Jumapili, 11 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  12 Safar 1437 Na: 1437/02 H
M.  Jumamosi, 28 Novemba 2015

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kanisa la Kikatoliki ni Lazima Lijue Kwamba Usekula Ndio Adui Mkuu wa Dini

Kiongozi wa kiulimwengu wa Kanisa Katoliki, Papa Francis yuko katika ziara ya kipapa barani Afrika ya siku tano. Alipokuwa nchini Kenya, Papa huyo alifanya mazungumzo na viongozi wa madhehebu mbali mbali ya kidini kuhusiana na ushirikiano na umoja wa kidini miongoni mwa dini tofauti tofauti. Pia aliukemea ugaidi na kutoa wito kwa viongozi wa kisiasa kukomesha mivutano na migogoro ya kisiasa na badala yake kuhubiri amani na utulivu. Mada hii ililengwa kusisitizwa katika ziara yake nchini Uganda. Kiongozi huyo wa Kikatoliki hatimaye atakamilisha ziara yake katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, nchi iliyo gubikwa na vita kati ya wanajeshi wa serikali ambao idadi yao kubwa ni Wakristo na kundi la Waislamu wachache la Seleka ambavyo vimepelekea uchomaji moto muovu na wa kikatili wa Waislamu wasio na hatia.

Chama cha kisiasa cha Kiislamu, Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki, kingependa kufafanua juu ya ziara hii ya Papa kama ifuatavyo:

Mazungumzo baina ya madhehebu ya kidini na imani tofauti tofauti, ni fahamu ya Kimagharibi ambayo haina msingi katika Uislamu. Fahamu hii imechipuza kutokana na itikadi ya kisekula ya kutenganisha dini na dola na kumpa mwanadamu mamlaka ya kutunga sheria na kanuni badala ya za Mwenyezi Mungu. Hii ni fahamu hatari, ambayo daima hutumiwa na mabepari wa Kimagharibi kuchochea fahamu za kimakosa kuhusu Uislamu. Lengo kuu ni kuwatongoza Waislamu kuachana na Uislamu wao kama ulivyofundishwa na Mtume Muhammad (saw), na badala yake kuukumbatia mfumo mpya wa kisekula. Sisi hatushangazwi na Papa kuongoza mazungumzo haya, kwa sababu yeye mwenyewe na waliomtangulia, walikubali kwa moyo mkunjufu kumeza sumu yenye madhara na maangamivu ya usekula iliyomlevya kufikia hadi kujipa mamlaka ya kutunga sheria kwa ajili ya wafuasi wake. Hakika, usekula umeenea pakubwa ndani ya dhehebu lake; kufikia hadi baadhi ya makasisi wake kujitangaza hadharani kuwa ni mashoga au madume jike! Kinacho tusikitisha kihakika ni kujitokeza kunako chukiza kwa baadhi ya viongozi wa Waislamu, Mwenyezi Mungu Mtukufu awaongoze, kushiriki katika jukwaa hili, lililolenga kuwapotosha Waislamu kutokana na dini yao chini ya pazia ya mazungumzo baina ya imani tofauti tofauti na uvumilivu wa kidini.       

Mzozo baina ya dini tofauti tofauti hausababishwi na Uislamu, bali mfumo wa kikoloni na serikali zake za kisekula ambazo daima huchochea uhasama. Hapa nchini Kenya, jamii ya Waislamu haina historia ya kuwalazimisha Wakristo kubeba maadili yao, mbali na hayo kanisa daima limekuwa likihubiri chuki dhidi ya mahakama za Kadhi (mahakama za Kiislamu) na kuwakataza wanafunzi wa kike wa Kiislamu kuvaa hijabu.

Vilevile tunajua kwamba Papa Francis anajisahaulisha kimakusudi kuwa viongozi wa Kidemokrasia ndio wanaopanda chuki hii ya kikabila na ya kidini ambayo hatimaye wameigeuza Afrika kuwa uwanja wa vita. Lawama na tuhuma zote za mizozo na migawanyiko ni lazima zibwagiwe mfumo wa kibepari na nidhamu yake ya kisiasa ya kidemokrasia na sio Uislamu. Licha ya kwamba Wakatoliki wamejibu wito wa Papa Benedict wa kuanzisha vita vya kimsalaba dhidi ya Waislamu. Katika karne ya 10, pindi walipoingia ndani ya neema ya utawala wa Kiislamu wa Khilafah, hakuna yeyote aliye lazimishwa kusilimu, licha ya kuwa maadili ya Wakatoliki yanaonyesha mgongano wazi na Uislamu.

Ama kuhusu shutma za ugaidi, tungeli mmiminia Papa pongezi na vigelegele, lau kama katika ziara yake ya hivi majuzi nchini Amerika, angeishutumu na kuikemea dola hiyo na kuiomba iwaondoe wanajeshi wake kutoka Mashariki ya Kati, ambako wanafanya vitendo viovu na vya kinyama vya ugaidi!  

Kwa yakini, uvamizi huu ndio kiini cha kile kinachoitwa ugaidi. Tungependa kusisitiza kuwa, baada ya kuvunjwa Muungano wa Kisovieti na Amerika, ambapo hatimaye ulipelekea kuporomoka kwa ujamaa/ukomunisti mwishoni mwa miaka ya themanini ya karne iliyopita, fahari ya Amerika imekuwa kubwa zaidi na kuipa ujasiri wa kutangaza vita dhidi ya mfumo wa Kiislamu, ambao pasi na shaka uko ukingoni mwa kusimamisha Dola yake hivi punde na itaongoza ulimwengu. Hivyo basi Amerika inatumia serikali zote vibaraka duniani, pamoja na mashirika tofauti ili kusaidia kujenga rai jumla muwafaka ili kuegemea msimamo wao wa kimakosa dhidi ya Uislamu.

Mwisho, tungependa kusema kuwa ziara hii ya Papa sio chochote ila ni jaribio ovu la kuwahadaa watu kuendelea kuwa mateka wa mfumo muovu wa kirasilimali. Wakati huo huo, kutoa vilio juu ya Uislamu na Waislamu, katika muendelezo wa kuwazuia kutokana na kuulingania kama mfumo mbadala wa urasilimali ulio na nguvu ya kukomboa ulimwengu mzima kutokana na makucha ya Urasilimali yaliyo jaa damu.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu