Jumapili, 25 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/06/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ukuzaji wa Fikra ya Usawa wa Kijinsia Katika Asia ya Kati

Katika miaka ya karibuni, Wamagharibi kupitia taasisi za kimataifa zisizo za kibiashara na vyombo vya habari vya mrengo wa Kimagharibi, wameanza kivitendo kutekeleza fikra ya usawa wa kijinsia katika nchi za Asia ya Kati. Zaidi ya hayo, Wamagharibi wanajaribu kuhusisha kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia katika maeneo yetu, na thaqafa ya Uislamu ya karne za zamani na njia ya maisha ya watu wetu.

Ikiwa ni sehemu ya maendeleo na mafanikio ya usawa wa kijinsia katika eneo, mpango wa kuzuia unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake umeshaanzishwa, ikiwa ni pamoja na warsha mwezi wa Disemba 2019, onyesho la “Feminale” lilifanyika katika mji mkuu wa Kyrgyzstan.

Julai 6, mwaka 2020, wasichana kadhaa kutoka Uzbekistan, wanachama wa jamii inayoitwa Exponautz Art Gallery, wametuma picha kwenye Internet za mabango yaliotengenezwa kienyeji yanayohusu usawa wa kijinsia. Waanzilishi wa zoezi hilo wametoa wito wa kusaidia wasanii hao kwa kutuma picha pamoja na sahani zao juu ya maudhui iliotajwa kwenye mitandao ya kijamii, hata hivyo, watumiaji wa mitandao ya kijamii katika sehemu ya Asia kwa ujumla ilijibu vibaya zoezi hilo la kisanii la umati mkubwa. Na, japokuwa wengi wa wakaazi wa eneo hili bado wanaikataa fikra ya usawa wa kijinsia kutokana na kutafautiana na thaqafa yao, lakini bado kuna wanaoonyesha kuiunga mkono.

Madikteta wa Kisekula katika nchi za Asia ya Kati, hatimaye, pia wanaunga mkono na kukuza hatua hizo za Wamagharibi kuwatoa watu wa eneo kutoka kwenye muelekeo wa dini, na fikra ya usawa wa kijinsia inayoonyeshwa kwao kuwa ni maendeleo na mageuzi ya kijamii.

Tatizo la kutokuwa na heshima na hata wakati mwingine tabia za kudhalilisha wanawake katika jamii ya kisasa katika nchi za Kiislamu lipo wazi, lakini ni muhimu kufahamu sababu ni nini. Je, sababu kubwa ya hili ni thaqafa ya Kiislamu na njia ya maisha ya Waislamu, kama Wamagharibi wanavyodai, au kuna chengine?

Kwa hakika, Uislamu umeonyesha haki na majukumu ya wanaume na wanawake kila mmoja kwa mwenzake, na pia umewapa wanawake nafasi maalum katika jamii. Mwanamke katika Uislamu huzingatiwa ni heshima ambayo lazima ilindwe hata kwa gharama ya kutoa maisha.

Mwanamke amepewa jukumu la kulea watoto, yeye ni msimamizi wa nyumba, lakini wakati huo huo, Uislamu haumzuii mwanamke kufanya kazi, kushughulika na biashara zake na kuingia kwenye shughuli yoyote ndani ya mfumo uliowekwa na sheria za Uislamu.

Hii maana yake ni kuwa muelekeo wa sasa kwa wanawake na nafasi yake iliyo dhalilishwa kwa hakika ni matunda ya juhudi za baadhi ya nchi kwa miaka mingi kuziweka mbali nchi zetu na Uislamu, zilizopelekea kutenganishwa kwa taasisi ya familia na njia ya maisha ya Uislamu na kutozingatiwa kwa sheria za Kiislamu. Huu ndio mzizi wa matatizo yote na taabu zinazoukumba Ummah hivi leo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Firdaus Salimzoda

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu