Hotuba Inayohusu Bendera za Rayah na Liwaa za Mtume (saw) Ilipambwa kwa Takbira na Machozi katika Soko Kuu la Port Sudan
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilitoa hotuba yake ya kisiasa ya kila wiki, iliyokuwa na kichwa: “Je, Mtume (saw) alikuwa na bendera na Rayah?”, mnamo Jumatatu tarehe 28 Jumada al-Akhirah 1446 H sawia na 30/12/2024 M. Ustadh Muhammad Jami’ (Abu Ayman), Msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, alizungumza akisisitiza kuwa bendera ya Liwaa na Rayah katika Uislamu ni suala la dini, itikadi, mfumo na nembo ya Uislamu. Mtume (saw), ana benera (Liwaa) nyeupe kama bendera ya amiri jeshi, na bendera (Rayah) nyeusi kwa makamanda wa majeshi na vikosi, na inaitwa Uqab, zimeandikwa juu yazo “La Ilaha illa Allah Muhammad Rasulullah”.