Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Bila Mfumo wa Elimu ya Kiislamu, Haramu inakuwa ni Sharti la Kusoma

Mnamo tarehe 16 Novemba, gazeti la Times la India liliripoti kwamba Chuo Kikuu cha Uttarakhand Sanskrit huko Haridwar kimeanzisha hatua za kutekeleza uamuzi wa Mahakama ya Upeo juu ya mavazi ya wanafunzi ndani ya chuo kikuu na madarasani, Makamu wa Chansela wa Chuo Kikuu Dinesh Chandra Shastri aliiambia TOI mnamo Alhamisi. Hatua hiyo imekuja baada ya malalamiko kuwa “wanafunzi kadhaa wa Kiislamu wa kike wanaendelea kuvaa burka au hijabu wakiwa chuo hicho kikuu.”

Soma zaidi...

Amani ya Kudumu Inaweza Tu Kupatikana huko Balochistan kupitia Kuung'oa Mfumo wa Wakoloni na Kusimamisha Khilafah Rashida

Machafuko katika jimbo la Balochistan si jambo geni. Yamedumu tangu uhuru wa Pakistan kutoka kwa Raj wa Uingereza. Watu wa Balochistan wana malalamiko ya kina, yaliyoachwa bila kutatuliwa na utawala wa kikoloni wa Uingereza na watawala ambao ni vibaraka wa wakoloni wa Magharibi. Mfumo wa wakoloni ulipangwa kuwatiisha Waislamu, badala ya kuangalia mambo yao. Unawanyima haki na unadumisha udhibiti kupitia nguvu za kijeshi.

Soma zaidi...

Msimamo Unaokinzana wa Indonesia juu ya umbile la Kiyahudi: Maneno Makali Lakini Ingali Inadumisha Mahusiano Mazuri

Indonesia imeyataka mataifa ya Kiislamu na Kiarabu kukata uhusiano wa kibiashara na kiuchumi na ‘Israel’ ili kukomesha ghasia mjini Gaza. Katika kikao cha Riyadh cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na OIC, Makamu wa Waziri wa Mambo ya Nje Anis Matta alisisitiza ulazima wa kukata vitega uchumi vinavyohusiana na taasisi za Kizayuni na kuimarisha biashara ndani ya uchumi wa nchi za Kiislamu. Licha ya wito huu, biashara ya Indonesia na ‘Israel’ ilifikia dolari milioni 173 kuanzia Januari hadi Septemba 2024, ongezeko la 24.6% kutoka mwaka uliopita.

Soma zaidi...

Mtazamo kwa Ghasia za Baada ya Uchaguzi wa Msumbiji

Kwa mujibu wa Kituo cha Demokrasia na Haki za Binadamu cha Msumbiji na shirika la Reuters, kufikia tarehe 8/11/2024, jumla ya vifo 34 viliripotiwa huku vyanzo vyengine vikisema kuwa waliouawa ni zaidi ya 50, kutokana na ghasia za baada ya uchaguzi. kutangazwa kwa mgombea wa chama tawala cha Front for Liberation of Msumbiji (Frelimo), Daniel Chapo kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika mnamo Oktoba 24 mwaka huu ambapo wapinzani walidai kuwa matokeo ya kura yaliibwa.

Soma zaidi...

Mvunjifu na Mdhamini Pamoja: Serikali Yalenga Nini?

Iwe ni serikali au upinzani, miundo kama hii ya kisiasa haiwezi kukwepa kuwa wafungwa wa ukoloni, kama vile mtazamo wao wakati wa Mapinduzi ya Kiarabu na Kimbunga cha Al-Aqsa kinachoendelea, wanatumikia maslahi ya makafiri wakoloni ili tu kudumisha viti vyao. Madhumuni yao pekee ni kuzuia ummah wa Kiislamu kuelekea katika Khilafah na kujaribu kuzalisha miungano bandia, dhidi ya umoja halisi wa Khilafah.

Soma zaidi...

Mirziyoyev Afufua “orodha nyeusi” za Waislamu

Mwanablogu mashuhuri wa Uzbekistan, Mirrahmat Muminov, alitangaza kwamba ana habari kuhusu kuanzishwa kwa udhibiti kamili na ufuatiliaji wa waumini sugu wa misikiti nchini. Aliripoti haya kwenye ukurasa wake wa Facebook: Kamati ya Masuala ya Kidini na Bodi ya Waislamu ya Uzbekistan, pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani, waliagizwa kuandaa orodha za waumini sugu wa kudumu wa misikiti. Uamuzi huu unahusiana na kukua kwa itikadi kali za kidini na umaarufu wa fikra za kidini miongoni mwa vijana.

Soma zaidi...

Kuchaguliwa tena kwa Trump: Mporomoko wa Demokrasia uso Kifani

Mnamo Novemba 6, 2024, ilithibitishwa kuwa Donald Trump, mhalifu aliyepatikana na hatia, alishinda tena uchaguzi wa rais nchini Marekani. Tukio hili sio tu suala la mtu wa kuchukiza, bali ni dalili ya uozo wa kina katika mfumo wa kidemokrasia wa Magharibi. Huku ulimwengu ukitazama, kuchaguliwa tena kwa Trump kunafichua udanganyifu mwingi ambao demokrasia ya Magharibi imeunadi kwa ulimwengu kwa miaka mingi.

Soma zaidi...

Maldives Yatumbukia Zaidi ndani ya Mgogoro wa Kifedha, huku Ikiyumba Kati ya China na India

Suluhisho la migogoro ya kiuchumi ya Maldives haliko katika kuyumba kati ya dola mbili zinazopiga vita Waislamu na Uislamu. Mfumo wa sasa wa ulimwengu unaleta madhara kwa Waislamu, kiuchumi na kijeshi. Unafanya dola za Waislamu kuwa uwanja wa kunyonywa na wakoloni, na washirika wao, India na umbile ya Kiyahudi. Suluhisho kwa Maldives ni kuwa sehemu ya Khilafah tukufu, kama ilivyokuwa huko nyuma.

Soma zaidi...

Wale Waliotazama Moto wa Gaza Wamehukumiwa Udhalilifu!

Ikiwa Bw. Erdogan angekuwa mkweli, angejibu uwepo huu wa kigaidi kwa nguvu za kijeshi, mateso haya yasingetokea Gaza. Ikiwa kweli wewe ni mkweli, hutanyamaza tena kuhusu mauaji yanayofanywa na magenge ya Kiyahudi huko Gaza na Lebanon, bali utahamasisha jeshi. Kwa hivyo, kanda na jiografia iliyo chini ya moto itakomesha ukatili huu, na utafanya kile kinachohitajika hata ikiwa kimechelewa.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu