Ijumaa, 09 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mfumo wa Kidemokrasia wa Kirasilimali Huzalisha tu Wanasiasa Majanga Pekee

(Imetafsiriwa)

Habari:

Imran Khan alijeruhiwa katika kisa cha ufyatuliwaji risasi wakati maandamano marefu marefu ya PTI

WAZIRABAD: Waziri Mkuu wa zamani na mwenyekiti wa chama cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) Imran Khan na viongozi wengine kadhaa wa PTI walijeruhiwa baada ya mtu mmoja kufyatua risasi karibu na kambi ya mapokezi ya PTI huko Allahwala Chowk wakati wa maandamano marefu ya chama hicho, ARY News iliripoti mnamo Alhamisi. (Arynews.tv)

Maoni:

Kadiri muda unavyosonga, siasa za Pakistan zinazidi kuwa mbaya, kila kukicha watu wanashuhudia kiwango cha wanasiasa wetu kiko katika hali mbaya. Mapazia yote yanafunuliwa kiasi kwamba hata mtu wa kawaida anaweza kuelewa wazi kwamba wanasiasa hawa walioko madarakani wanatamani sana kubaki madarakani na kwa ajili hiyo wako tayari kufanya lolote lile, katika kuwafurahisha mabwana zao Marekani na mamlaka nyingine za ndani, wanasiasa wetu wako tayari kuitoa kafara damu, mali na heshima ya Waislamu kwani hawajali ustawi wa Waislamu. Wanachotaka ni biashara ya kupora mali zetu kwa msaada wa IMF kupitia kutekeleza ushuru wa kinyama wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja au kulizika suala la Kashmir kwa kuipa India zawadi kwa utiifu wa mabwana zao wa Amerika. Hali ni hiyo hiyo kwa wanasiasa walioko upinzani ambao pia wako tayari kufanya chochote ili kuwafurahisha mabwana zao ili kupata uamuzi wa kuwapendelea wao lakini pambizoni mwa matukio haya yote, jambo moja la daima ni masaibu ya Waislamu nchini Pakistan. Kila siku inayopita mfumko wa bei unaongezeka na wengi wanaoishi Pakistan wanasonga chini ya mstari wa umaskini ambapo hawajui kama watapata chakula au la siku inayofuata kwa ajili yao na familia zao. Mfumko wa bei na kutokuwa na uhakika wa chakula yako kwenye msukosuko, sheria na utangamano, elimu, vituo vya matibabu zinaonekana kama hadithi za zamani.

[إِنَّ اللَّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ]

“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao.” [Ar-Ra’d 13:11].

Umefika wakati sasa wa kuung'oa mfumo huu mbovu wa Kidemokrasia wa Kibepari unaoweza tu kuzalisha betri za aina hii za wanasiasa wakorofi wanaoingia madarakani kwa nguvu za vichochoro kisha kufanya tu yale ambayo mabwana zao wanawataka kufanya wasitujali sisi, taabu itaendelea ikiwa watawala hawa vibaraka wasaliti na mabwana zao wa Magharibi wataendelea kunyonya damu zetu hadi Mfumo huu wa Kidemokrasia wa Kibepari utakapong'olewa na kwa ajili hiyo tunachohitaji ni kufanya kazi kwa bidii ili kuusimamisha tena mfumo pekee wa utawala ambao Mwenyezi Mungu (swt) ametupa, huo ndio mfumo uliotabikishwa na kipenzi chetu Mtume Muhammad (saw) mjini Madina na baadaye Khilafah ikauendeleza kwa mafanikio kwa mamia ya miaka.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Mohammad Adel

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu