Ewe Hamasa ya Uislamu ndani ya Umma wa Muhammad (saw) Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: “Si Muumini anayelala ameshiba na hali jirani yake ana njaa.”
- Imepeperushwa katika Palestina
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Miti na mawe yamelia kutokana na hofu iliyotusibu. Vifua vyetu vinatoa damu na maumivu, watoto wetu wanasisimka kutokana na njaa na kiu, wanawake wetu wanalia ili kuchochea wivu wa ulinzi wa waumini. Asiyeuawa kwa kupigwa mabomu hufa kwa njaa na kiu. Lakini maumivu ya usaliti ni mazito juu yetu kuliko milipuko ya mabomu, njaa, na kiu. Kaka na dada zenu mjini Gaza wanatangatanga bila malengo, bila makaazi, sauti zao zimenyamazishwa na udhaifu ulioletwa na njaa na kiu, baada ya kutoweka matumaini yote kwamba yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu atakuja kuwasaidia. Wanapiga kelele: Uko wapi Umma wa Uislamu? Iko wapi hamasa ya Dini? Uko wapi msaada wa Waumini?