Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Sababu za Kubuniwa Hizb ut Tahrir

Hizb ut Tahrir imebuniwa kwa kuitikia mwito wa maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):

“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu na hao ndio walio fanikiwa” [Aal-Imran:104]

Dhamira yake ni kuleta mwamko katika Umma wa Kiislamu kutokana na mporomoko mbaya uliofikia, na kuukomboa kutokana na fikra, nidhamu na sheria za kikafiri, pamoja na kutawaliwa na athari ya dola za kikafiri. Pia inalenga kurudisha serikali ya Kiislamu ya Khilafah ili kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt) kurudi tena.

Wajibu wa Kishariah wa Kuanzisha Vyama vya Kisiasa

(a) Kuanzishwa kwa Hizb ut Tahrir ni kuitikia kauli ya Mwenyezi Mungu (swt): Na uwe kutokana na nyinyi umma…Hapa Mwenyezi Mungu [swt] amewaamrisha Waislamuu kwamba wajiweke katika kikundi chenye muundo wa kichama kitakachoundwa kwa ajili ya kazi mbili: Kwanza ni kulingania katika kheri, yaani ulinganizi wa Uislamuu. Pili ni kuamrisha mema na   kukataza mabaya.   

Amri hii ya kubuni kikundi cha kichama ni ombi tu, isipokuwa kunapatikana qarina [kiunganishi cha dalili] cha kuonyesha kuwa ombi hilo ni la lazima, kwa sababu kazi ya kundi lenye muundo wa kichama kama ilivyofafanua aya kulingania Uislamu, kuamrisha mema na kukataza maovu ni faradhi kwa Waislamu kuitekeleza, kama ilivyothibitishwa na aya nyingi katika Qur’an na Hadith za Mtume (saw) zenye kuonyesha hayo. Amesema Mtume (saw): “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, mutaamrisha mema na kukataza maovu au Mwenyezi Mungu atawateremshia adhabu  itokayo kwake kisha mumuombe asikujibuni”

Hadith hii inakuwa ni kiunganishi cha dalili ya kuonyesha kuwa ombi hilo ni la lazima na amri hii ni ya wajibu. 

(b) Ama kuwa kikundi hichi ni chama cha kisiasa, hufahamika kutokana na aya iliyowataka Waislamu waunde kundi, na kuwa kazi ya kundi hili ni kulingania Uislamu, kuamrisha mema na kukataza mabaya.

Na kufanya kazi ya kuamrisha mema na kukataza maovu imekusanya pia katika kuamrisha watawala kutenda mema na kuwacha maovu, bali hiyo ni kazi muhimu zaidi katika kuamrisha mema na kukataza maovu, na huko ndio kuwahesabu watawala na kuwanasihi, na hii ni kazi ya kisiasa, vile vile ni kazi muhimu zaidi miongoni mwa kazi za kisiasa, na ndio katika       kazi inayodhihiri katika vyama vya kisiasa.

Hivyo aya imekuwa ni dalili ya uwajibu wa kusimamisha vyama vya kisiasa.

Hata hivyo, aya imefunga kuwepo kwa vyama hivyo kuwa ni vya Kiislamu, kwani kazi ya vyama hivi kama ilivyoainisha aya nayo ni kulingania Uislamu, na kuamrisha mema na kukataza maovu kwa mujibu wa Uislamu haifanywi ila na vikundi na vyama vya Kiislamu.

Chama cha Kiislamu ni kile ambacho kinasimama juu ya Aqeedah ya Kiislamu, na kujifunga na fikra, hukmu na utatuzi wa Kiislamu, na kuifanya njia yake ni ya Mtume (saw).

Kwa Hivyo, haijuzu kwa Waislamu kuwa na kikundi kilichoundwa katika msingi usiokuwa wa Kiislamu katika fikra na njia yake. Kwani Mwenyezi Mungu (swt) amewamrisha hivyo, na kwamba Uislamu ni mfumo pekee unaofaa katika  ulimwengu huu na ni mfumo wa kiulimwengu unaowafikiana na maumbile ya mwanadamu na unasimama kutatua tatizo la mwanadamu kama mwanadamu, unatatuwa mahitaji ya kimamubile kama hisia za kimaumbile (ghariza) za mwanadamu na mahitaji ya kiviungo, unazipangilia na kuziwekea nidhamu sahihi za kuzishibisha bila ya kuzinyima au kuziwacha huria, wala ghariza moja kuchupa mipaka ya ghariza nyingine, nao ni mfumo uliojitosheleza wenye kupanga mambo yote ya kimaisha.

(c) Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha Waislamu kujifunga na hukmu za Uislamu zote katika mambo yao yote ya maisha yao, sawa ikiwa ni katika mafungamano na Muumba wao kama vile hukmu za imani na ibada, au baina yao binafsi kama akhlaqi, chakula na mavazi, au hukmu za baina yao na wengine kama za maingiliano na sheria.

Mwenyezi Mungu (swt) amewawajibisha Waislamu kuutekeleza Uislamu kwa ukamilifu wake katika nyanja zote za maisha na kuhukumu kwa kutumia Uislamu, na iwe katiba yao na kanuni zao zimetokana na hukmu za kishari’ah kutokana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume Wake (saw). Mwenyezi Mungu (swt) asema:

“Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia.[Al-Maidah: 48]

“Na wahukumu baina yao kwa aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao ili wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyokuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Al-Maidah: 49]

Mwenyezi Mungu (swt) amezingatia kuwa kutohukumu kwa Uislamu ni Ukafiri. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

“Na wasio hukumu kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio makafiri” [Al-Maidah: 44]

Na mifumo ya kimaisha isiyokuwa Uislamu kama Urasilimali na Kkomunisti (unaojumuisha Ujamaa) ni mifumo fisadi, inayogongana na maumbile ya mwanadamu na zimetungwa na mwanadamu. Hakika ufisadi wao uko wazi, na aibu yake imedhihiri, nayo inagongana na Uislamu na hukmu zake.  Hivyo kujifunga kwayo na kuifuata ni haramu, na kuilingania ni haramu, na kuasisi makundi kwa msingi wake ni haramu. Hivyo basi, ni wajibu kwa Waislamuu wanapoasisi makundi yawe msingi wake uwe ni Uislamu pekee kifikra na njia, na ni haramu kwa Waislamu kuunda, kujinasibisha au kupigia debe makundi/vyama vilivyoasisiwa kwa msingi wa fikra za Urasilimali, Ukomunisti, Ujamaa, Utaifa, Uzalendo, Utabaka au Ujenzihuru, kwani ni makundi/vyama vya kikafiri na ya/vinalingania katika Ukafiri. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

“Na anayetafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri.” [Al-Imran:85]

Na aya tuliyoitaja inasema, “kulingania kheri” [Al-Imran: 104] yaani Uislamu. Na Mtume (saw) alisema: “Yeyote yule anayetenda jambo, lisilo na amri (Uislamu) yetu basi ni lenye kurudishwa” Na akasema: “Yeyote anayelingania uasabiya (ubaguzi) sio katika sisi.”

(d) Ama kuhusu kuunyanyua Ummah wa Kiislamu kutokana na mporomoko uliofikia, kuukumboa  kutoka kwa kifikra na mifumo ya kikafiri na hukmu zake, na kutokana na kutawaliwa, na pia ushawishi wa dola za kikafiri basi hukombolewa kwa kunyanyuliwa kifikra kwa njia ya kimapinduzi ya kimsingi na kijumla, na kubadilisha fahamu zilizopelekea uzorotefu, na kuweka  fikra za Uislamu na fahamu zake zilizo sahihi ili uwe muelekeo wa Ummah          maishani unaafikiana na fikra na hukmu za Uislamu.

Kilichopelekea mporomoko huu wakushtusha na usiostahiki ni udhaifu mkubwa uliotokea kwenye mabongo ya Waislamu katika ufahamu wao na utekelezaji wa Uislamu. Hali hiyo ili sababishwa na mambo kadhaa yasiyokuwa wazi kwao, ya fikra na njia ya Uislamu, tokea karne ya 2 Hijria hadi sasa. Yaliyopelekea kutokuwa wazi kwao yanatokana na vitu vingi. Vilivyojitokeza zaidi ni:

1. Kuchukuwa falsafa ya Kihindi, Kifursi na Kiyunani, na jitihada ya baadhi ya Waislamu kuoanisha falsafa hizi na Uislamu, hali ya kuwa kuna mgongano kamili baina yao. 

2. Wenye nia mbaya dhidi ya Uislamu kuingiza fikra na hukmu zisizotokana na Uislamu, ili kuukashifu na kuwaweka Waislamu mbali na Uislamu.         

3. Kuidharau lugha ya Kiarabu katika kuufahamu Uislamu na katika kuutekeleza na kuitenga na Uislamu katika karne ya 7 Hijria, pamoja na kuwa dini ya Mwenyezi Mungu haifahamiki bila lugha yake. Zaidi ya hayo, istinbat (uvuaji wa hukmu) kwa matukio mapya hutokana na njia ya Ijtihad, na hii haiwezekani bila ya lugha ya Kiarabu.   

4. Uvamizi wa kimishenari, kithaqafa kisha wa kisiasa kutoka kwa dola za Kimagharibi na  Kikafiri kutoka karne ya 17 Miladi, zikidhamiria kuwatenga Waislamu na Uislamu wao kwa lengo la kuumaliza.

(e) Majaribio kadhaa yamefanyika na harakati nyingi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu kwa lengo la kuwanyanyua Waislamu, lakini zimefeli zote na hazikuweza kuwanyanyua Waislamu, wala kuzuia kudidimia kwao kuliko kukubwa. Yaliyopelekea kufeli kwa majaribio haya na mkaundi haya yaliyobuniwa ili kuwanyanyua Waislamu kupitia Uislamu ni kutokana na sababu kadhaa:

1. Kukosekana ufahamu sahihi wa fikra ya Kiislamu kwa wale wanaosimamia kazi ya kuwanyanyua Waislamu. Kwa sababu ya kuathirika kwao na vigezo visivyokuwa wazi. Walikuwa   wanalingania Uislamu kwa sura jumla isiyokuwa na muelekeo, bila ya kufafanua fikra na hukmu zitakikanazo kwa ajili ya kuwanyanyua Waislamu, kutatua matatizo yao kwa huo Uislamu na kuutekeleza. Hili lilisababishwa na kutokuwa wazi fikra na hukmu hizi katika mabongo yao. Na wakafanya hali halisi ndio msingi wa kufikiri kwao, wakizalisha fikra zao. Wakautafsiri na kuufafanua Uislamu ili uafikiane na hali halisi bila ya kuwa na dalili ya kisheria, hatakama Uislamu na hali haisi vinapingana. Hawakuifanya hali halisi ni sehemu ya kufikiriwa ili kubadilishwa kwa mujibu wa Uislamu na hukmu zake. Kinyume chake wakalingania uhuru na Demokrasia, nidhamu za Urasilmali na Ujamaa, wakifahamu kuwa zinatokana na Uislamu, hali ya kuwa zinagongana nao moja kwa moja.

2. Kukosa njia sahihi na ya uwazi ya kutekeleza fikra za Kiislamu na hukmu zake utekelezaji uliotimia. Wakachukuwa fikra ya Kiislamu kwa njia ya mchanganyiko na kwa sura iliyogubikwa na ukakasi. Wakaona ya kuwa ulinganizi wa Kiislamu huwa kwa kujenga misikiti au kuchapisha vitabu, na wakaona kuundwa kwa jumuiya za kikhairati na kusaidiana, au kwa malezi ya kiakhlaq na kumtengeneza mtu mmoja mmoja, wakighafilika na ufisidifu wa jamii na kupuuzia fikra za Ukafiri, hukmu na nidhamu zake zilizo juu yao. Wakiona kuwa jamii hutengenea kwa kutengenea mtu mmoja mmoja, hali ya kuwa jamii hutengenea kwa kutengeneza fikra, hisia na nidhamu, na kutengenea kwa jamii ndio kutengenea mtu binafsi.

Kwani jamii si mtu mmoja mmoja tu, bali ni mtu mmoja mmoja na mafungamano, yaani mtu mmoja mmoja, fikra, hisia na nidhamu. Namna hivi ndivyo alivyofanya Mtume (saw), kuibadilisha jamii ya kijahiliya na kuifanya kuwa jamii ya Kiislamu, kwa kubadilisha aqeedah zilizokuwepo kwa kuweka fikra za aqeedah ya Kiislamu, na pia kwa kubadilisha fikra na fahamu na mila za kijahiliya kwa kuweka fikra za Kiislamu na fahamu na hukmu zake, na hivyo kubadilisha hisia za watu zilizojifunga kwa itikadi za kijahilia na fikra na ada zake, kuelekea katika kujifunga na aqeedah na fikra za Kiislamu na hukmu zake.  Hadi pale Mwenyezi Mungu alipomuwezesha kuubadilisha mujtama wa Madina, baada ya kupatikana kwa walio wengi ndani ya Madina walioamini aqeedah ya Kiislamu na kuchukuwa fikra za Kiislamu na fahamu za Kiislamu na hukmu zake. Hapo Mtume (saw) akahama yeye na Maswahaba wake baada ya kufanyika kiapo cha utiifu cha pili cha Aqaba, na akawa anatekeleza juu yao hukmu za Uislamu, na hivyo ndivyo ulivyopatikana mujtama wa Kiislamu ndani ya Madina.

Harakati nyingine zilibeba fikra ya Kiislamu kwa kutumia nguvu na kubeba silaha, bila ya kutofautisha baina ya Dar al-Islam (nchi ya Kiislamu) na Dar al-Kufr (nchi ya Kikafiri), na namna ya ubebaji da’wah, na kukanya maovu kwa kila mojawapo kati ya hali hizo mbili. Nchi ambazo sisi tunaishi hivi sasa ni Dar al-Kufr kwa sababu ndani yake sheria zinazotekelezwa ni za kikafiri, kwa mtazamo huu basi mujtama unafanana na wa Makkah wakati Mtume (saw) alipopewa utume na Mwenyezi Mungu (swt).  Hivyo basi, inakuwa ubebaji wa ulinganizi ndani ya hali hii ni kwa njia ya da’wah na matendo ya kisiasa na sio kwa utumiaji nguvu kama alivyobeba Mtume (saw) da’wah ndani ya Makkah, alijifunga na ubebaji wa da’wah tu bila ya kutumia amali za kinguvu.  Kwani lengo sio kumbadilisha mtawala anaye hukumu kwa Ukafiri ndani ya Dar al-Islam, bali lengo ni kuibadilisha Dar al-Kufr yote pamoja na nidhamu na fikra zake. Na mabadiliko hutumia kwa kubadilisha fikra, hisia na nidhamu zilizomo ndani yake kama alivyofanya Mtume (saw) akiwa Makkah.

Lau ingelikuwa ni Dar al-Islam, ambamo inahukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu; pindi ikiwa kiongozi anapohukumu kwa Ukafiri wa wazi, basi Waislamuu ni wajibu kumuonya juu ya hilo na kumuhesabu ili arejee katika hukmu ya Uislamu. Ikiwa hatojirekebisha ni wajibu kumnyanyulia silaha kumlazimisha ili arejee kwenye kuhukumu kwa Uislamu. Kama ilivyopokewa kwenye Hadith kutoka kwa Ubada ibn Samit:…na wala tusizozane na watawala mpaka wakifanya ukafiri wa wazi ambao mna dalili kutoka kwa Mwenyezi Mungu.”  Na imefafanuliwa katika Hadith kutoka kwa ‘Auf ibn Malik aliyoipokea   kutoka kwa kitabu cha Imamu Muslim kwamba Maswahaba walimuuliza Mtume (saw), “Je tuwakabili (watawala) kwa upanga?  Mtume (saw) akajibu, “La, kwa kuwa wanasimamisha swalah miongoni mwenu.” Kusimamisha swala ni kiashirio cha kuhukumu kwa Uislamu. Na Hadith mbili hizi zinaonyesha namna ya kumuhesabu mtawala ndani ya Dar al-Islam         na kubainisha namna ya kumuhesabu, na wakati gani wa utumiaji wa nguvu dhidi yake kuzuia kuzuka kwa ukafiri wa wazi ndani ya Dar al-Islam baada ya kutokuwepo awali.

(f) Ama hitajio la kufanya kazi ya kurejesha Khilafah, na kuhukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewawajibisha Waislamu kujifunga na hukmu zote za kisheri’ah na akawawajibisha kuhukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu. Na hayapatikani hayo ila kwa kuwepo Dola ya Kiislamu, na Khalifah anaye hukumu watu kwa Uislamu.

Tangu kuangushwa kwa Khilafah baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, w Waislamu wanaishi bila ya Dola ya Kiislamu na bila ya hukmu za Kiislamu, hivyo imekuwa suala la kurejesha Khilafah na kurejesha hukmu alizoteremsha Mwenyezi Mungu, ni faradhi ya wazi kabisa inayowajibisha Uislamu, nao ni wajibu usioepukika, hauna khiyari ndani yake na hakuna kufanyiwa wepesi jambo lake. Kupuuza katika kuisimamisha Khilafah ni katika madhambi makubwa ambayo Mwenyezi Mungu humuadhibu kwayo mja adhabu kali. Mtume (saw) alisema, “Yeyote anayekufa na hana bay’ah (ahadi ya utiifu kwa Khalifah) katika shingo yake anakufa kifo cha kijahiliya.”

Na kufeli kuchangamkia faradhi hii ni kushindwa kusimamisha miongoni mwa faradhi muhimu zaidi za Uislamu, kwani husimama utekelezaji wa hukmu za Uislamu, bali hupelekea kusimama kwa uwepo wa Uislamu katika maisha. Na, (Qaida inasema): ‘Kile ambacho wajibu hautimii ila kwacho basi nacho ni wajibu.’

Kwa ajili hiyo Hizb ut Tahrir imeasisiwa na imesimamisha muundo wake juu ya aqeedah ya Kiislamu. Imejifunga na fikra na hukmu za Kiislamu zinazohitajika kwa ajili ya kulifikia lengo lake. Imejiepusha na mapungufu yote na sababu zilizopelekea kufeli kwa harakati zilizoundwa kuhuisha Waislamu kupitia Uislamu. Chama kimetambua fikra na njia kwa umakini wa kifikra wa kindani kutoka kwa Qur’an. Sunnah, Ijma’ Sahabah na Qiyas. Kimeifanya hali halisi ni nukta yake ya kufikiri ili kuibadilisha kwa mujibu wa hukmu za Uislamu. Kimejilazimisha na njia ya Mtume (saw) katika kazi yake ya kuibeba da’wah ndani ya Makkah, mpaka akasimamisha Dola ndani ya Madinah. Chama kimeifanya aqeedah, fikra zake na sheria zake kuwa sehemu ya kuwaunganisha wanachama pamoja.

Hivyo imekuwa ni jambo ambalo Ummah unastahili kukikumbatia na kwenda pamoja nacho, bali ni wajibu kwao kukipokea na kusonga pamoja nacho, kwa sababu ni chama pekee chenye kuifahamu kindani fikra yake, chenye uoni wa njia yake, chenye kufahamu kadhia     yake, chenye kujifunga katika kufuata seerah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) bila kuipindisha na bila kuruhusu chochote cha kushawishi kikazuia kufikia lengo lake.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 25 Februari 2020 12:36
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Hizb ut Tahrir Lengo la Hizb ut Tahrir »

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu