Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Gaza: Mwaka Mmoja ndani ya Mauaji ya Halaiki, Na Hakuna Msaada kutoka kwa Vikaragosi vya Magharibi

Ni dhahiri kwamba mwaka mmoja baada ya kuanza kwa mauaji ya halaiki, viongozi wa Waislamu hawajaweza kukata kamba wanazoshikilia mabwana zao. Kwa kufanya hivyo wanauthibitishia Ummah kwamba wao hawasimami pamoja na Waislamu. Wanasimama na pamoja uvamizi, na dola za Magharibi. Kwa hiyo ni wakati wa Ummah kuamka kama kizazi kipya. Ni wakati wa Umma kuungana chini ya Dini moja, bendera moja, kiongozi mmoja. Ni wakati wa sisi kuacha kuomba amani na usitishaji vita na kuanza kuitisha suluhisho halisi.

Soma zaidi...

Kufahamu Uke na Uume katika Uislamu

Mtazamo wa Kimagharibi kuhusu jinsia unasalia kuwa umejaa ukinzani na unafiki, hasa unapotazamwa kupitia jicho la matukio ya hivi majuzi kama vile sintofahamu inayomhusisha bondia wa Algeria kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris. Bondia huyo ambaye ni mwanamke kibaiolojia, amekosolewa na baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za Magharibi na mamlaka za michezo kwa madai ya kumiliki viwango vya juu vya homoni za “kiume” na kupendekeza kuwa asiruhusiwe kushindana na wanawake wengine.

Soma zaidi...

Marekani Inatafuta Ushindi Madhubuti nchini Afghanistan

Serikali ya Marekani, kupitia taasisi za kimataifa, hasa Umoja wa Mataifa, inalenga kupata ushindi madhubuti. Ni ushindi ambao haikuweza kuupata, licha ya zaidi ya miaka ishirini ya vita dhidi ya Uislamu na Mujahidina nchini Afghanistan. Utafutaji ushindi huu ulianza pale Marekani ilipoiruhusu Qatar kuwa mwenyeji wa vuguvugu la Taliban, na kufungua afisi kwa ajili ya vuguvugu hilo huko Doha mwaka 2013. Kupitia afisi hii, Marekani ilijihusisha kisiasa na harakati hiyo, na kusababisha duru kadhaa za mazungumzo yaliyohusisha Marekani na waamuzi, ukiwemo ujasusi wa Pakistan.

Soma zaidi...

Kwa Mujibu wa Uislamu, Hairuhusiwi Kugombea, au Kupiga Kura kwenye Chaguzi za Kidemokrasia

Ushiriki wa Muislamu katika Demokrasia ni jambo lenye kuwashughulisha watawala, wanasiasa, wasomi na watungaji sera. Hii ni ima Waislamu wakiwa katika Ulimwengu wa Kiislamu, au wakiishi ughaibuni katika nchi za Magharibi. Hivyo kuna mjadala kuhusu ushiriki wa Muislamu katika Demokrasia nchini Australia, Uingereza na Amerika, kama ulivyo mjadala kuhusu ushiriki wa Waislamu katika uchaguzi nchini Uturuki, Pakistan na Misri.

Soma zaidi...

Marufuku ya Hijab ya Ubelgiji: Kutopendelea upande wowote kama Haki mpya ya Kimungu (Droit Divin)

Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR) imeidhinisha marufuku ya Ubelgiji ya kuvaa hijab shuleni, uamuzi ambao umezusha mijadala kuhusu uhuru wa kidini na usekula barani Ulaya. Mahakama ilipata kwamba marufuku hiyo, iliyokusudiwa kuhakikisha ‘kutopendelea upande wowote’ katika elimu ya umma, haikiuki Mkataba wa Ulaya wa Haki za Kibinadamu. Kesi hiyo ilianzishwa na mwanafunzi mmoja Muislamu ambaye alidai kuwa sera hiyo inakiuka haki zake za uhuru wa dini na elimu. Hata hivyo, ECHR iliamua kwamba marufuku hiyo ilihalalishwa na haja ya kudumisha ‘kutopendelea upande wowote,’ kama ilivyotarajiwa.

Soma zaidi...

Zama za Mitandao ya Kijamii: Ufichuaji wa Uongo

Kuibuka kwa mitandao ya kijamii, watu wamejikuta wakiweza kuunganika na walioko maeneo mengine ya dunia. Hili liliyapa faida makampuni na serikali hadi ilipotumika dhidi yao. Wakati mauwaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina yalipoanza, watu wa Gaza waliweza kuunganika kwenye majukwaa kama ya TikTok na kuchapisha picha na video juu ya hali ya sasa.

Soma zaidi...

Katika Historia nzima ya Kijeshi ya Kiislamu, Makamanda wa Kijeshi wa Kiislamu Waligeuza Mawimbi ya Vita katika Hali Mbaya. Wako wapi Warithi wa Waheshimiwa wa Leo?

Mtume wetu (saw) ndiye kielelezo pekee kwa maafisa wetu wa kijeshi katika kubadili wimbi la vita. Pindi idadi kubwa ya Waislamu ilipozidiwa na shambulizi la kushtukiza la adui katika Vita vya Hunain, Waislamu waliangukia chini ya shambulizi hilo katika wakati dhaifu na wakavunja muundo. Wimbi la vita lilibadilika kwa muda mfupi na kushindwa kulianza kuonekana.

Soma zaidi...

Mauaji ya Halaiki ya Kimya nchini Congo: Kimya cha Magharibi na Usaidizi kwa Jina la Faida

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni nyumbani kwa usambazaji mkubwa zaidi wa cobalt, chuma muhimu kinachotumika katika utengenezaji wa betri za lithiam-ion kwa ajili ya simu, tablets na magari ya umeme. Mnamo 2022, akiba ya cobalt ya Congo ilikadiriwa kuwa karibu tani milioni nne za metric, ambazo ziko mashariki mwa nchi, huku akiba ya kimataifa ikiwa ni tani milioni 8.3.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu