Jumapili, 11 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Muongo Mmoja Unakaribia: Mafunzo Kutoka Syria

Mapigano nchini Syria mwaka huu yatafikia muongo mmoja katika maadhimisho yake. Huku haya yakijiri, mwisho wa mchezo wa Syria sasa unakaribia wakati eneo la mwisho lililobakia – Idlib – likishuhudia vita vikali katika eneo la mwisho lililo nje ya mikono ya utawala wa Bashar al-Assad. Haikuwa muda mrefu nyuma al-Assad alikuwa akiomba msaada huku akihangaika kudhibiti nchi yote. Lakini wakati vita vikipamba moto ndani ya eneo la mwisho nchini kuna mafunzo mengi ya kujifunza katika muongo huu mmoja.

Ukosefu wa utambuzi wa kisiasa umewagharimu kaka na dada zetu wapendwa na matokeo yake hawakuweza kujuwa ni nani waliojumuisha maadui na nani walikuwa washirika. Ilhali utawala wa Ba’ath ulikuwa ni wa ukandamizaji, uungwaji mkono wake ulienea vizuri hadi nje ya Syria. Kando na madoido kutoka kwa Wamagharibi dhidi ya utawala wa al-Assad, Bashar akipatiwa ya kumfurahisha katika miji ya Wamagharibi kabla ya machafuko. Akielezewa kuwa ni mhuishaji na Hilary Clinton akisema al-Asad apewe muda nchini Syria. Matokeo yake, vikundi vingi vya waasi vilichukuwa silaha za Wamagharibi na misaada wakifikiria kuwa watasaidia njia yao dhidi ya utawala wa Ba’ath. Ilhali kiuhalisia walikuwa wanapanga njama ya kuyazima mapinduzi.

Mnamo 2012 aliyekuwa Katibui wa Ulinzi Leon Panetta, katika mahojiano na CNN akiielezea sera ya Amerika, alisema: “Ninafikiri ni muhimu wakati Assad atakapoondoka, na ataondoka, kujaribu kuhifadhi utulivu ndani ya nchi hiyo. Njia nzuri ya kuhifadhi utulivu huo ni kudhibiti jeshi na polisi kwa kiwango kikubwa kwa kadri inavyowezekana, pamoja na vikosi vya usalama, na kuwa na matumaini kwamba watafanya mpito kuelekea serikali ya kidemokrasia. Hilo ndio jambo muhimu.”

Lengo la Marekani lilikuwa ni kudumisha utawala, kwa kuwepo au bila ya kuwepo al-Assad. Makundi ya uasi yalioungana na Wamagharibi hatimaye walilazimika kusaini makubaliano ya kusimamisha vita pamoja na utawala, kwa kuwa hawakupatiwa silaha za kutosha, na kisha wakahudhuria makongamano Riyadh, Geneva, Vienna na Astana na kujadiliana na utawala moja kwa moja.

Uingiliajikati wa moja kwa moja wa Wamagharibi ukiongozwa na Amerika ulikuwa na athari ndogo, kwa kuwa mengi ya makundi hayakuchukuwa msaada kutoka Amerika. Kwani Amerika iliyatumia mataifa jirani ya karibu kuyasimamia maeneo tofauti ya Syria na makundi ya waasi yanayopigana ndani yao. Uturuki ikisimamia Syria kaskazini na ikipangilia kuwaingiza kwenye Jeshi Huru la Syria (FSA). Saudi Arabia imeyapatia silaha na fedha makundi ya fikra za kisalafi yaliyoko Kusini mwa Syria.  Saudia hatimaye imeyalazimisha makundi haya kuingia kwenye mazungumzo ya Vienna. Qatar pia ilianza kuwasaidia baadhi ya makundi ya waasi likiwemo la muungano ujulikanao kama Jeshi la Ukombozi, iliweza pia kuendesha kambi ya mafunzo ya waasi nchini mwake.

Ilikuwa ni Qatar iliyopanga mkakati wa Ulaya wa kundi la “Marafiki wa Syria” ambalo lilikuwa ni jaribio la kuanzisha mchakato sambamba na wa Amerika, Qatar iliwalazimisha viongozi wote wa waasi kushiriki, baada ya mkakati huu kutofanikiwa makundi yote yalijiunga na mchakato wa Geneva. Jordan iliyasaidia makundi ya waasi katika Mamlaka ya Deraa ikiwemo Kundi la Kusini la FSA. Hatimaye Jordan ilipunguza msaada wake kwa kundi na kuyapatia silaha makundi yaliyopigana na makundi ya waasi yaliyoegemea zaidi kwenye fikra ya Uislamu.         

Kila moja katika nchi hizi inasaidia kundi fulani katika eneo fulani, wanahakikisha kuwa makundi haya hayajienezi nje ya maeneo yao na Amerika inahakikisha hakuna katika nchi hizi zinazosaidia makundi ya waasi inakuwa na nguvu kubwa. Makundi ya waasi yamepatiwa silaha za msingi tu, hawakupatiwa kattu silaha nzito ziwezazo kuleta mabadiliko, kwa hivyo hawatoleta mabadiliko. Kukosa msaada wa silaha nzito hatimaye imelazimisha takribani makundi yote ya waasi kuingia kwenye makubaliano ya kusitisha vita na utawala kwa kuwa hawakuweza kuwashinda wapiganaji wanaoungwa mkono na al-Assad. Makubaliano yanahusisha kukusanyika Idlib, ambayo sasa inapigwa mabomu. Kuna mawasiliano ya moja kwa moja baina ya makundi ya waasi na nchi husika zinazozunguka eneo. Kila mataifa jirani ya kieneo yanapoingilia zaidi Syria, ndipo makundi ya waasi yanavyopoteza zaidi maeneo yao. Mataifa haya hayakutaka kuwachwa nyuma wakati yakiona nchi wapinzani zikimimina fedha na silaha Syria.

Qatar na Saudia inaona uwepo wa Iran kuwa ni tishio na nchi hizi mbili kila moja inamtizama mwenzake kuwa ni tishio. Amerika imeweza kuzitumia nchi zote hizi kwa ajili ya malengo yake kwa kuwa nchi zote hizi zinafuata malengo yao finyu ya upeo mdogo.

Kwa upande wa Uturuki katika Syria kaskazini, ni hali ya kuhuzunisha wakati majeshi ya Uturuki yalipoingia Syria, makundi ya waasi yalibaki kupoteza maeneo na hivi sasa yanabaki kupigana kuhifadhi maisha yao tu katika Idlib. Uturuki haiwezi kuangalia zaidi ya Wakurdi na kumiminika kwa Waislamu ndani ya Uturuki kwani hii itaathiri nafasi ya Erdogan ndani ya Uturuki.  

Mwisho wa mchezo nchini Syria ndio unakamilika hivi sasa na hakuna shaka kuwa haya hayatokuwa ni mapinduzi ya mwisho katika ulimwengu wa Waislamu na hii ndio sababu ya mafunzo yake muhimu yanasomwa. Funzo muhimu zaidi ni kuwa licha ya kuipoteza Syria, sisi tukiwa ni Ummah, tunachohitaji ni kufaulisha mapinduzi yetu kwa mara moja tu. Maadui wa Uislamu wanahitaji kufanikiwa mara zote.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Adnan Khan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 06:40

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu