Jumatatu, 27 Shawwal 1445 | 2024/05/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  6 Rabi' II 1445 Na: 1445/05 H
M.  Jumatatu, 30 Oktoba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Kenya yafanya Maandamano baridi kutoa mwito kwa Majeshi ya Kiislamu Wakomboe Al-Aqsa kutoka kwa Makucha ya Umbile la Kiyahudi

(Imetafsiriwa)

Kufuatia mauaji ya halaiki yanayoendelea kufanywa na serikali ya kinyama ya kizayuni dhidi ya watu wa Ghaza, Hizb ut Tahrir Kenya iliweza kufanya maandamano baridi mnamo siku ya Ijumaa Oktoba 20,2023 katika miji ya Nairobi na Mombasa sambamba na miji mengine ya pwani.

Awali, Hizb ilikuwa imepanga kuongoza swala ya Ijumaa kwenye uwanja maarufu wa Makadara Jijini Mombasa kusimama pamoja na ndugu zao wa Palestina, hata hivyo kufuatia hali mbaya ya hewa amali hiyo ikahamishiwa msikiti wa Taqwa. Na baada ya swala ya Ijumaa, maandamano hayo yakafanywa nje ya msikiti ambapo mwito ulielekezwa kwa majeshi ya nchi za Kiislamu hususan Misri, Lebanon na Jordan yaweze kuvunja vizuizi walivyowekewa na watawala wao katika kambi zao ili waweze kunusuru operesheni ya Tufani ya Al-Aqsa kukomboa Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa kutoka kwa makucha ya walowezi wa Kiyahudi. Maandamano hayo yalitamatika kwa kufanya mkao mfupi na wanahabari kuangazia mashambulizi ya umbile la Kiyahudi dhidi ya watu wa Palestina.

Hizb ilikariri kwamba majeshi ya Kiislamu na watu wenye nguvu wana jukumu kubwa la kuunga mkono vijana wa Ardhi Iliobarikiwa. Umma wa Kiislamu aidha, ukakumbushwa jukumu lao tukufu la kubeba ulinganizi wa kuregesha maisha ya Kiislamu kwa kupitia kusimamisha Dola ya Khilafah ambayo ndiyo itakayosukuma kikweli jeshi kupambana na dola ya kizayuni na zile zinazoiunga mkono ambazo ni Amerika na Uingereza.

  [وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Al-Anfal 8:72].

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Sehemu ya Amali ya Kisimamo 1

Sehemu ya Amali ya Kisimamo 2

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu