Jumanne, 28 Shawwal 1445 | 2024/05/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Talaka ni Halali Hata Kama ni Halali Inayo Chukiwa Zaidi

(Imetafsiriwa)

Kwa kuwa ni sheria kamili, imemsimamia mwanadamu na kumpatia njia za kumuwezesha kukidhi mahitaji yake ya kiviungo na kighariza pasina na kumsababishia majonzi yeye na wanadamu wengine. Na kuweka suluhisho mwanana na zilizo kamilika kwa matatizo na mazito yote anayo kumbana nayo. Huu ni Uislamu, Dini ambayo Muumba ameiidhinisha kwa watumwa Wake ili waweze kuishi kwa kufurahi, kutosheka na kutaka radhi za Mwenyezi Mungu wao. Kama ghariza nyingine, Uislamu unaangazia ghariza ya kuendeleza kizazi na kuhifadhi wanadamu na kuashiria njia halali ya kufikia hilo. Kwa hivyo ikatambua ndoa kuwa ni mahusiano matukufu baina ya wanandoa. Fungamano lenye nguvu linalo waunganisha, Mwenyezi Mungu asema:

وَكَيْفَ تَأْخُذُونَهُ وَقَدْ أفضى بَعْضُكُمْ إلى بَعْضٍ وَأَخَذْنَ مِنكُم مِّيثَاقاً غَلِيظاً “Na mtachukuaje na ilhali mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti?" [An-Nisa: 21]

Fungamano hili ambalo kila mmoja anayemuani Mwenyezi Mungu anatakiwa kujifunga nalo na asifuate suluhisho nyingine ambazo zinakidhi ghariza hii. Na ndio maana Uislamu ukatuamrisha sisi kufanya chaguo zuri na kusisitiza kuhusu wanaume wema wawe ni kwa wanawake wema:

  وَالطَّيِّبُونَ لِلطَّيِّبَاتِ “Na wanawake wema ni wa wanaume wema" [An-Noor: 26] Kwa hivyo mahusiano haya ni dhabiti, yenye kudumu katika maisha yao.

Lakini makosa yaweza kutokea katika kuchagua ima kwa kuchagua mume au mke, ambapo inapelekea kuharibu mahusiano baina yao na kutafuta maisha inakuwa vigumu kutokana na wao kuwa na tabia tofauti au kwa sababu ya mgongano katika maslahi yao, au kukosekana kwa utulivu na mapenzi kati yao. Natija yake ni kuwa maisha yanakuwa moto usiovumilika na suluhisho lisiloepukika hujitokeza: talaka! Naam, Uislamu umeweka sheria ya talaka na kuifanya kuwa ni halali inayo chukiwa zaidi –lakini ni suluhisho la dharura katika baadhi ya hali za ndoa ambapo hakuna makubaliano baina ya pande mbili kutokana na kuwa haiwezikani kuendelea kuishi pamoja.

Ili kuihifadhi chembe chembe hii kutokana na maangamivu hatari juu yake na kwa mujtama mzima, Uislamu umeweka sheria ya talaka. Na ili kuweza kutochafua mahusiano na kutoharibu fungamano madhubuti kwa kukosekana utulivu na makubaliano baina ya wanandoa, Uislamu ukaweka talaka.  Kwa sababu Mwenyezi Mungu Anajua alivyoviumba na Anajua alivyoviweka ndani ya alivyoviumba. Mwenyezi Mungu akawahalalishia wanandoa njia ya kulifungua (kutoka katika) fungamano hilo ili wasielekee katika njia ambazo zitawapelekea kuyakiuka mahusiano yao na kumkasirisha Mwenyezi Mungu wao.

Ukristo ulipoliangazia suala hili, ili liona kuwa halikubaliki na haukuwaruhusu wanandoa kutalikiana (kuachana), kwa kuwa inalitizama kuwa ni fungamano tukufu. Mwanamume lazima aunganishwe na mwanamke mmoja kwa maisha yake yote na wanandoa lazima wawe waaminifu kwa viapo vyao vya ndoa tukufu. Kwa msingi huo ikaharamisha talaka kama sheria. Lakini ukajipata mbele ya hali ambayo wanandoa hawawezi kuishi pamoja na kuwasukuma kutafuta njia nyingine za kuishi, kila mmoja akikidhi matamanio na mahitaji yake anavyotaka. Hivyo basi, mahusiano haramu yakaanza kusambaa, mahusiano ya kifamilia kuvunjika na mujtama kuwa fisadi. Kanisa linategemea marudio yake ya kwanza, "kitabu Kitukufu" ambacho kinasema kwamba "mwanamume yeyote anayemuacha (kumpa talaka) mkewe, isipokuwa kwa makosa ya ya zinaa, ana msababishia mkewe kufanya zinaa, na yeyote anayeoa mwanamke aliyeachwa (kupewa talaka) anafanya uzinifu." Lakini kutokana na ugumu uliokumbana nao katika kutoa uamuzi juu ya mahusiano ya ndoa zilizo na matatizo. Ili lazimishwa kutunga sheria ili kuruhusu talaka. Hii ikijumuisha kufanya uzinifu kati ya mmoja wa wahusika, kukiuka utukufu wa ndoa, uwenda wazimu kati ya mmoja wa wahusika na maumivu ya kihisia ambayo hayawezi kutibika na ambayo yamekuwa ni tishio hatari kwa maisha ya ndoa na kwa watoto, au mwanandoa ameondoka katika nyumba ya ndoa bila ruhusa au kumjuza mwenziwe na kwa muda wa takribani miaka mitatu au zaidi, na pia wakati ambapo mmoja kati ya wahusika aliingia katika ndoa kwa kulazimishwa na bila ya idhini yake au kuridhia.

Huo ndio msimamo wa Kanisa ambao unaitizama ndoa kuwa ni fungamano tukufu ambalo lazima lidumu na lisivunjwe. Lakini hata hivyo, baada ya kukumbana na changamoto katika familia nyingi ambazo zilihusiana na matatizo kati ya wanandoa, ikaruhusu matukio mengi ya kuachana (kupeana talaka).

Msimamo mwingine unaopigiwa debe ni ule wa uhuru na ukombozi wa mwanamke, unaolingania kuishi bila fungamano hilo. Hivyo basi, kila mmoja anaishi anavyotaka! Msimamo ambao wanaoshikilia wanalenga kuikandamiza familia na kuivunjilia mbali.

Muandishi maarufu, Simon de Beauvoir, anaitizama ndoa kuwa ni, "gereza la milele kwa mwanamke ambalo linakata matumaini yake na ndoto zake." Anaitizama taasisi ya ndoa kama taasisi ya ukandamizaji wa wanawake inayotakiwa kuvunjwa na kupigwa marufuku. Filosofia ya ukombozi wa wanawake pia nayo inapigia debe "uhuru wa mafungamano na uhuru wa kutengana wakati wowote kati ya watu wawili; ima wawe ni wa mahusiano ya jinsia moja au jinsia tofauti." Imeleta fujo na mkorogo katika maisha, mchanganyiko wa kizazi na kuvunja familia na mujtama jumla.

Uislamu ni sheria ya Mwenyezi Mungu ambayo ni kitu bora cha kupangilia maisha ya mwanadamu. Nani anayejua kuhusu viumbe isipokuwa Muumba, na nani mbora wa kupangilia maisha yao na vitendo vyao kama si Yeye? Yeye amewawekea sheria ya ndoa ili kukidhi ghariza zao na kuendeleza kizazi na kuendelea kuzaana ili kizazi kiendelee kuwepo na maisha yao yaendelee. Na Yeye akawashajiisha wafanye chaguo zuri ili kuendeleza ndoa na kuishi katika maisha ya maelewano na utulivu. Lakini ukuruba wa mahusiano unaweza kuvurugwa na kazi za Shetani ili kuwatofautisha wanandoa, kisha kujigamba na kufurahia kufaulu hilo. Mtume (saw) alisema:

«إنّ إبليس يضع عرشه على الماء ثمّ يبعث سراياه فأدناهم منه منزلة أعظمهم فتنة يجيء أحدهم فيقول فعلت كذا وكذا فيقول ما صنعت شيئا قال ثمّ يجيء أحدهم فيقول: ما تركته حتّى فرّقت بينه وبين امرأته قال فيدنيه منه ويقول: نِعم أنت...» “Iblis huweka kiti chake juu ya maji; kisha akaitisha vikosi vyake vya kusababisha kukosekana maelewano; kilichoko karibu kwa cheo ni kile maarufu kwa kuleta mfarakano. Mmoja wao anakuja na kusema: "Nimefanya hili na hili." Na husema: "Hujafanya kitu." Kisha mwengine miongoni mwao anakuja na kusema: "Sikuwacha lolote mpaka nimeleta mfarakano baina ya mume na mkewe." Basi Shetani humuendea karibu na kumwambia: "Umefanya vyema zaidi"

Ni kazi ya Shetani. Na licha ya kuwa ni jambo lililoruhusiwa na linalochukiwa na Mwenyezi Mungu, linabakia kuwa ni halali na suluhisho baada ya majaribio yote kufeli kutatua mizozo na tofauti zilizopo na maisha baina ya wanandoa kuwa magumu. Kwa hiyo, kuivunja ndoa linakuwa ni jambo muhimu na linakuwa ni suluhisho bora kutokana na maisha baina ya wanandoa kuwa mabaya zaidi ya kuvunjwa huko.

Uislamu ulikuja na kuusafisha mujtama na machafu yote, fikra fisidifu na mahusiano ya kimakosa na kumakinisha usafi na utulivu kwa mujibu wa fikra na mahusiano yake na hivyo kukawa kusafi. Hizo ni fahamu, tiba na suluhisho zake kwa mahusiano ya wanandoa pale ambapo imefikia kuwa maisha ni vigumu kuendelea na hivyo talaka ndio njia pekee ya kutatua suala hilo kwa kuwa mahusiano yamekosa utulivu, mapenzi na kuhurumiana na badala yake ni chuki, uadui na kukosekana kwa maelewano. Mwenyezi Mungu (swt) amelizungumzia suala hilo kwa ukamilifu katika Surah, At-Talaq (Talaka) na akaiweka wazi kwa mapana ndani ya Surat al-Baqarah. Hivyo basi, hukumu Yake kuhusiana nayo (talaka) imeelezewa na kufafanuliwa kwa watu ili waweze kupeleka maisha yao kwa mujibu wa (hukumu) hizo kama anavyotaka Mwenyezi Mungu ili kuhifadhi mujtama, ambao lau chembe chembe yake moja itaingia maradhi, utasimama madhubuti ili kuhimili mashambulizi hayo na kuyashinda. Hakika, ndani ya Dini hii tukufu zimo suluhisho ambazo kupitia kwazo mujtama waweza kujikinga na madhara na kumakinisha misingi yake. Katika Uislamu, zimo kheri zote licha ya kwamba kwa mujibu wa mitizamo yetu tunaona kuwa labda hatuna manufaa au kuna uovu katika vitu au athari mbaya au mapungufu kutokana na hukumu zetu za (kiakili), kwa kuwa hatuoni siri zake na Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayejua:

وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ “Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui." [Al-Baqara: 216]

Talaka hata kama itaoneka ina ubaya ndani yake; ni nzuri kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kwa wanandoa, watoto na familia kwa ujumla. Ni bora kuliko wao kuishi pamoja –baada ya kuwa haiwezikani –kwani maisha hubadilika na kuwa moto na kuleta maovu na kukandamizana. Ndoa ni fungamano la ukaribu na madhubuti ambalo Uislamu umesisitiza lijengwe kwa nguzo madhubuti ambazo zitaweza kuhimili matatizo na tofauti watakazo kumbana nazo wanandoa na kuzitibu kwa mujibu wa vipengee walivyo tabbani na kwa mahusiano baina yao ambayo yamesimama juu ya mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kufanya kazi kumridhisha Yeye. Hili ndilo ambalo Mwenyezi Mungu ameliamrisha kwa watumwa Wake ili familia iweze kuwa na maelewano, kuhurumiana na mapenzi. Mujtama unakuwa na uwiano na kufungamanisha wanachama wake kuwa na mashindano ya kutafuta kheri na radhi za Bwana wa Mbingu na Ardhi. Na lau mahusiano haya yatakumbwa na matatizo na mapungufu basi suluhisho zipo ambazo zimeelezewa na sheria ya Ar-Rahman.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir na
Zaina Al-Saamit

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 06:53

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu