Jumanne, 13 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa

Amiri wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah katika Ukurasa Wake wa Facebook

Jibu la Swali
Kuwapa Hongera Wakristo na Makafiri Kwenye Sikukuu Zao

Kwa: Bahaa Alden Torman

Swali:

Assalam aleykum wa rahmatullah wa barakatuh, ndugu yenu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Bahaa kutoka Palestina. Twamuomba Mwenyezi Mungu muwe na afya njema na nguvu.

Swali langu ni kuhusu kuwapa hongera Wakristo kwa sherehe zao na kushiriki nao, na kilichonisukuma kuuliza swali hili ni jibu la swali la Sheikh Taqiuddin al-Nabhani, Mwenyezi Mungu amrehemu, kuliruhusu hilo, hivyo nataraji kutoka kwenu ufafanuzi wa jambo hili. Pamoja nalo ni jibu la swali la Sheikh Taqi.

Jibu: 

Waaleykum salaam wa rahmatullah wa barakatuh

Tumeshatangulia kujibu swali hili, na hili hapa jibu kwako:

(Ndugu mtukufu

Waaleykum salaam wa rahmatullah wa barakatuh

Kuhusu swali lako kuhusu kuwapongeza Watu wa Kitabu katika sikukuu zao, kabla sijakujibu, nitakutajia baadhi ya matoleo yaliyotangulia yanayohusiana nalo:

[1- Ilitolewa hapo awali mnamo tarehe 1/30/1970: (- Ni ipi hukmu ya kuwazuru Wakristo kwenye sherehe na sikukuu zao, kuwatembelea wagonjwa wao, na kwenda katika mazishi yao? Na je, Muislamu anafanya nini anapowatembelea? Na hii ina uhusiano gani na Hadith tukufu, "لا تبادئوا اليهود والنصارى السلام ...الحديث"؟ “Musianzeni kuwatolea salamu Mayahudi na Wakristo...hadith”?

Jibu: Imethibiti kuwa Mtume (saw) alimtembelea Yahudi mmoja alipokuwa mgonjwa, na imethibiti kuwa alisimama kwa ajili ya jeneza la Yahudi mmoja, na imethibiti kuwa yeye, Rehema na amani zimshukie, aliusia kuhusu madhimmi (raia wa dola ya Kiislamu wasiokuwa Waislamu). Hivyo haya yote na mfano wake ni dalili ya kujuzu kuwatembelea Wakristo katika sherehe zao na sikukuu zao na kuwazuru wagonjwa wao na kwenda katika mazishi yao na kuwapa rambirambi na yanayofanana na hayo. Ama Hadith “Musianzeni kuwatolea salamu”, hii ni makhsusi kwa salamu pindi mkikutana nao njiani, na ni andiko (nasw) katika salamu hivyo haijumuishi kitu chengine chochote. 23 Dhul Qi’dah 1389 – 30/1/1970) 

2- Kisha ikatolewa mnamo tarehe 7/17/1976: (- Je, yajuzu kuwatembelea Wakristo na Mayahudi katika sherehe zao?

Jibu: Inajuzu kuwatembelea Wakristo kwa sababu ni katika wema, nalo ni jambo linalojuzu. 17/7/1976)

3- Pia ilitolewa mnamo tarehe 16/1/2010:

(Inajuzu kuwapongeza Ahlul-Kitaab katika sikukuu zao, ama kusema kwetu “na kwenu” ni kana kwamba umefanya qiyas kwa yale yaliyotajwa katika Hadith kwa kuwaambia “wa alaykum” pindi wanaposema “assalam aleykum” ...

Lakini si hivyo, kwani yale yaliyotajwa katika Hadith ni jibu la kusema kwao “as-saam aleykum” na neno ‘as-saam’ ni kifo, andiko la Hadith hiyo katika Bukhari na Muslim kupitia kwa mama wa waumini, Aisha (ra), ambaye alisema: Kundi la Mayahudi liliingia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) wakasema: Assaam aleykum (kifo kiwe juu yenu). Aisha asema: nilifahamu basi nikasema wa alaykum as-saam wa al-la’natu (nanyi pia kifo na laana viwe juu yenu. Akasema: kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema:  «مَهْلاً يَا عَائِشَةُ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الرِّفْقَ فِي الْأَمْرِ كُلِّهِ» “Taratibu ewe Aisha, hakika Mwenyezi Mungu anapenda upole katika mambo yote.” Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je hukusikia waliyoyasema? Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema: «قَدْ قُلْتُ وَعَلَيْكُمْ» “Nilisema na juu yenu.” Na katika riwaya nyengine ya Muslim kupitia kwa Ibn Omar (ra), amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): «إِنَّ الْيَهُودَ إِذَا سَلَّمُوا عَلَيْكُمْ يَقُولُ أَحَدُهُمْ السَّامُ عَلَيْكُمْ فَقُلْ عَلَيْكَ» “Pindi Mayahudi wanapokusalimieni, mmoja wao akisema: assamu aleykum (kifo kiwe juu yenu), basi sema:  iwe juu yako.” Na kwa hivyo umeona kuwa hii ni kwa sababu wanasema "assaam aleykum" (kifo kiwe juu yenu).

Lakini wakisema neno jema la kutupongeza, basi tunalikubali kutoka kwao, wakisema: Idd yenu iwe yenye baraka, tunawaambia jibu zuri na sahihi, kama vile kusema shukrani kwa kupongezi hizo, na ahlan wa sahlan au mfano wa hayo katika majibu yasiyopingana na Sharia. 16/1/2010) Mwisho

 Kutoka na haya, yanabainika yafuatayo:   

1- Inajuzu kuwapongeza ahlu dhimma kwa sikukuu yao kwa maneno mazuri yasiyopingana na Sharia, kwa hivyo hatuisifii sikukuu yao, yaani hatusemi “Idd Mubarak” au mfano wa hayo.

2- Lakini hii ni kwa wale wanaotimiza masharti yafuatayo:

A- Kwamba wawe miongoni mwa watu wa dhimma wanaoishi miongoni mwa Waislamu katika nchi za Kiislamu na mkataba wa dhimma unawahusu kwamba wasiwasaliti Waislamu...

B- Kwamba wasitupige vita kwa sababu ya dini au wasiunge mkono kufukuzwa kwetu... kama ilivyokuja katika Aya tukufu...

- Ama dalili kuwa wao wawe katika ahlu dhimma, jibu la kwanza la tarehe 30/1/1970 linaeleza juu ya hilo: (Ilithubutu kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alimtembelea Yahudi mmoja akiwa mgonjwa, na ikathubutu kuwa alisimama kwa ajili ya jeneza la Yahudi mmoja, na ikathubutu kuwa yeye (saw), aliusia kuhusu madhimmi, hivyo yote haya na mfano wake ni dalili ya kuruhusiwa kuwazuru Wakristo katika sherehe zao na sikukuu zao, na kuwatembelea wagonjwa wao, na kwenda katika mazishi yao, na kuwafariji, na mengineyo...) Hii inaashiria kwamba kinachokusudiwa hapo ni watu wa dhimma, kwani walikuwa wakiishi miongoni mwa Waislamu na walikuwa katika dhimma yao. Kisha Yahudi ambaye alitembelewa na Mtume (saw) katika maradhi yake alikuwa akimtumikia Mtume ﷺ kama ilivyoelezwa katika Hadith ya Al-Bukhari 1356 kutoka kwa Anas, (ra) أَنَّ غُلَاماً مِنَ اليَهُودِ كَانَ يَخدُمُ النَّبِيَّ ﷺ فَمَرِضَ، فَأَتَاهُ النَّبِيُّ ﷺ يَعُودُهُ، فَقَعَدَ عِندَ رَأسِهِ، فَقَالَ: أَسلِم. فَنَظَرَ إِلَى أَبِيهِ وَهُوَ عِندَ رَأسِهِ، فَقَالَ لَه: أَطِع أَبَا القَاسِمِ ﷺ. فَأَسلَمَ، فَخَرَجَ النَّبِيُّ ﷺ وَهُوَ يَقُولُ: الحَمدُ لِلَّهِ الذِي أَنقَذَهُ مِنَ النَّارِ).  “Kwamba kijana mmoja miongoni mwa Mayahudi, aliyekuwa akimtumikia Mtume (saw) alikuwa mgonjwa, basi Mtume (saw) akamjia na kumtembelea, akaketi mbele ya kichwa chake, kisha akamwambia: Silimu. Akamtazama babake naye yuko mbele ya kichwa kichwa chake, basi akamwambia:  Mtii Aba Al-Qasim (saw), basi akasilimu. Mtume (saw), akatoka huku akisema: Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliyemuepusha (kijana) na moto.” Yote haya yanaashiria kuwa yaliyotajwa katika jibu la kwanza ni makhsusi kwa madhimmi.

 - Ama dalili ya kuwa wasiwe ni wenye kutupiga vita kwa sababu ya dini na wala wasiunge mkono kutolewa kwetu... nk. Ni Aya tukufu:

لَا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ أَنْ تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ * إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ.﴿

“Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita katika dini, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu. Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Al-Mumtahina: 8-9]

Anasema Ibn Kathir katika sababu ya kuteremshwa aya hii tukufu: (Na neno lake Mwenyezi Mungu (swt) ﴿لا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ﴾ “Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu.” yaani hakukatazini kufanya wema kwa makafiri ambao hawawapigi vita katika Dini, kama wanawake na wanyonge wao, ﴿أَنْ تَبَرُّوهُمْ  “kuwafanyia wema” yaani kuwafanyia ihsan ﴿وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ﴾ “kuwafanyia uadilifu” yaani kuwa waadilifu ﴿إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴾ “Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu”... Imam Ahmad amesema: Aarim alitwambia, Abdullah bin Al-Mubarak alitwambia, Musab bin Thabit alitwambia, Aamir bin Abdullah bin Al-Zubayr alitwambia, kutoka kwa babake alisema: Kutayla alimjia binti yake Asma binti Abi Bakr na zawadi: Sinab, Aqtu (maziwa mgando) na samli, na hali yeye ni mshirikina, lakini Asmaa alikataa kupokea zawadi yake na kumuingiza nyumbani kwake, basi Aisha akamuuliza Mtume (saw) Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha: ﴾لا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ﴿“Mwenyezi Mungu hakukatazini wale ambao hawakukupigeni vita katika dini” mpaka mwisho wa Aya. Basi akamwamuru apokee zawadi yake, na kumuingiza nyumbani kwake.

Na kauli yake (swt): ﴾إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ﴿Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu.” Yaani: hakika anakukatazeni kuwafanya ni vipenzi watu hawa ambao wamekuwekeni kuwa maadui, wakawapiga vita na wakakufukuzeni, na wakasaidia kukufukuzeni, Mwenyezi Mungu amekukatazeni kuwafanya vipenzi vyenu na anakuamrisheni kuwafanyia uadui. Kisha akathibitisha adhabu kali kwa kuwafanya vipenzi, basi akasema: وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿ . “Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” Kama kauli yake: ﴾يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ مِنْكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللَّهَ لا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿ Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Al-Maida: 51].

Kwa hivyo, inajuzu kuwapongeza watu wa dhimma katika sikukuu zao kwa maneno yasiyopingana na sheria, na pia inajuzu kuwapongeza wasiokuwa watu wa dhimma miongoni mwa makafiri kwa maneno yasiyopingana na sheria, pongezi ni katika wema, lakini hili ni kwa sharti kwamba Aya hii tukufu iwe inatekelezeka juu yao, wawe hawatupigi vita katika Dini na watutoi majumbani mwetu na wakaunga mkono kufukuzwa kwetu ﴾لَا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ أَنْ تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴿ “Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita katika dini, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.” Na hivi sasa hao ni wachache... 

Nataraji hili linatosheleza, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Zaidi Mwingi wa Hekima.

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

10 Jumada al-Akhir 1443 H

13/01/2022 M

Link ya jibu hili katika ukurasa wa Amiri (Mwenyezi Mungu amhifadhi) wa Facebook 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu