Mnamo tarehe 30 Disemba, iliripotiwa kuwa mtoto wa 6 waliganda hadi kufa mjini Gaza ndani ya wiki mbili kutokana na hali ya baridi inayovumiliwa na wakimbizi wa Kipalestina katika mahema ya muda, waliohamishwa kutoka kwa nyumba zao kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya Ukanda huo na uvamizi wa Kiyahudi. Ali al-Batran mwenye umri wa mwezi mmoja alifariki siku moja baada ya kaka yake pacha, Jumaa al-Batran, huko Deir el-Balah. Baba yao, Yahya Muhammad al-Batran, alisema kuwa Jumaa alipatikana kichwa chake kikiwa kama “donge la barafu”. Nariman, mama wa Sila Mahmoud al-Fassih mwenye umri wa siku 20, ambaye pia alifariki kutokana na kupungua kwa joto la mwili, alielezea kumkuta mtoto wake akiwa rangi ya bluu na kuuma ulimi wake huku damu ikimtoka mdomoni. Zaidi ya watu milioni 1.6 wa Gaza wamelazimishwa kuingia kwenye makaazi ya muda, wakiishi katika mahema hafifu ambayo hayatoi ulinzi kutokana na hali ya hewa ya baridi kali.