Jumanne, 13 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki wa Habari 26/04/2023

Matumizi ya Jeshi la Marekani Yako Juu Kushinda Nchi Nyengine 11 Zikiunganishwa

Matumizi ya silaha duniani yalifikia rekodi ya $2.24 trilioni mwaka 2022, ongezeko la karibu 4%, kulingana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (SIPRI). Shirika hilo la kimataifa liligundua kuwa mwelekeo huo uliongozwa na nchi za Ulaya kuregea katika viwango vya matumizi ya Vita Baridi, ingawa Marekani imesalia kuwa nchi inayotumia pesa nyingi zaidi katika vita. Dkt. Nan Tian, mtafiti mkuu wa Mpango wa Matumizi ya Kijeshi na Uzalishaji wa Silaha wa SIPRI, alisema, "Kuongezeka kwa kuendelea kwa matumizi ya kijeshi duniani katika miaka ya hivi karibuni ni ishara kwamba tunaishi katika ulimwengu unaozidi kukosa usalama." Matumizi ya kijeshi ya Marekani yanaendelea kuvunja rekodi, baada ya kushikilia nafasi ya kwanza kwa wanajeshi wengi. Kulingana na ripoti ya SIPRI, karibu dolari bilioni 20 katika silaha ambazo Washington ilizisafirishwa hadi Kiev mnamo 2022 ni msaada mkubwa zaidi wa usalama ambao nchi moja imewahi kutoa kwa nchi nyingine katika mwaka mmoja. Zaidi ya hayo, Marekani ilibakia kuwa mtumiaji mkubwa zaidi wa kijeshi duniani kwa dolari bilioni 877 - zaidi ya jumla ya bajeti za kijeshi za nchi 11 zengine zinazotumia matumizi ya juu zikiunganishwa kwa pamoja. Mataifa mengine mengi yanayotumia fedha nyingi ni washirika wa Washington, huku matumizi ya kijeshi miongoni mwa wanachama wa NATO yakizidi dolari trilioni 1.23. William Hartung, mtafiti mkuu katika Taasisi ya Quincy, alieleza kuwa kuongezeka kwa matumizi ya kijeshi ni ishara mbaya kwa amani huku akisisitiza umuhimu wa diplomasia.

Upanuzi wa BRICS

Balozi wa Afrika Kusini katika BRICS (kambi isiyo rasmi ya Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini) alisema nchi 19 zimeonyesha nia ya kujiunga na jumuiya hiyo, ambayo itakutana jijini Cape Town Juni 2-3 kujadili upanuzi huo. Saudi Arabia na dola zengine za Baraza la Ushirikiano wa Dola za Ghuba zinazozalisha mafuta, pamoja na Misri na Indonesia, zinaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kujiunga na BRICS haraka. Upanuzi huu ungeongeza utajiri wa kambi hii na pengine kuiwezesha kufadhili na kuwekeza katika miradi zaidi, na uwezekano wa kuongeza uwezo wake wa kufanya kazi kama mwanakandarasi dhidi ya taasisi za Magharibi. Hata hivyo, nchi zinazoshiriki katika BRICS, haswa ikiwa itapanuliwa, zina maslahi tofauti kutoka kwa kila mmoja, ambayo itazuia uwezo wa umoja huo kuzingatia malengo ya pamoja. Zaidi ya hayo, nia ya nchi za GCC kujiunga na BRICS haimaanishi kuwa zinaachana na uhusiano wao wa kiulinzi na kijeshi pamoja na Marekani na Magharibi.

Kushindwa Kulipa Madeni kwa Marekani Kutachochea 'Janga la Kiuchumi'

Waziri wa Hazina wa Marekani Janet Yellen mnamo Jumanne alionya kwamba kushindwa kwa bunge la Congress kuongeza kiwango cha deni la serikali - na natija ya kushindwa kulipa deni - kunaweza kusababisha "janga la kiuchumi" ambalo litapandisha viwango vya riba juu kwa miaka mingi ijayo. Alisema ni "jukumu msingi" la bunge la Congress kuongeza au kusitisha kiwango cha ukopaji cha $ 31.4 trilioni, akionya kwamba kushindwa kulipa deni kunaweza kutishia maendeleo ya kiuchumi ambayo Marekani imepata tangu janga la maambukizi la COVID-19.

Tofauti na nchi nyingine nyingi, Marekani inaweka kikomo kigumu juu ya ni kiasi gani inachoweza kukopa. Kwa sababu serikali inatumia zaidi ya inavyozalisha, wabunge lazima mara kwa mara waongeze kiwango cha deni. Kevin McCarthy, kiongozi wa Baraza la Wawakilishi linalodhibitiwa na chama cha Republican, wiki iliyopita aliolesha mpango ambao ungeongeza $4.5 trilioni katika kubana matumizi na ongezeko la $1.5 trilioni katika kikomo cha deni, na kuutaja kuwa msingi wa mazungumzo katika wiki zijazo. Ikulu ya White House inasisitiza kuwa masuala hayo mawili hayafai kuhusishwa, na Seneti inayodhibitiwa na chama cha Kidemokrasia huenda ikakataa pendekezo hilo. Huku mijadala ya kikomo cha deni ikizidi kuwa ya mara kwa mara tofauti za Congress zinaongezeka ili kujumuisha masuala mengi ambayo yanaathiri taswira ya Marekani ya kimataifa.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu