Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Marekani, kupitia Usitishaji vita, Inafikia Malengo Mawili Muhimu kwa Uvamizi wa Kiyahudi:
Kuondolewa kwa Vikosi vya Hezbollah vinavyoungwa mkono na Iran Kaskazini mwa Mto Litani, na Kutenganishwa kwa Pande Mbili!

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 27 Novemba 2024, usitishaji vita ulitangazwa katika upande wa Lebanon kati ya umbile la Kiyahudi na Hezbollah. Moja ya masharti yake ilikuwa kwamba umbile la Kiyahudi lingeondoa jeshi lake linalovamia kutoka kusini mwa Lebanon ndani ya miezi miwili, huku Hezbollah ingerudisha nyuma majeshi yake kaskazini mwa Mto Litani. Makubaliano hayo pia yalivipa vikosi vya Kiyahudi uhuru wa kutembea kusini endapo chama hicho kitakiuka makubaliano hayo, sambamba na kuendelea na safari za ndege za adui katika anga ya Lebanon kwa ajili ya uchunguzi na ujasusi.

[Maelezo ya makubaliano ya kusitisha mapigano, kama yalivyochapishwa na Al Jazeera mnamo tarehe 27 Novemba 2024, yalijumuisha:

Kujiondoa kwa wanajeshi: Jeshi la ‘Israel’ litaondoka polepole kutoka kusini mwa Lebanon, na kukamilisha kujiondoa ndani ya siku 60. Hezbollah itaondoka kaskazini mwa Mto Litani, takriban kilomita 30 kaskazini mwa mpaka na ‘Israel’. Jeshi la Lebanon litapeleka karibu wanajeshi 5,000 kusini mwa Mto Litani, na kuweka nafasi 33 kwenye mpaka wa ‘Israel’.

Utaratibu wa ufuatiliaji: Utaratibu uliopo wa ufuatiliaji wa pande tatu unaohusisha Kikosi cha Muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL), jeshi la Lebanon, na jeshi la ‘Israel’ utasimamia utekelezaji wa makubaliano hayo. Utapanuliwa ili kujumuisha Marekani na Ufaransa, huku Washington ikiongoza kundi hilo.]

Licha ya makubaliano haya, umbile la Kiyahudi liliwakamata watu wanne walioregea katika vijiji vyao, wakiwashuku kuwa wapiganaji wa upinzani. Pia liliweka amri ya kutotoka nje kusini mwa Mto Litani kana kwamba eneo hilo lilikuwa chini ya udhibiti wake. Al Sharq Al Awsat iliripoti mnamo tarehe 27 Novemba 2024:

[Jeshi la ‘Israel’ limetangaza leo (Jumatano) amri ya kutotoka nje kwa wakaazi wa kusini mwa Lebanon kuelekea kusini mwa Mto Litani...

Msemaji wa jeshi la ‘Israel’ kwa lugha ya Kiarabu, Avichay Adraee, alisema leo (Jumatano):

‘Matembezi yoyote kuelekea maeneo haya yanakuwekeni kwenye hatari. Tunakufahamisheni kwamba kuanzia saa 5:00 jioni ya leo hadi saa 7:00 asubuhi kesho, matembezi yoyote kusini mwa Mto Litani ni marufuku kabisa.’]

Al Arabiya Net ilichapisha maelezo ya makubaliano hayo mnamo tarehe 27 Novemba 2024, ikisema:

[Uhuru wa kutembea: ‘Israel’ inahifadhi haki ya kuchukua hatua katika eneo la kusini dhidi ya ukiukaji. Nje ya eneo hili, inashikilia haki ya kujibu vitisho vinavyoendelea, ikiwa ni pamoja na ulanguzi wa silaha haramu hadi Lebanon. Katika hali kama hizi, ‘Israel’ itaiarifu Marekani kila inapowezekana. Safari za ndege za ‘Israel’ juu ya anga ya Lebanon zitazingatia ujasusi, uchunguzi, na upelelezi, kupunguza mwonekano na kuepuka kuvunja kizuizi cha sauti.]

Makubaliano haya yanatenganisha kikamilifu pande za Lebanon na Gaza, na kuiacha Gaza ikiwa imetengwa chini ya mashambulizi ya Kiyahudi bila kunusuriwa na upande wa Lebanon.

Wakati huo huo, Amerika, Mayahudi, na tawala za kisaliti zinazozunguka Palestina zinapanga makubaliano ambayo yatahakikisha ushindi kwa Mayahudi dhidi ya Gaza chini ya masharti wanayoamuru. Haya yanatokea wazi mbele ya watawala wasiomcha Mwenyezi Mungu wala hawaoni haya. [قَاتَلَهُمُ اللهُ أَنَّى يُؤْفَكُونَ [ “Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?” [Surat Al-Munafiqun: 4]

Amerika na washirika wake wanalenga kuitenga Gaza kikamilifu, na kuwapa utawala wa Kiyahudi juu yake, Ukingo wa Magharibi, Jerusalem, na Palestina yote. Makubaliano ya kutenganisha pande na kuondoa vikosi vya Hezbollah kaskazini mwa Litani yaliwezeshwa na ushirikiano wa kimya wa watawala wa Waislamu, hasa wale walio karibu na Palestina, kama vile Misri, Jordan, Saudi Arabia, Uturuki, Iran, Syria na Iraq. Watawala hawa wanajifanya kama wasioegemea upande wowote kati ya Mayahudi na Waislamu, lakini kwa uhalisia, wanaegemea upande wa umbile la Kiyahudi.

Hata Iran haikupeleka jeshi lake kunusuru chama chake nchini Lebanon, ili kisifungwe na makubaliano ya kujiondoa kwenye nyadhifa zake na kusitisha kunusuru kwake Gaza. Kadhalika, tawala za Misri na Jordan, ambazo kijiografia ziko karibu zaidi na Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, hazikukusanya majeshi yao kutetea maeneo haya. Badala yake, walikutana jijini Cairo ili kujadili mazungumzo na Mayahudi kuhusu ardhi ya Wapalestina, badala ya kupeleka majeshi yao kung'oa mwiba uliopandwa na wakoloni katika Ardhi Iliyobarikiwa.

Kama ilivyoripotiwa na “Youm7” kwenye tovuti yake mnamo tarehe 27/11/2024:

‘Rais Sisi na Mfalme wa Jordan wanajadili juhudi za kuratibu misimamo kuhusu maendeleo katika maeneo ya Wapalestina...’

bila ya kutaja hata neno moja kuhusu kuhamasisha majeshi kuihami Palestina dhidi ya jinai za kikatili za Wazayuni, ambao uvamizi wao umewalenga watu, miti na mawe sawia!”

Enyi Waislamu: Tunafahamu kikamilifu kwamba umbile la Kiyahudi halina uwezo wa kupigana vita, kwani udhalilifu na fedheha zimetupwa juu yao.

[وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ * ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلَّا بِحَبْلٍ مِنَ اللهِ وَحَبْلٍ مِنَ النَّاسِ]

Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa. Wamepigwa na udhalili popote wanapo kutikana, isipo kuwa wakishika kamba ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu.”[Surat Aal-i-Imran:111,112]

Uoga umewekwa katika nyoyo zao, na hawawezi kusimama kidete isipokuwa kwa kamba kutoka kwa Mwenyezi Mungu au kutoka kwa watu. Uhusiano wao na Mwenyezi Mungu umekatika tangu zama za mitume wao, na kuwaacha wakitegemea tu msaada wa wengine. Kamba yao sasa inashikiliwa na kiongozi wa ukafiri, Marekani, pamoja na usaliti wa watawala katika ardhi za Waislamu. Bila msaada huu, umbile la Kiyahudi ni dhaifu kuliko utandu wa buibui.

Ukweli unajieleza wenyewe: kwa zaidi ya siku 400, hawajaweza kufikia malengo yao, hata dhidi ya vikundi ambavyo vinakosa ndege na magari ya kivita.

Vile vile tunaelewa kwamba kuondolewa kwa umbile la Kiyahudi na kung'olewa kwa misingi yake hakuwezi kupatikana kwa juhudi za makundi peke yake. Njia pekee ya kulifanikisha hili ni kwa kuyakusanya majeshi, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu Anavyosema:

[فَإِمَّا تَثْقَفَنَّهُمْ فِي الْحَرْبِ فَشَرِّدْ بِهِمْ مَنْ خَلْفَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ]

Basi ukiwakuta vitani wakimbize walio nyuma yao ili wapate kukumbuka.” [Surat Al-Anfal:57]

Wakoloni wanalifahamu hili kikamilifu, ndiyo maana wanatoa amri kali na madhubuti kwa watawala katika ardhi za Waislamu kuwafungia majeshi kwenye kambi zao. Mnawaona wajumbe wa wakoloni, hasa kutoka Amerika, wakisafiri katika eneo hilo, kutoka Qatar hadi Misri, Jordan, Saudi Arabia, Uturuki na kwengineko, ili kuhakikisha kwamba watawala vibaraka wao wanafuata amri hizi, kuhakikisha majeshi yanabaki bila kusonga katika maeneo yao.

Enyi Waislamu, enyi askari katika majeshi ya Uislamu:

Msiba wa Ummah huu uko kwa watawala wake. Wanashuhudia miili ya mashahidi kwa macho yao wenyewe, wanasikia vilio vya watoto kwa masikio yao, na wanaona familia zilizohamishwa kutoka kwa nyumba zao, wakiwa wamebeba watoto wao na wanawake katika matukio ya kuumiza nyoyo. Watawala wameyaona haya yote na yamefikia akili zao, lakini hayakugusa uungwana wa mtu kama Al-Muutasim!

Hata wanapolizunguka umbile la Kiyahudi mithili ya bangili inavyozunguka kifundo cha mkono, wanashindwa kupeleka jeshi au kuitikia vilio vya kuomba msaada. Wamejishusha thamani, kwani majeraha hayawaumizi waliokufa.

Enyi askari katika majeshi ya Uislamu:

Bila shaka mnafahamu kwamba Palestina ni ardhi iliyobarikiwa, ardhi ya Kiislamu ambayo Mayahudi hawana mamlaka halali ndani yake. Lile linaloitwa kama “suluhisho la dola mbili” halina nafasi ndani yake. Kama vile Umar ibn al-Khattab alivyoifungua, Al-Khulafa’ Alrashideen (Makhalifa Waongofu) waliihifadhi, Salahuddin akaikomboa, na Sultan Abdul Hamid akailinda kutokana na Mayahudi; itaregeshwa tena kwa juhudi za askari waaminifu wa Mwenyezi Mungu, wakiongozwa na kiongozi wao chini ya Raya ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt). Watatimiza maneno ya Mtume (swt): «لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ...» “Kwa yakini mtapigana na Mayahudi na kwa yakini mtawaua.” [Imepokewa na Muslim kutoka kwa Ibn Umar]

Enyi askari katika majeshi ya Uislamu:

Je, hamutamani moja kati ya matokeo mawili matukufu?

[يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ * وَأُخْرَى تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِنَ اللهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ]

Atakusameheni dhambi zenu, na atakutieni katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani nzuri nzuri katika Bustani za milele. Huko ndio kufuzu kukubwa. Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini![Surat As-Saff:12,13]

Basi inukeni, enyi askari katika majeshi ya Uislamu, kuinusuru Ardhi Iliyobarikiwa, ili iweze kung'aa tena kama nyumba ya Uislamu. Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwausuru wanaoinusuru njia yake.

[وَلَيَنْصُرَنَّ اللهُ مَنْ يَنْصُرُهُ إِنَّ اللهَ لَقَوِيٌّ عَزِيز]

“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.” [Surat Al-Hajj:40]

H. 27 Jumada I 1446
M. : Ijumaa, 29 Novemba 2024

Hizb-ut-Tahrir
 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu