Jumapili, 11 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  10 Muharram 1437 Na: 1437/01 H
M.  Ijumaa, 23 Oktoba 2015

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mgogoro wa Kifedha: Thibitisho Jingine la Udhaifu wa Uchumi wa Kirasilimali

Hazina ya Taifa imekiri waziwazi kuwa Kenya kwa sasa inakumbwa na mgogoro wa kifedha. Waziri wa Fedha Henry Rotich amefafanua kuwa jumla wa mikopo ya ndani na ya kimataifa ambayo muda wake wa malipo umewadia imesababisha migogoro ya kifedha na mwendo wa kinyonga wa ukusanyaji ushuru umechangia pakubwa hali hii. Taarifa kutoka kwa Hazina ya taifa zinaashiria deni la umma kufikia Trilioni 2.8 (Deni la ndani ni Trilioni 1.42 na Deni la kigeni ni Trilioni 1.42).

Harakati ya Kiislamu ya Hizb ut Tahrir / Afrika Mashariki ingependa kuangazia yafuatayo:

Kwanza, hali hii ina waumiza raia wa kawaida ambao daima hata kabla ya tatizo hili la kifedha wangali wanateseka ndani ya lindi la umasikini. Licha ya mageuzi yote kama katiba mpya na nidhamu mpya ya utawala wa ugatuzi, umasikini ungali unamzonga mtu wa kawaida.

Pili, kuenea kwa ufisadi na ulafi wa wanasiasa ni mojawapo ya sababu kuu zinazopelekea hali hii. Katika Ripoti ya Kila Mwaka ya Kutathmini Utekelezaji wa Bajeti ya Kitaifa ya Serikali FY 2014/2015, iliyotolewa hivi majuzi inaashiria namna wanasiasa walivyo fyonza pesa za umma. Na katika ripoti nyingine muhimu kutoka kwa Mhasibu Mkuu imefichua kwamba takribani robo ya bajeti ya serikali ya Kenya ya dola bilioni 16 zilikuwa zina kosekana! Kutokana na ulafi wao, Wabunge sasa wanapanga njama ya kupitisha Mswada wa Jumuia ya Bunge la Kenya ambao utawabebesha mzigo Wakenya wa athari ya maisha ya kifahari ya wabunge hao walafi ya muda mrefu hata baada yao kuondoka katika siasa!   

Tatu, jaribio lililo dhamiriwa na Serikali la kukabiliana na migororo litaendelea kuwabebesha mzigo raia wa kawaida ambao tayari wameghubikwa na umasikini badala ya kuwaletea afueni. Serikali inalenga kukopa Ksh. milioni 78 nyingine licha ya madeni yote ya umma ya sasa.

Hili hapa janga jingine la nchi za kirasilimali lililo jengwa juu ya uchumi wa matumizi ambao usambaaji wa pesa (taslimu) unakuwa ndio jambo msingi na chombo cha kudhibiti ni riba. Fauka ya hayo, ni kupitia mikopo hii ambapo mataifa ya kilafi ya Kimagharibi humakinisha ubepari wao juu ya nchi za ulimwengu wa tatu hivyo basi kuzifanya zikose ustawi wa kiuchumi na kushindwa kuendesha hata miradi yao wenyewe ya maendeleo ilhali zinadai kuwa huru.

Mwisho, mgogoro wa kiuchumi ambao Kenya kwa sasa inakumbwa nao umefichua utawala tete wa uchumi wa kirasilimali unaobebwa na Amerika kama taifa lenye nguvu zaidi. Nidhamu iliyojengwa juu ya sera za kimakosa kama riba, ubinafsishaji wa mali za umma, matumizi mabaya ya pesa za umma ndio sababu halisi za migogoro ya kiuchumi. Hivyo basi, ili kutatua tatizo hili tunahitaji kuung'oa mfumo fisadi wa urasilimali na kutafuta suluhisho kutoka kwa mfumo mbadala ambao tunatangaza hadharani kuwa ni Uislamu. Nidhamu ya Kiuchumi ya Kiislamu ina sera msingi imara za kiuchumi zinazodhamini usimamizi barabara wa uchumi wa dola. Uislamu umepiga marufuku kuchukua au kutoa mikopo yenye riba, ushuru wa VAT na ubinafsishaji wa mali ya umma. Hivyo ni Uislamu pekee ulio na uwezo wa kukabiliana na matatizo yote ya kiuchumi ambayo hayaikumbi Kenya pekee bali ulimwengu mzima kwa jumla. 

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu