Hatari ya Uhamisho Inayotafutwa na Trump na Umbile la Kiyahudi Inalazimu Hatua Kali katika Kuamiliana nao kama Maadui
- Imepeperushwa katika Jordan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Utawala wa Jordan na kundi la watu wake wakati wote wa vita vya Kiyahudi dhidi ya Gaza walikuwa na bado wangali wanatetea kutowanusuru watu wa Gaza kijeshi, na angalau sio kufutilia mbali makubaliano ya udhalilishaji na aibu na umbile la Kiyahudi, lakini kwa busara na hekima na ujanja wa kisiasa hii ni hatua na udhoofishaji wa amani, usalama na chemchemi ya utulivu ambayo Jordan inaishi ndani yake. Mfalme alifikiri kwamba Uingereza ilimuamuru kurukuu na kujibu ajenda ya Amerika ambayo imelitawala eneo hilo tangu aingie madarakani, kufuatia mbinu ya baba yake, na kile ilichomuagiza kuhitimisha makubaliano ya pamoja ya ulinzi nayo mwaka 2021 ambayo yanahujumu kila maana ya ubwana wa nchi yoyote, na kuifungua nchi kwa ujumla kwa kambi za Amerika pekee na viwanda na vikosi vyake.