Jumatano, 16 Safar 1446 | 2024/08/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Yaandaa Maandamano mjini Al-Qadarif Kutaka Kukomeshwa kwa Vita na Umwagaji damu ya Waislamu

Mnamo siku ya Ijumaa, Agosti 2, 2024, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iliandaa maandamano katika mji wa Al-Qadarif baada swala ya Juma’a karibu na Jami’ Al-Atiq (Msikiti Mkongwe) katika Soko la Al-Qadarif. Maandamano hayo yalitaka kukomeshwa kwa vita na umwagaji damu ya Waislamu.

Soma zaidi...

Wale Ambao Hawakufa kwa Risasi za Vita Walikufa ndani ya Makaazi ya Serikali!

Sudan Tribune iliripoti jana, Jumamosi, Julai 27, 2024, ikinukuu taarifa iliyotolewa na Kamati ya Maandalizi ya Umoja wa Madaktari wa Sudan, iliyosema: “Kamati ya Maandalizi ya Umoja wa Madaktari ilisema katika taarifa iliyopokelewa na Sudan Tribune kwamba watu waliokimbia makaazi yao mjini Kassala wanaishi kwenye mahema yaliyochakaa na kuzungukwa na maji kila upande, na watoto wao wanalia kwa njaa. Iliongeza kuwa hali imekuwa mbaya zaidi, kwani watoto wawili walikufa kwa shoti ya umeme, na kuna vifo kutokana na kuumwa na nyoka na kesi zingine zisizojulikana.”

Soma zaidi...

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Tufani ya Twitter “Enyi Umma; Kilio Wanacholia Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!”

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir yaandaa Tufani ya Twitter kwa kichwa: “Enyi Umma; Kilio Wanacholia Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!” ili kuwanusuru wabebaji ulinganizi wenye ikhlasi wanaonyanyaswa na utawala dhalimu wa Uzbekistan.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu