Marekani, kupitia Usitishaji vita, Inafikia Malengo Mawili Muhimu kwa Uvamizi wa Kiyahudi: Kuondolewa kwa Vikosi vya Hezbollah vinavyoungwa mkono na Iran Kaskazini mwa Mto Litani, na Kutenganishwa kwa Pande Mbili!
- Imepeperushwa katika Hizb ut-Tahrir
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 27 Novemba 2024, usitishaji vita ulitangazwa katika upande wa Lebanon kati ya umbile la Kiyahudi na Hezbollah. Moja ya masharti yake ilikuwa kwamba umbile la Kiyahudi lingeondoa jeshi lake linalovamia kutoka kusini mwa Lebanon ndani ya miezi miwili, huku Hezbollah ingerudisha nyuma majeshi yake kaskazini mwa Mto Litani. Makubaliano hayo pia yalivipa vikosi vya Kiyahudi uhuru wa kutembea kusini endapo chama hicho kitakiuka makubaliano hayo, sambamba na kuendelea na safari za ndege za adui katika anga ya Lebanon kwa ajili ya uchunguzi na ujasusi.