake vibaraka sichochote bali ni watumishi watiifu wanaotekeleza sera za mabwana zao! Hivyo basi, Afrika kupitia AU walipitisha kanuni zifuatazo katika kuunga mkono eti usawa wa kijinsia na uinuaji wa wanawake ambazo zitatoa muongozo kieneo, kitaifa, sera na mipango ifuatayo:

1. Sheria Juu ya Haki za Wanawake ndani ya Afrika za 2003;

2. Mpango wa Maputo Juu ya Afya na Haki za Jinsia na Uzazi wa 2006 unaoazimia kulisukuma mbele bara la Afrika kutimiza lengo la kupata huduma jumla za afya na kijinsia kufikia 2015 ikiwa ni pamoja na kupunguza vurugu za kijinsia;

3. Tangazo la 2010-2020 kama Muongo wa Wanawake wa Afrika mnamo 2008 kusukuma usawa wa kijinsia kwa kufanya haraka utekelezaji wa Maamuzi ya Dakar, Beijing na Baraza la Muungano wa Afrika juu ya Usawa wa Kijinsia na Uinuaji wa Wanawake kupitia mipango ya juu-chini na chini-juu na

4. Kanuni za Kufanyiwa Kazi na Mapendekezo dhidi ya Madhara ya Vitendo vya Kitamaduni mnamo 2011 ambazo zitatathmini vipaombele vya kufanyiwa kazi ili kupambana na madhara ya vitendo vya kitamaduni.

Natija ya utekelezaji wa kanuni hizo na nyingine ambazo sikuzitaja zimesababisha huzuni katika ndoa, umama na muundo wa familia. Kwa kuwa zote zimekitwa juu ya kauli ya kirongo ya “ukombozi wa wanawake” kutoka katika majukumu yao msingi kama wake, mama na wasimamizi wa nyumba hadi kuwafanya kuwa ni bidhaa za ngono na za biashara zinazopatilizwa na waajiri na makampuni eti kwa usawa wa kijinsia na uinuaji wa wanawake! Kwa maana nyingine, wanawake waliokombolewa wanakwenda mbio kushindana na wanaume katika ajira, kuwashinda wanaume katika majukumu yao msingi ya utafutaji.

Baadhi ya athari za maangamivu yanayoshuhudiwa leo Afrika kote na duniani ni kukosekana kwa furaha katika jamii kunakotokamana na kuwa wanawake wengi wanazunguka kati ya maeneo yao ya ajira ambayo yamewekwa viashiria vya kufaulu na huku kuna majumba yao ambapo kuna watoto na majukumu ya familia yanayohitaji kutekelezwa! Kupigia debe kucheleweshwa kwa ndoa na uzinifu kwa vijisababu visivyokuwa na mashiko vinavyokuza kusomea ajira na kukashifu ndoa za mapema kama mila zenye kuwafunga wanawake jikoni, ulezi wa watoto na usimamizi wa nyumba! Yeyote anayepinga ubadilishaji wa majukumu ya kijinsia ikijumuisha lakini sio tu wanawake waliosoma au kutosoma wanatizamwa kuwa ni watu walioko nyuma, wamepitwa na wakati na wanaunga mkono dhuluma na ukandamizaji wa wanawake kwa ujumla!

Afrika inahitaji kuzinduka kutoka usingizini kwa kujitoa katika minyororo ya wamagharibi wakoloni mabwana ambao wamewalazimishia mfumo batili wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake ovu ikijumuisha ile ya uhuru wa jamii inayopigia debe ukombozi wa mwanamke na nidhamu ya kiuchumi ya kisekula ambayo imeifunga Afrika na kuwa bara la kuombaomba licha ya kuwa na rasilimali nyingi! Njia pekee ya kufikia hapo ni kuukumbatia mwito wa Khilafah kwa njia ya Utume ambayo itawafurusha wakoloni na kuipa Afrika ukombozi wa kweli uliokitwa juu ya utekelezaji wa Uislamu safi kupitia kumakinisha utambulisho wa Kiislamu unaothamini ndoa, umama na muundo wa familia kama msingi wa jamii ya Kiislamu! Ni kupitia Khilafah pekee ndiyo wanawake watafikia uwezo wao katika majuku yao msingi kama wake, mama na wasimamizi wa nyumba.

Imeandikwa Kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:44

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu