Jumamosi, 25 Shawwal 1445 | 2024/05/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Nchi Zinazozungumza Kijerumani

H.  15 Rabi' II 1442 Na: 1442 H / 02
M.  Jumatatu, 30 Novemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Nia ya Austria ya Kulazimisha Kosa la Jinai linaoitwa "Uislamu wa Kisiasa"
(Imetafsiriwa)

Chansela wa Austria Sebastian Kurz alitangaza mnamo tarehe 11 Novemba nia ya serikali kuunda kifungu kipya cha makosa ya jinai chini ya jina "Uislamu wa kisiasa", "ili iweze kuchukua hatua dhidi ya wale ambao si magaidi, lakini ambao wanaunda ardhi yenye rutuba kwao." Kwa kuongezea, mbinu mpya zitabuniwa kufunga maeneo ya ibada (yaani misikiti), kuanzisha usajili wa maimamu, na kukaza sheria inayozuia alama na vyama. Kupitia tangazo hili la kuundwa kwa kifungu kipya cha jinai chini ya jina la "Uislamu wa kisiasa", serikali ya Austria inafichua kiini halisi cha sera ya ujumuishaji wa kiimla, ambayo ni uoanishaji kamili wa kifikra na wa kivitendo wa Waislamu wanaoishi Austria.

Tangazo hili lilitanguliwa na hotuba mnamo 3 Novemba ambapo Sebastian Kurz alisema juu ya mapambano yanayoendelea "kati ya hadhara na unyama mkali", ambayo kwa suala la "magaidi", hii inatumika kwa "wenye msimamo mkali ambao wanakataa njia ya maisha ya Austria na maadili yake msingi, na vile vile kwa wale wanaokataa demokrasia." Kurz anasema: "Tutawasaka wahalifu, watu walio nyuma yao na watu wenye nia moja, na tutawafuata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria!" Katika hotuba yake katika mkutano wa Bunge uliofanyika tarehe 5 Novemba, Chansela aliweka wazi kuwa jambo hilo halihusiani tu na wale wanaofanya vitendo vya vurugu, lakini kwa wale ambao wanashirikiana nao kifikra na kupigania mfumo ulio nyuma yao, kwani alisema: "Hatuwezi na hatutakubali miundo na jamii sambamba kuweko katika maeneo ya Austria ambayo inachukia jamhuri yetu na inafanya kazi dhidi ya katiba yetu. Kituo cha Kuhifadhi Nyaraka za Uislamu wa Kisiasa na Afisi ya Shirikisho ya Ulinzi wa Katiba na Kupambana na Ugaidi (BVT) ina jukumu muhimu katika kufuatilia vyama vyenye msimamo mkali na kuvisambaratisha kwa kushirikiana na huduma za usalama ". Hii ilifuatwa mnamo 9 Novemba na utekelezaji wa "Operesheni Luxor", ambapo zaidi ya maafisa 900 wa polisi katika majimbo manne ya shirikisho walivamia vyumba zaidi ya 60, nyumba, makao makuu ya kibiashara na vyama vya mashirika ya Kiislamu.

Namna ya hotuba hizi zilizotangulia Operesheni Luxor na kisha utekelezaji wa mchakato huu inaonyesha wazi kuwa hatua zilizotangazwa sio jibu la shambulio la Novemba 2, lakini ni sehemu ya sera ya ujumuishaji ambayo inakusudia uoanishaji kikamilifu, yaani, uoanishaji wa kimfumo wa Waislamu wanaoishi Austria. Katika "Mpango wa Utekelezaji wa Kitaifa wa Ushirikiano" (NAP.I) uliopitishwa na serikali, kujitolea wazi kwa Austria na viwango na maadili yake "inachukuliwa kuwa moja ya misingi muhimu ya ujumuishaji". Pia, hatua zilizochukuliwa katika miaka ya hivi karibuni, kama vile kupiga marufuku khimar na kufunga misikiti mingi na jumuia za Kiisilamu, zilichukuliwa kwa kisingizio cha "kupigana na Uislamu wa kisiasa" na kama hatua muhimu kwa mchakato wa ujumuishaji, na walichukua uhalali wao kwa msingi huu. . Ndivyo ilivyo ripoti ya Afisi ya Ulinzi wa Katiba ya 2018, ambayo inaonyesha wazi kwamba wahusika wote katika jamii ya Waislamu wanaweza kugawanywa chini ya istilahi ya wapiganaji "Uislamu wa kisiasa." Chini ya anwani "Uislamu wa Kisiasa nchini Austria", ripoti hiyo inasema: "Wanaharakati wa Kiislamu hawavutiwi tu na mambo ya ibada ya kidini katika jamii ya Waislamu [...]. Badala yake, pia ni wachangamfu katika mambo zaidi ya hayo, kama vile elimu, utunzaji wa kijamii na mpangilio wa maisha ya kitamaduni ya Waislamu nchini Austria. "Kwa hivyo, kinyume na kile Kurz amedai, hatua zilizochukuliwa hazihusiani na kupambana na ugaidi, Bali kufutilia mbali

utambulisho wa Kiislamu na njia ya maisha ya Kiislamu. Afisi ya Ulinzi wa Katiba imetambua wazi kuwa shida kuu inayoiona katika Uislamu wa kisiasa ni (jaribio lake la kuwazuia Waislamu "wasiyeyuke"(kuoanishwa) katika jamii hii). Ili kumakinisha ufafanuzi huu katika majadiliano ya umma na kuhalalisha hatua za kisiasa kwa msingi wake, Wizara ya Mambo ya Ndani ilitangaza mnamo Julai 15 kuunda Kituo cha Kunakili Uislamu wa Kisiasa. Kwa tangazo la serikali mnamo Novemba 11, Sebastian Kurz sasa anasonga kumshambulia hadharani adui aliyetambuliwa hapo awali, na kuimarisha mateso ya adui huyu kisiasa kupitia kutekelezwa kwa kanuni ya jinai kushutumu fikra na imani.

Yote haya yanafichua kwamba serikali ya mseto inalichukulia shambulizi la Novemba 2 kama kisingizio kinachofaa ili kuimarisha sera ya uoanishaji wa kidhalimu na kuinyanyua kwa kiwango kisichokuwa cha kawaida kupitia uingiliaji kimpangilio katika kujitambulisha binafsi kwa Waislamu. Kwa hali hii, Hizb ut Tahrir katika nchi zinazozungumza Kijerumani inatoa wito kwa vikosi vyote vya kazi katika jamii ya Kiislamu kupinga kabisa maendeleo haya na kutojisalimisha kwa hatua hizi za mamlaka ya kufundisha! Jukumu hapa ni letu sote na linatuhitaji kutetea imani zetu na kuchukua msimamo wazi dhidi ya sera ya uangamizaji wa kidini unaofanywa na serikali ya Austria. Hii ni kweli haswa kwa mashirika ya Kiislamu na wawakilishi wa jamii walio na ushawishi mkubwa na uwezo mkubwa wa uhamasishaji. Ni kwa pamoja pekee ndio tunaweza kuzuia mpango huu haribifu wa kisiasa na kulinda uwepo wetu wa Kiislamu katika siku zijazo.

Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

]يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنْتُمْ مُسْلِمُونَ * وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعاً وَلَا تَفَرَّقُوا وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنْتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُمْ بِنِعْمَتِهِ إِخْوَاناً وَكُنْتُمْ عَلَى شَفَا حُفْرَةٍ مِنَ النَّارِ فَأَنْقَذَكُمْ مِنْهَا كَذَلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ * وَلْتَكُنْ مِنْكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ]

Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha; wala msife ila nanyi ni Waislamu* Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka* Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.” [Al-i-Imran: 103-104]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Nchi Zinazozungumza Kijerumani

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Nchi Zinazozungumza Kijerumani
Address & Website
Tel: 0043 699 81 61 86 53
Fax: 0043 1 90 74 0 91
E-Mail: shaker.assem@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu