Jumatatu, 27 Shawwal 1445 | 2024/05/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

[إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَنْ كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ]

“Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.” [Qaf: 37]
(Imetafsiriwa)

Enyi Watu... Enyi Waislamu... Enyi Wanajeshi katika Majeshi ya Waislamu:

Mnamo Jumamosi, 11/11/2023, takriban watawala sitini wa Kiarabu na wasiokuwa wa Kiarabu wa nchi za Waislamu walikutana jijini Riyadh kujadili uvamizi wa Mayahudi dhidi ya Gaza, yaani zaidi ya mwezi mmoja baada ya uvamizi wa Mayahudi kuanza, na baada ya mashahidi zaidi ya elfu kumi na moja na Karibu elfu thelathini kujeruhiwa. Ni kana kwamba watawala hawa walikuwa wakingojea Mayahudi kutenda uhalifu mwingi kadri wanavyoweza dhidi ya watu wa Gaza! Watawala hawa, kutokana na idadi yao kubwa, walijaza skrini za vyombo vya habari! Kisha wakaanza kuongea na kutaja ukatili wa umbile la Kiyahudi huko Gaza. Wengine walisema: Suluhisho la mzozo huo ni suluhisho la dola mbili ... Kuzingirwa kwa Gaza ni lazima kuondolewe ...

Tunataka Baraza la Usalama lichukue majukumu yake ya kuzuia vita kwa watu wetu ... tunataka vivuko vifunguliwe ili kuleta misaada ya kibinadamu kwa watu wa Gaza ... 'Israel' inatekeleza adhabu ya kijumla ... hali hiyo ni ya janga na ya kushtua huko Gaza ... Upigaji mabomu hospitali, shule, na taasisi ni jinai ... Tunataka kusitishwa mara moja kwa mapigano ... 'Israel' inawajibika kwa ukiukwaji dhidi ya raia ... umbile la Kizayuni lilikiuka sheria za kimataifa na kutumia Silaha zisizoruhusiwa ... Marekani inalisaidia umbile hilo na silaha ... na mmoja wao akatuma salamu kwa upinzani huko Gaza, nk. Haya ni maneno yasiyo na maana, na hayaungi mkono Gaza au kukomesha uvamizi dhidi yake! Mfano wao wa wazi zaidi ni jinsi alivyotuma salamu kwa upinzani huko Gaza huku akitazama kwa mbali! Wanamuuliza nani kuondoa uzingirwaji, kukomesha shambulizi dhidi ya Gaza, na kufungua vivuko ... wakati wao wamekaa?!

Halafu, baada ya kila mmoja wao kukunja karatasi ambayo hotuba zao ziliandikwa na kisha kufunga mkutano, walitoa taarifa yao, ambayo ilikuwa hoja ya hotuba zao mwanzoni mwa mkutano huo, wakilaani uvamizi huo ... wakiuelezea kama ukiukaji wa sheria ya kimataifa ... na kulitaka Baraza la Usalama lichukue uamuzi mkali na wa lazima ambao unakomesha na uchokozi na mamlaka ya uvamizi wa kikoloni ambayo inakiuka sheria za kimataifa, sheria za kimataifa za kibinadamu, na maazimio ya uhalali wa kimataifa. Taarifa hiyo ilitoa wito wa "kuvunjwa kwa mzingiro wa Gaza na kulazimisha uingiaji wa misafara ya misaada ya kibinadamu ya Kiarabu, Kiislamu, na ya kimataifa." Na kuwapa majukumu mawaziri kadhaa wa mambo ya kigeni kuanzisha hatua za kimataifa za kuzuia vita dhidi ya Gaza; kulaani kuhamishwa kwa karibu watu milioni moja na nusu kutoka kaskazini kwenda kusini mwa Ukanda wa Gaza; kulaani operesheni za kijeshi zilizozinduliwa na vikosi vya uvamizi dhidi ya miji na kambi za Palestina: kulaani mashambulizi ya 'Israel' kwenye maeneo matakatifu ya Kiislamu na Kikristo huko Al-Quds; Kuthibitisha tena kushikamana na amani kama chaguo la kimkakati; Suluhisho kamili ambalo linahakikisha umoja wa Gaza na Ukingo wa Magharibi, dola huru ya Palestina huku Mashariki ya Al-Quds (Jerusalem) ikiwa kama mji mkuu wake, kwenye mipaka ya Juni 4, 1967!

Na hivyo ndivyo ulivyokuwa mkutano wao, hotuba zao, kufunga kwao, na kisha taarifa yao ... haikuleta tofauti yoyote kuhusiana na uhalifu wa Mayahudi katika kuwauwa watoto, wanawake, na wazee, na hata kubomoa hospitali, misikiti, nyumba, mawe, Na miti! Sio hivyo tu, bali walikata umeme na kuzuia mafuta na dawa kufikia hospitali na wagonjwa walio ndani yake, na kusababisha vifo zaidi. Maiti zilizorundikana kwenye sakafu za hospitali, familia zikishindwa kuzizika. Yote haya yalionekana na kusikika na watawala katika nchi za Waislamu!

Enyi watu ... Enyi Waislamu ... Ewe Wanajeshi katika Majeshi ya Waislamu:

Je! Watawala hawa wanawezaje kutogundua au kutoelewa kuwa uvamizi wa jeshi la adui unahitaji jeshi kuisimamia dhidi yao na kuwaondoa wale walio nyuma yake?

[فَإِمَّا تَثْقَفَنَّهُمْ فِي الْحَرْبِ فَشَرِّدْ بِهِمْ مَنْ خَلْفَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ]

“Basi ukiwakuta vitani wakimbize walio nyuma yao ili wapate kukumbuka.” [Al-Anfal: 57]

Je! Wanawezaje kutotambua kuwa yeye ambaye amedhalilishwa na kulaaniwa ataendelea katika ukatili wake ikiwa hakuna mtu kusimama dhidi yake? Vipi?! Kumzuia adui kunafanywa kwa hotuba zilizopambwa kutoka kwa watawala wa Waislamu badala ya kuhamasisha majeshi kupigana nao? Je! Hawajasikia maneno ya Mwenyezi Mungu al-Qawi al-Aziz (Mwenye nguvu na imara):

[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ]

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini” [At-Tawbah: 14].

Wanawezaje kutotambua kwamba Palestina ni ardhi ya Msikiri wa Al-Aqsa Mosque ambao Mwenyezi Mungu amebariki viunga vyake?

[سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ]

“SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka” [Al-Isra’: 1].

Je! Suluhisho la dola mbili ambalo watawala hawa wanalilingania sio usaliti kwa Mwenyezi Mungu, Mtume wake, na waumini? Je! Ardhi ya Uislamu inakubali kugawanywa baina ya watu wake na maadui zake? Je! Kundi la nchi miongoni mwa nchi za Waislamu zinazoizunguka Palestina hazina wanajeshi wenye uwezo wa kulifunga umbile hili ovu linaloikalia kimabavu Palestina na kuwafukuza watu wake kutoka kwake? Je! Wanajeshi wa Kiislamu hawana uwezo wa kuliondoa umbile hili na kuiregesha Palestina kwa ukamilifu kama ilivyokuwa mwanzoni kwa mara nyingine tena Dar ul-Islam (Nyumba ya Uislamu)? Je! Yule anayeikalia kimabavu ardhi ya Waislamu na kuwafukuza watu wake kutokana nayo hastahili kupigwa vita na majeshi ya Waislamu na kufukuzwa kutoka humo kama walivyowafukuza watu wake?

[وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُمْ مِنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ] “Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni” [Al-Baqarah: 191]. Wanawezaje kutotambua kwamba hii ni fardhi kubwa?

Hapana shaka kuwa watawala hawa wanajua, lakini unyonge wao umewazidi nguvu. Wako kwa huruma ya wakoloni wa Makafiri, haswa Marekani. Wanarudia maneno ya nchi za wakoloni makafiri na kufuata matendo yao, na hawakataa matakwa yao ili kuhifadhi viti vyao vibovu.

[قَاتَلَهُمُ اللَّهُ أَنَّى يُؤْفَكُون] “Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?” [Al-Munafiqun: 4].

Enyi watu ... Enyi Waislamu ... Ewe Wanajeshi katika Majeshi ya Waislamu:

Janga la Ummah huu ni watawala wake. Wanashuhudia miili ya mashahidi kwa macho yao wenyewe, wanasikia mayowe ya watoto kwa masikio yao, na wanaona uhamishwaji wa watu kutoka nyumba zao na watoto wao na wanawake katika mandhari za kuatua moyo. Watawala hawa wameshuhudia haya yote, na yaligusa masikizi na macho yao, lakini hayakugusa ushujaa wa al-Mu'tasim! Yote haya ni katika wakati ambao wao ndio wanaolizunguka umbile la Kiyahudi mithili ya bangili mkononi, na ilhali bado hawahamasishi jeshi au kujibu wito wa msaada ... wamezoea kudhalilishwa, wao ni mithili ya wafu, wasiohisi maumivu!

Enyi watu ... Enyi Waislamu ... Enyi Wanajeshi katika Majeshi ya Waislamu:

Je! Hamumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake? Je! Nyinyi sio watoto wa Ummah bora aliyewahi kuletwa kwa wanadamu? Je! Nyinyi sio wana wa Mujahidina wakombozi wanaoeneza kheri kote ulimwenguni? Je! Nyinyi askari sio watoto wenu? Je! Hamuwezi kuwashinikiza kupigana, kwa kuwa wanao uwezo, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kufikia haki na kuwapa Nusrah (msaada) ndugu zao katika Ardhi Iliyobarikiwa.

[وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ] “Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal: 72].

Kumbilieni Enyi wanajeshi, kuwanusuru ndugu zenu huko Gaza ambao wanapigana na umbile la Kiyahudi ambalo limeinyakua Ardhi Iliyobarikiwa. Kimbilieni enyi wanajeshi, kupigana na wale waliodhalilishwa na kulaaniwa na kukasirikiwa na Mwenyezi Mungu. Kimbilieni enyi wanajeshi, kuiregesha Palestina kwa jumla kwa Uislamu na Waislamu. Kimbilieni enyi wanajeshi, kwenye ushindi (nasr) kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ufunguzi wa karibu, na muwape habari njema kwa waumini.

Enyi watu ... Enyi Waislamu ... Enyi Wanajeshi katika Majeshi ya Waislamu,

[إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَنْ كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ] “Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.” [Qaf: 37].

H. 28 Rabi' II 1445
M. : Jumapili, 12 Novemba 2023

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu