Ijumaa, 24 Shawwal 1445 | 2024/05/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Habari na Maoni

Urasilimali Hudanganya na Kuhofisha kwa Maslahi ya Kidunia! 

Habari:

Waziri wa Mambo ya Ndani ametuma ziada ya waraka kuhusiana na tahadhari ya virusi vya Korona katika serikali za majimbo 81. Katika muendelezo wa tahadhari hiyo; inaeleza kwamba ili kujikinga na maambukizi ya mkurupuko wa virusi vya Korona (Covid-19) na kusambaa kwa mkurupuko huo, shughuli za mikusanyiko vibandani, madisko, mabaa na vilabu vya usiku vitasitishwa kwa muda, kwa sababu kuwa pamoja kwa umbali mfupi katika “Mapumziko ya wazi na maeneo ya burudani” inaweza kuwa hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa. (Mashirika 16.03.2020)

Maoni:

Watawala madhalimu wa nidhamu ya kirasilimali ambao hudai kuwa uungu wa dunia, leo wamekuwa hawana msaada na wamekuwa wenye kuona haya mbele ya uungu wa Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Ta’ala, Bwana wa mbingu na dunia, kama ilivyokuwa mwanzo. Ukweli kwamba wadudu wakubwa, ambao huaribu mazao na vimelea na thamani zake kwa ajili ya kupata manufaaa zaidi, wamekuwa wanyonge mbele ya virusi hii ndiyo hali halisi iliyopo. Hapa sitoweka mkazo wa kuthibitisha au kupinga kufanyika kwa njama au hila kinadharia na maoni mbalimbali yanayotolewa kwa kuzingatia virusi vya Korona.

Nukta ya kuwekewa mkazo, ni kwamba Mwenyezi Mungu, ambaye yupo mbali na mapungufu na ambaye ni mmiliki wa nguvu na muweza kwamba angeweza kupelekea kushindwa kwa kila kitu, ametikisa misingi ya nidhamu zao na zao duni kwa virusi tu.  Katika hali hii, ametukumbusha tena kuhusiana na ukweli kwamba anaweza kubadilisha mazingira yaliyopo kwenye jamii kutoka hali moja kuelekea nyingine.

Ingawa hatua zinazochukuliwa dhidi ya virusi vya Korona, na watawala ambao wana nguvu ya utawala, zinaonekana kwa sura ya kujali maslahi ya wanadamu, lakini kiuhalisia ni kwamba ni kwa ajili ya wasiwasi kwa uchumi wao na madaraka yao. Zana ya hofu ya katika nidhamu ya kirasilimali, ambayo hukifanya kila kitu kuwa ni bidhaa ya kibiashara, pia huzingatia kanuni ya kupungua kutoka katika vitu inavyovitilia thamani. Serikali ambazo zimekuwa uongozini nchini Uturuki kwa miaka kadhaa zimeusalimisha mujtama katika ukandamizaji wa demokrasia kwa kuzitumia hisia na mawazo ya Waislamu kwa maslahi yao binafsi.

Serikali ambayo haiondoshi uovu wowote na hasa husababisha kutokea kwa uovu mpya kila kukicha, imeonyesha kwamba inaweza kufunga maeneo ambapo haramu inafanyika siku zote kwa wasiwasi wa kidunia. Tena kwa waraka mmoja tu. Maeneo kama vile vibandani, madisko, baa na vilabu vya usiku ambayo Mwenyezi Mungu amezikataza na ambamo ukatili na uhalifu unafanyika, zinafungwa kwa hofu ya maisha ya kidunia na maslahi yake. Hata hivyo, wanaruhusu maovu haya yote ambayo hupelekea uharibifu na kuondosha thamani zote za Dini na maadili ya mujtama, bila kujali hatari na maagizo ya Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu (swt). Kwani Mwenyezi Mungu hastahiki kuogopewa zaidi?

Urasilimali hudanganya na kuhofisha kwa maslahi ya kidunia. Hata hivyo, Mola wetu ametutahadharisha na kutuonya dhidi ya dunia na akhera vile vile.

Na ilhali huku virusi vya korona vimewadhibiti watawala wenye nguvu ya utawala, kwa upande mwingine vimewavua barakoa watawala. Kwa hiyo, kuchukua tu maamuzi ilitosha kuangamiza na kufunga mizizi ya fitna. Wale ambao hawataki kuthubutu kubadilika, kuangamiza nidhamu ya kirasilimali ambayo imeharibu mujtama wote, wanafanya uovu mkubwa mno kwa Waislamu. Pamoja na vitendo vya hivi karibuni, hasa Waislamu walioiunga mkono serikali kutokana na hisia zao za Kiislamu, lazima wameona namna wanavyodanganywa na watawala. Haya yanatosha kuwa ni ukumbusho kwa watu wenye akili.

Na huku watawala wakijitolea muhanga kwa kila kitu katika njia hii ili kupinga Aya ya Mwenyezi Mungu iliyoko hapo chini, kwa bahati mbaya wao wamekuwa wenye kutangaza vita na Dini ya Mwenyezi Mungu, kwa kufanya kinyume na kuyalinda na kudumisha maovu .

(الَّذِينَ إِن مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنكَرِ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ)

“Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Sala, na wakatoa zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote.” [Al-Hajj:41]  

Ni ukatili kuendelea kuing’ang’ania demokrasia, na kumpa mgongo Bwana wa Siku ya Kiyama anayestahiki kuogopewa na ambaye ameumba uhai na mauti.

Karibuni, kutakuja kuwa na Khilafah Rashidah ambayo itajifunga na Aya hii, itakayohifadhi maslahi ya kidunia kwa kutenda vitendo vyake kwa mujibu wa kuhofia Mwenyezi Mungu, huku ikiweka utafutaji radhi za Mwenyezi Mungu kuwa ndio msingi wa maisha yake na usimamizi wa watu kwa mujibu wa Dini ya Mwenyezi Mungu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ahmet SAPA

#Korona

#Covid19
 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 06 Aprili 2020 20:06

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu