Alhamisi, 01 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Barua ya Wazi kutoka Hizb ut Tahrir Australia kwenda kwa Balozi za Waislamu nchini Australia

(Imetafsiriwa)

[وَإِذَ قَالَتْ أُمَّةٌ مِّنْهُمْ لِمَ تَعِظُونَ قَوْمًا اللّهُ مُهْلِكُهُمْ أَوْ مُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا قَالُواْ مَعْذِرَةً إِلَى رَبِّكُمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ]  

Na kikundi kati yao walisema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu atawateketeza au atawaadhibu adhabu kali? Wakasema: Ili uwe ni udhuru kwa Mola Mlezi wenu, na huenda nao wakamchamngu.’” [Al-A’raf 7:164].

Tunakuhutubieni wakati ulimwengu unakusanyika dhidi ya kikundi kidogo cha watu ambao hawajapata wasaidizi wala walinzi, huku wavamizi wa Kiyahudi - waliowezeshwa na Magharibi - wakitawalisha ugaidi juu ya miji na vijiji, hospitali na shule, unyama ambao huyafanya hata mawe kulia kwa maumivu.

Licha ya uwezo wa serikali katika ulimwengu wa Kiislamu, za karibu na mbali, kuwasaidia watu wetu wanaokandamizwa katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, serikali hizi zimechagua kukaa kimya na kutazama huku uvamizi wa Mayahudi ukitekeleza mauaji yasiyokuwa ya kawaida katika Ardhi Iliyobarikiwa. Je! Hili halithibitishi kushiriki katika uhalifu huku kwa kutoa nafasi isiyo na kizuizi kwa umbile hili uaji? Ni lipi basi linaloweza kusemwa kwa yule anayetoa msaada wa kiuchumi, kisiasa na vifaa?

Tunawasilisha yafuatayo:

1. Palestina ni kadhia ya Kiislamu pekee, inayochipuza katika Iman yetu, ambayo inavuka mipaka bandia waliyoichora wakoloni Makafiri kwa nchi za Kiisilamu.

2. Mzozo nchini Palestina ulianza kama kadhia ya Kiislamu, kisha kila juhudi ilifanywa ili kuipunguza kuwa kadhia ya Kiarabu, kisha kadhia ya Wapalestina… na sasa jambo hilo limegeuka kuwa mduara kamili kama kadhia ya Kiislamu pekee inayoelezea mapambano kati ya Uislamu na ukafiri. Magharibi imejihamasisha ipasavyo, kwa hivyo ni lazima kwa Ummah vilevile.

3. Ummah nzima imehamasika kujibu kadhia hii, ukitamani kukusanyika nyuma ya kiongozi wa dhati wa Kiislamu. Kutochukua hatua kwenu kumelaaniwa sana na kunasimama tofauti kabisa na ujasiri wa Waislamu wa Palestina na kwengineko.

4. Uingiliaji kati ni lazima utokee kuitikia maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt), sio njama za Magharibi na mifumo yake ambayo imeiandaa kwa kukariri ili kupindua utashi wa Waislamu. Badilisheni usaliti wenu kwa Ummah kwa kufutilia mbali mara moja makubaliano yote ya amani, kuwafukuza wawakilishi wao, kusitisha ushirikiano wa kiusalama na kijasusi, kukomesha ushirikiano wa kiuchumi, kukata biashara katika rasilimali za nishati, kukomesha kuitambua sheria ya kimataifa ambayo hutumika kama zana mikononi mwa Wakoloni, na kufungua mipaka yenu ili kuruhusu umoja wa kijeshi wa nchi jirani za Waislamu kulizunguka umbile la Kizayuni.

5. Ikiwa mtadumu katika kubaki kama wale waliosifiwa na Mwenyezi Mungu (swt) kama:

[فَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَفْقَهُونَ]

“kwa hivyo umepigwa muhuri juu ya nyoyo zao. Kwa hivyo hawafahamu lolote.” [Munafiqun: 3], basi tunatoa wito kwa watu wenye nguvu kujitenga na watawala hawa, wawape Nusrah wale mwenye ikhlasi, waaminifu na waliojitolea kwa Uislamu na kuandamana pamoja na Ummah kufikia ukombozi wa Palestina.

H. 26 Rabi' II 1445
M. : Ijumaa, 10 Novemba 2023

Hizb-ut-Tahrir
Australia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu