Jumatatu, 27 Shawwal 1445 | 2024/05/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 [هَذَا بَلَاغٌ لِلنَّاسِ وَلِيُنْذَرُوا بِهِ]

“Hili ni Tangazo liwafikie watu, liwaonye” [Ibrahim: 52]

(Imetafsiriwa)

 

Leo, Jumatano, 18/10/2023, mhalifu wa White House, Biden, alikutana na mhalifu wa Kiyahudi Netanyahu kukagua mabaki ya ardhi ya Gaza ambayo bado hawajayaunguza, na ni silaha na vifaa gani Mayahudi wanahitaji kwa Marekani kuwapa, ili kukamilisha (sera) ya kuiunguza ardhi. Biden alisema (kwamba alitaka kuja "Israel" ili watu huko na katika ulimwengu mzima wajue kuwa Marekani inasimama na "Israel," ikionyesha kuwa Washington inataka kuhakikisha kuwa "Israel" ina kile inachohitaji kujibu mashambulizi ya harakati ya Hamas, ambayo anaikadiria kuwa amefanya kile alichoelezea kama mauaji nchini "Israel". "(Al Jazeera, 18/10/2023). Hili lilijiri baada ya mauaji yaliyofanywa na Mayahudi ya kupiga mabomu hospitali ya Baptist katika Ukanda wa Gaza, na kuwaacha mamia ya mashahidi, wengi wao wakiwa watoto na wanawake.

Biden alipangwa kwenda leo, Jumatano, kutoka Tel Aviv hadi Amman kukutana na Mfalme wa Jordan na marais wa Misri na Palestina kujadili jinsi ya kumaliza kadhia ya Palestina, kwa kuasisi dola katika sehemu iliyokaliwa kimabavu 1967 ambayo imeondolewa silaha. Kama rais wa Misri alivyosema katika mkutano na Chansela wa Ujerumani: (Ni nini kilichofanya jambo hili lifikie hivi?) Je! Kunao upeo au dola ya Palestina ambayo tumefanikiwa kuiangazia kwa zaidi ya miaka thalathini iliyopita? Hii, ni licha ya mipango na sheria mbali mbali zilizotolewa na Umoja wa Mataifa, mashirika ya kimataifa, na mipango ya Kiarabu ambayo ilijitokeza katika kadhia hii kuanzisha dola ya Palestina." (Al-Shorouk News, 18/10/2023). Walakini, mkutano huu ulifutiliwa mbali au "kuahirishwa" baada ya uhalifu wa Mayahudi kwenye hospitali ya Baptist, kama afisa mmoja wa ikulu ya White House alivyosema ("Rais Biden alifutilia mbali ziara iliyopangwa ya Jordan baada ya kuzuru Israel," ikionyesha kwamba baada ya kushauriana na Mfalme Abdullah II na kwa kuzingatia siku za kuomboleza zilizotangazwa na Rais wa Palestina wa Mamlaka ya Palestina. Rais Biden ataahirisha safari yake kwenda Jordan na mkutano uliopangwa na viongozi hawa wawili ..."

Wizara ya Afya huko Gaza ilitangaza kwamba idadi ya wahasiriwa wa ulipuaji mabomu wa 'Israel' ambao ulilenga ua wa Hospitali ya Baptist huko Gaza iliongezeka hadi mashahidi 500, ambao wengi walikuwa wanawake na watoto ... "(Al Jazeera, 18 /10/2023).

Kwa hivyo, licha ya kuungwa mkono na Marekani kwa umbile la Kiyahudi linaloikalia kimabavu Palestina, na licha ya uungaji mkono ambao Biden aliueleza wakati akimhutubia Netanyahu katika mkutano huo, ambapo alisema kuwa, "Israel" lazima iwe mahali salama kwa Mayahudi. Na nakuahidi, tutafanya kila kitu ndani ya uwezo wetu ili kuhakikisha kuwa itakuwa." Alimhakikishia zaidi Netanyahu, akisema, "Huko peke yako... hatutakuacha uwe peke yako." Kwa hivyo alisisitiza kwamba "Israel" haiko peke yake, na kwamba nchi yake inaendelea kuiunga mkono. Aliongeza, "Hatutasimama na kutofanya chochote tena ... sio leo, sio kesho, sio milele." (CBS News;; Dubai Al Arabiya Net, 18/10/2023)). Licha ya yote haya, watawala katika nchi za Waislamu wanajipendekezesha kwa Marekani na wanaiomba kufungua kivuko cha Rafah ili waweze kutoa dawa na chakula kwa watu wanaoteseka wa Gaza. Hili ndilo lililodhihiri lakini lile lilichofichwa ni kubwa zaidi! Wanatarajia kupata hili kutoka kwa Biden kama anavyotangaza, sio kwa kuashiria, kwamba anawaunga mkono Mayahudi mchana na usiku wanapolipua nyumba zenye watu ndani yake, na kulipua hospitali, na kuwauwa wagonjwa na familia zao kwa mamia, huku upigaji mabomu wa Hospitali ya Baptist unaonyesha uadui wao, katika wakati ambao Biden anahalalisha uhalifu wao na udhalimu wao wote!

Kabla ya kuwasili kwa Biden, Waziri wake wa Mambo ya Kigeni, Blinken, alikutana na wakuu wa nchi za Kiarabu, Jordan, Mamlaka ya Palestina, Misiri, Saudi Arabia, Qatar, Imirati, na Bahrain ... kabla ya kukutana nao, alikutana na Mayahudi , akifungua ziara yake kwa kusema kwamba "Anakuja mbele yenu sio tu kama Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani lakini pia kama Myahudi." Kisha majadiliano yao yakawa juu ya kufungua kivuko na kutuma dawa na chakula! Watawala walimtaka awashawishi Mayahudi kukubali kufungua kivuko cha mpakani cha Rafah!! Je! Hii sio aibu na fedheha? Je! Vikosi vyetu vinavyozunguka Palestina haviwezi kufungua kivuko cha Rafah ?! Jeshi la Jordan, jeshi ndogo zaidi yao, lina uwezo wa kuziangamiza ngome za Mayahudi, kwa hivyo vipi basi jeshi la Misri? Je! Majeshi ya Waislamu pambizoni mwa Palestina hayawezi kuikomboa?! Je! Wanahitaji kumuomba Biden kuwafungulia kivuko cha Rafah?!

Msiba wa Waislamu ni watawala wao. Wamezuia majeshi kuwanusuru ndugu zao huko Gaza al-Hashem, wamesimama na kutazama kile kinachotokea, wakihisabu mashahidi, wakiwaita "wafu". Wamewasajili majeruhi, na wameridhika na kuwasajili ... mbora kati yao ni yule anayetarajia kwamba Biden atawafungulia kivuko hicho ili waweze kusaidia kuzika wafu na kutoa dawa kwa waliojeruhiwa ... wameridhika na hilo.

[صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ]

“Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea.” [Al-Baqara: 18].

Watu wa Palestina hawahitaji dawa au chakula, lakini badala yake wanahitaji mtu atakaye wanusuru, kumsagasaga adui wao, na kuregesha fahari yao. Wanahitaji jeshi la Jordan, Ibn al-Walid, na Abu Ubaidah, ambao waliwafurusha Warumi kutoka ardhi ya Ash-Sham. Wanahitaji jeshi la Misri na Salahuddin, msindi wa Makruseda. Wanahitaji jeshi la Misri, Qutuz, na Baybars, mshindi wa Wamongolia na Matatari huko Ain Jalut ... wanahitaji Abdul Hamid II na msemo wake maarufu kwamba Palestina haiwezi kununuliwa au kuuzwa, lakini badala yake ni ya Waislamu, bila ya mamlaka juu yake kwa Mayahudi ... wanahitaji mtawala wa dhati ambaye atapambana na Mayahudi na kutimiza maneno ya mkweli na mwaminifu (saw), «لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ...» “Kwa yakini mtapigana na Mayahudi, na kwa yakini mtawauwa” kama ilivyosimuliwa na Muslim kutoka kwa Ibn Omar. Hii ni ili Palestina iweze kurudishwa kuwa yeye nguvu na isiyo shindika, kama iliyokuwa nyuma, Nyumba ya Uislamu (Dar ul Islam),iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu (swt), Mtume Wake (saw) na waumini.

Enyi Majeshi katika Ardhi za Waislamu:

Mnaweza kumuona na kumsikia adui yenu akiupiga mabomu Ukanda wa Gaza kupitia ardhini, baharini na angani na kuigeuza kuwa ardhi iliyoungua… vipi basi hamuwanusuru ndugu au kupigana?!

[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ]

Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini” [At-Tawba: 14]

Nyote  wawili mnasikia na kuona jinsi watawala wenu wanavyokukatazeni na kukuzuieni kupigana na Mayahudi; ambao wanaikalia kimabavu ardhi ya Isra' na Mi'raj, kuwafukuza watu wake kutokana nayo na kukupigeni vita katika Dini yenu, na bado wangali wanafanya hivyo. Mwenyezi Mungu (swt) anakuamuruni kupigana nao na hakuharamishini kupigana nao.

[إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَىٰ إِخْرَاجِكُمْ أَن تَوَلَّوْهُمْ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ]

“Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni tu kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Al-Mumtahana: 9].

Enyi Majeshi katika Ardhi za Waislamu:

Ardhi ya Isra’ na Mi’raj inakuiteni, itikieni wito huo. Watu wa Ukanda wa Gaza Strip wanakuombeni nusra yenu, basi wanusuruni. Msiwe miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]

“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache. Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [At-Tawba: 38-39].

H. 3 Rabi' II 1445
M. : Jumatano, 18 Oktoba 2023

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu