Jumamosi, 10 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kombe la Dunia nchini Qatar: Dosari ya Kihistoria

(Imetafsiriwa)

Habari:

Katika siku chache, timu ya taifa ya kandanda ya Denmark itasafiri hadi Qatar kuiwakilisha Denmark katika Kombe la Dunia 2022. Wachezaji wa Denmark watacheza wakiwa na nguo nyeusi, ambazo zitaashiria bendi ya maombolezi ambayo inaashiria kutoridhika na serikali nchini Qatar na ambayo inaashiria kwamba Denmark anahudhuria mazishi. Mantiki iliyoko ni kwamba, huwezi kuunga mkono nchi inayo kiuka haki za binadamu, inayozuia kujieleza kijinsia na kuwatendea vibaya wafanyikazi wahamiaji. Hata hivyo, nchi zote zinazohitimu hushiriki, kadhaa hata kwa uwakilishi wa kisiasa.

Maoni:

Kwa miezi kadhaa, mjadala umekuwa mkali kuhusu chaguo la Qatar kama taifa mwenyeji, na wanasiasa kadhaa barani Ulaya wameikashifu vikali Qatar na kutoa wito wa kususiwa duru ya mwisho, haswa katika kutetea jamii ya LGBT+. Hivi majuzi, kituo cha televisheni, DR, ambacho kinamilikiwa na serikali ya Denmark na chini ya muafaka uliowekwa na waziri wa utamaduni, kimechapisha filamu inayoonyesha upande fisadi na katili wa Kombe la Dunia. Maandamano na filamu hizi zilikuwa ngumu kuzifuatilia wakati Kombe la Dunia lilipofanyika nchini Urusi mnamo 2019, hata wakati wafanyikazi wa uwanja walikabiliwa na hali mbaya na kusababisha vifo na wasiokuwa na hatia walipigwa mabomu na kuuawa na wanajeshi wa Urusi nchini Syria. Kwa sababu hupaswi kuchanganya michezo na siasa pamoja, walisema. Leo Urusi imepigwa marufuku kushiriki Kombe la Dunia baada ya vita nchini Ukraine.

Hakuna shaka kwamba Qatar ni serikali ya kidikteta ya kibaguzi, dhalimu inayowanyonya wafanyikazi wahamiaji na kuwaweka katika utumwa wa kisasa, na kusababisha vifo vya zaidi ya 6,500. Lakini ni serikali ya kidikteta ambayo kwayo serikali ya Denmark imekuwa na mahusiano ya kisiasa na biashara kwa miongo kadhaa. Na inaendelea kufanya hivyo! Kama vile serikali ya Denmark inavyoshirikiana na Modi, mchinjaji kutoka India, ambaye damu ya Waislamu wasio na hatia inachuruzika mikononi mwake muda huu huu na hayo hayo yanaweza kusemwa kuhusu "demokrasia pekee ya Mashariki ya Kati" katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Palestina! Yako wapi maandamano na mazungumzo ya ususiaji!? Au haki za binadamu ni kitu tu ambacho kinatumika kwa jumuiya ya LGBT+ na Waukraine pekee?

Nchini Denmark, sheria maalum zilitungwa kwa ajili ya wakimbizi wa Kiukraine, ili wasiathiriwe na sera ile ile ya kikatili ya wakimbizi ambayo wakimbizi wa Syria walikutana nayo. Wakati huo huo, Denmark imepata hisia zake za haki kuhusu wafanyikazi wahamiaji nchini Qatar, lakini hisia hii haipatikani katika siasa za Denmark, ambapo wakimbizi wanakabidhiwa kwa dikteta nchini Syria.

Kuandaliwa kwa Kombe la Dunia nchini Qatar kwa njia nyingi ni fedheha ya kihistoria, inayogharimu zaidi ya dolari bilioni 200, ambazo zinatosha zaidi ya sana kutokomeza umaskini duniani! Serikali hiyo inatumia mapato yake makubwa ya mafuta, ambayo ni mali ya umma wa Kiislamu, kujinadi yenyewe huku idadi ya watu ikitumbukia ndani ya umaskini wakati wa mgogoro mbaya.

Polisi wa Magharibi, wanaojitukuza na wenye maadili ya kinafiki hawana haki ya kuilaumu Qatar. Nchi za Magharibi, zilizozama katika damu ya ukoloni, kuziuzia silaha tawala za kiimla na kusababisha vifo na uharibifu nchini Afghanistan na Iraq, hazina haki ya kutoa mihadhara kwa mataifa mengine kuhusu kutokiukwa kwa maisha ya binadamu.

Huu ndio urefu wa unafiki na unduma kuwili. Ni kama kung'arisha vito kwenye taji huku wakifinika pembe zao za kishetani!

Ulimwengu unahitaji mfumo mbadala unaotenda maadili na utu thabiti na usiobadilika, bila ubaguzi na unafiki. Badali pekee ya unafiki wa Urasilimali ni maadili ya kikweli ya Kiislamu, ambayo hayatukuzi manufaa na faida, bali ambayo yameteremshwa na Muumba wa ulimwengu, Mwenyezi Mungu, Mtukufu, na yanayoonyeshwa katika sera za dola ya Kiislamu, al-Khilafah.

[وَمِمَّنْ خَلَقْنَا أُمَّةٌ يَهْدُونَ بِالْحَقِّ وَبِهِ يَعْدِلُونَ]

“Na katika tulio waumba wako watu wanao ongoza kwa Haki, na kwayo wanafanya uadilifu.” [Al-A’raf: 7:181].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ibrahim Atrach

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu