Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 530
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika mwezi wa Rajab Mtukufu mwaka huu 1446 H - 2025 M, tunakumbuka kumbukumbu mbaya ya miaka 104 ya kuvunjwa kwa Dola ya Kiislamu na wahalifu wa Waarabu na Waturuki, ambayo ilianzishwa na Bwana wa Mitume, Muhammad, rehma na amani ziwe juu yake, na Maswahaba zake watukufu na waliobarikiwa, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na kuondolewa kwa mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu katika mwaka wa 1342 H sawia na tarehe 3 Machi 1924 M mikononi mwa mhalifu Mustafa Kemal. Kutokana na hili, Hizb ut Tahrir inaandaa amali mbalimbali za umma katika nchi zote ambazo inaendesha shughuli zake za kuwahamasisha Waislamu kufanya kazi kwa bidii ili kusimamisha Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.
Katika kumbukumbu ya mwaka wa 104 H wa kuanguka kwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H sawia na tarehe 3 Machi 1924 M, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inafuraha kuwasilisha kwa wafuasi na wageni wa tovuti za Afisi Kuu ya Habari, silsila mpya inayoitwa: “Ummah Mmoja... Khilafah Moja” iliyotolewa na Afisi ya Habari wa Hizb ut Tahrir ya Wilayah Pakistan.
Kalima kuhusu “Kubadilisha Sarafu ya Karatasi nchini Sudan!”
Kama vile Yalivyo anza na “Ni ya Mwenyezi Mungu,” lazima Yamalizike na “Ni ya Mwenyezi Mungu”!
Enyi Waislamu kwa jumla, na watu wa Ash-Sham hasa: Kiongozi wa Hizb ut Tahrir, asiyewadanganya watu wake, anakuonyeni juu ya mikono ya mashetani wa wanadamu wanaotaka damu yenu imwagike bure, ili msifikie wema msafi na dhahiri, kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, bali hukmu iliyotungwa na mwanadamu lakini yenye jina na maana tofauti. Badala ya kuwa Umma ambao makafiri wanauchukulia kwa uzito, mumerudi kuwa wafuasi wa makafiri wakoloni na vibaraka wao, na huu ni uhalifu, Mwenyezi Mungu aepushie mbali, ambao hatima yake ni udhalilifu duniani na adhabu kali kesho Akhera.