Jarida la Al-Waie: Vichwa Vikuu vya Habari vya Toleo (472)
- Imepeperushwa katika Jarida la Al-Waie
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Shambulizi la silaha jijini Washington, D.C. wiki moja iliyopita—ambapo Rahmanullah Lakanwal, raia wa Afghanistan, anatuhumiwa kuwafyatulia risasi Walinzi wawili wa Kitaifa wa Marekani—lilitokea karibu na kituo cha Metro cha Farragut Magharibi, mita mia chache tu kutoka Ikulu ya White House, eneo ambalo kwa kawaida linalindwa na baadhi ya tabaka kali zaidi za usalama. Kutokana na ufyatuaji risasi huo, Sarah Bäckström, mlinzi wa Kitaifa wa miaka 20, aliuawa na Andrew Wolf alijeruhiwa vibaya.
Rais wa Marekani Donald Trump alituma barua iliyoandikwa kwa mkono kwa kiongozi wa Syria Ahmed Sharaa, akisisitiza uungaji mkono wake na kuahidi msaada wa Marekani. Barua hiyo iliwasilishwa Damascus kupitia Tom Barrack, mmoja wa washirika wa karibu wa Trump na mfanyibiashara wa kimataifa. Picha ya wakati Trump alipokutana na Sharaa katika Afisi ya Oval iliambatanishwa na barua hiyo. Trump aliandika barua ifuatayo kwenye picha hiyo kwa mwandiko wake mwenyewe: “Ahmed, utakuwa kiongozi mzuri, na Amerika itasaidia!” (Mashirika, 3 Disemba 2025)
Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon inamuomboleza: Mwanachuoni mtukufu, khatib, sheikh, mwandishi, na mshairi, Marwan al-Khatib (Abu Muhammad)
Mnamo Alhamisi, 27/11/2025, vikosi vya usalama vya Mahouthi vilimkamata Saddam Ali Qa’id al-Mukirdi, mwenye umri wa miaka 28, kutoka wilaya ya Ṣabr al-Mawadim katika Mkoa wa Taiz ulio chini ya udhibiti wa Mahouthi katikati mwa Yemen. Kukamatwa huku ni kwa pili, kufuatia kukamatwa kwa ndugu Osama na Mohammad Mas’ad Al-Wurafi katika Mkoa wa Ibb mnamo 21/11/2025, baada ya kugawanya toleo lenye kichwa: “Trump Awaongoza Wafuasi Wake Miongoni mwa Watawala katika Ardhi za Waislamu kwenye Mpango wa Fedheha na Aibu, Wanaosujudu Vichwa Vyao Nyuma Yake kwa Kuiweka Gaza ya Hashim Chini ya Udhamini na Ukoloni.”
Mnamo Jumamosi, 29/11/2025, vikosi vya jeshi vya Kikosi cha Ulinzi cha Hadramawt chenye uhusiano na Amr bin Habrish Al-Ali viliingia katika vituo vya mafuta vya Petro Masila katika Bonde la Hadramawt, vikinyanyua kauli mbiu ya kulinda vituo vya mafuta, huku vikiwaondoa wale waliokuwa hapo vikosi vya kawaida vya jeshi vilivyokuwa na uhusiano na Baraza la Octet.
Tangu Marekani ilipovamia mwaka wa 2003 hadi sasa, Iraq imekuwa ikizama katika matatizo, na hali yake inazidi kuwa mbaya. Yote hayo ni matokeo ya ramani ya kisiasa ambayo mvamizi Marekani aliiunda na kuilazimisha. Ndiyo iliyoweka misingi ya mfumo huo na kuchora ramani ya kisiasa ya nchi hii, ikiudanganya umma wa Iraq kuamini kwamba suluhisho la matatizo yanayozalishswa na mfumo huu ni masanduku ya kura.
Katika wakati ambapo vyama tawala vinajiandaa kushindana katika uchaguzi na ngawira zake zilizopangwa kufanyika Novemba 11 mwaka huu, vikosi maalum, vifaru, na magari ya kivita, alfajiri ya Ijumaa, 22/08/2025, vilizingira Hoteli ya Lalezar katikati ya Sulaymaniyah na kuivamia, ili kutekeleza operesheni ya kumkamata mkuu wa Chama cha Jabhat Ash-Sha’ab, Lahur Sheikh Jangi. Baada ya mapigano makali ya silaha yaliyodumu kwa masaa mengi kati ya Vikosi vya Kupambana na Ugaidi na Vikosi Maalum (Commandos) na “Asayish,” vikosi vya usalama vilivyounganishwa na Muungano wa Uzalendo wa Kurdistan upande mmoja, na walinzi wa Sheikh Jangi upande mwengine, yalimalizika kwa kukamatwa kwa Lahur na kaka yake Pulad, na kusababisha vifo na majeraha.
Tangu Jumamosi iliyopita, mkoa wa Erbil umekuwa ukishuhudia mvutano wa kiusalama kufuatia maandamano ya makabila ya Herki katika wilaya ya Khabat, yakikituhumu Chama cha Kidemokrasia kwa kukaidi ahadi zake za kuwapa viti vitatu bungeni kwa badali ya kabila hilo kuwapa kura zao katika uchaguzi. Maandamano hayo kisha yakageuka kuwa mapigano kati ya makabila ya Herki na vikosi vya usalama, na kusababisha vifo na majeraha. Katika tukio muhimu, kabila hilo lilitangaza uhamasishaji wa jumla huko Erbil, na waandamanaji wakachoma makao makuu ya Chama cha Kidemokrasia cha Kurdistan katika wilaya hiyo leo, Jumatatu.