Jibu la Swali: Matukio nchini Syria na Kuanguka kwa Utawala wa Assad
- Imepeperushwa katika Maswali ya Kisiasa
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Asharq Al-Awsat ilichapishwa mnamo tarehe 8 Disemba 2024: (Utawala wa Assad umeanguka: Upinzani wa Syria umetangaza leo, Jumapili, kwamba umeikomboa Damascus na kuupindua utawala wa miaka 24 wa Rais Bashar al-Assad. Taarifa ya upinzani kwenye televisheni ya taifa ilisomeka: “Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu, mji wa Damascus umekombolewa na dhalimu Bashar al-Assad amepinduliwa.” Upinzani uliongeza kuwa wafungwa wote wameachiliwa huru.)