Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mkasa wa Mashua za Wahamiaji kati ya Njama na Ufisadi wa Mamlaka

(Imetafsiriwa)

Neema mbili ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwakumbusha nazo watu wa Makka baada ya kuupa mgogo ulinganizi wa Uislamu.

(الَّذِي أَطْعَمَهُم مِّن جُوعٍ وَآمَنَهُم مِّنْ خَوْفٍ)

“Ambaye anawalisha wasipate njaa, na anawalinda na khofu.” [Quraysh:4]; chakula na usalama, na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie, amesema katika yale aliyoyasimulia Al-Tirmidhi kutoka kwa Ubayd Allah bin Muhsin, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«مَنْ أَصْبَحَ مِنْكُمْ آمِناً فِي سِرْبِهِ، مُعَافًى فِي جَسَدِهِ، عِنْدَهُ قُوتُ يَوْمِهِ، فَكَأَنَّما حِيزَتْ لَهُ الدُّنْيَا»

“Yeyote miongoni mwenu anayepambaukiwa akiwa na amani katika boma lake, mwenye afya mwilini mwake, akiwa na chakula cha siku yake, ni kama aliyemilikishwa dunia nzima.”

Mwishoni mwa mwaka wa 2019, hali ya kuporomoka polepole ilianza nchini Lebanon, ambayo watu walipoteza au walikaribia kupoteza maisha yao, na mapato ya watu yakawa rundo la karatasi, na yakiwalisha kwa uchache, mapato ya kila mwezi ya mfanyikazi yakawa kati ya chini zaidi dunia, sawa na dolari moja kwa siku.

Halafu, hivi majuzi, kupotea kwa usalama miongoni mwa watu kuliongezea hilo, ni vigumu siku kupita bila ya kusikia kesi za mauaji hapa, wizi na uvamizi kule, na matumizi ya silaha za aina mbalimbali miongoni mwa watu kwa sababu zisizo na maana katika shida yoyote ya muda mfupi. Lebanon ilirekodi kiwango cha juu cha watu kumiliki silaha za kibinafsi, kwa kile kilichojulikana kama usalama wa kibinafsi! Kulingana na tovuti ya Uswizi iliyobobea katika kufuatilia na kupambana na kuenea kwa silaha za kibinafsi kote duniani: "Lebanon ina silaha milioni 1.927 kwa wakaazi wapatao milioni 6, ambapo ina maanisha kuwa inashikilia nafasi ya pili katika ulimwengu wa Kiarabu baada ya Yemen, na ya tisa duniani, katika idadi ya silaha ikilinganishwa na idadi ya watu, na inashinda Iraq, ambayo imezama katika utovu wa usalama na machafuko ya kisiasa kwa karibu miaka 20!

Kutokea kwa mambo haya mawili nchini Lebanon, njaa na ukosefu wa usalama, kumeendeleza hali ya kusikitisha kwa miezi kadhaa, ambayo ni jaribio la watu kuondoka nchini kupitia njia zisizo salama, haswa kwa kupitia baharini ili kujaribu kufikia fuo za nchi za Ulaya, ambapo jaribio la mwisho liliwaacha karibu wahasiriwa mia moja.

Mashua hizi, zisizofaa kwa ajili ya safari kama hizo, zinaondoka fuo za Lebanon zikiwa zimesheheni watu waliouza mali zao na kila kitu walichokuwa nacho, na kubeba wanyonge miongoni mwa wanawake na watoto wao, hata watoto wachanga miongoni mwao, kutoka kwa watu wa Lebanon, Palestina na Syria, kama abiria. Kisha boti hizi huzama kwenye bahari ya wazi, katika matukio ya kuatua moyo yenye mayowe ya watoto, wanawake na wanaume, na mandhari ya mtu kutupa mwili wa mwanawe kabla haujaoza baada ya kifo chake katika hali ya kiu na njaa na kunywa maji ya bahari, au mwili wa mtoto mchanga unaoelea, au ambaye moyo wake ulipiga kwa kiungulia kwa sababu hakuweza kumwokoa rafiki yake ambaye hakujua kuogelea, au ambaye aliyaita mabaki ya mtoto wake akipiga akilia, Ee Mwenyezi Mungu.

Ni nani anayehusika na haya yanayotokea leo katika suala la njaa na ukosefu wa usalama?! Je, ni sahihi kuyaweka haya juu ya mabega ya watu?!

Sisi, katika Hizb ut Tahrir Wilaya ya Lebanon, tunapaza sauti zetu juu kwa kuyawajibisha kikamilifu mamlaka ya Lebanon na vyombo vyake kwa hali hiyo, kutokana na kukosekana kwa dola na vyombo vyake, ambayo ni wazi na kimsingi imesababishwa na ufisadi uliokithiri katika tabaka tawala la kisiasa kwanza, na pili, ukosefu wa maendeleo ya kweli katika suluhu zozote zinazopatikana.

Mamlaka na vyombo vyake vinafahamu kuhusu kuondoka kwa boti kama hizo kutoka fuo za Lebanon. Baadhi ya walanguzi hata huwapeleka wanaotafuta uhamiaji hadi fukweni kwa misafara ya wazi, na wengi wa walanguzi hawa wanajulikana sana na mamlaka. Je, ziko wapi taasisi na teknolojia mamlaka inazomiliki kufuatilia mienendo ya meli?! Na ziko wapi huduma za usalama zenye majina, sifa na vitendo vingi zinazokimbia kutoka kona moja hadi nyingine kwa utashi wa mwanasiasa na mamlaka?!

Jambo ni kwamba mamlaka hii inayauza maisha ya watu hawa kutoka Lebanon, Palestina na Syria, na kuwafanya kama kadi ya kutafuta misaada ya nchi wafadhili. Utaratibu wa nchi za Ulaya kwa wanaotafuta uhamiaji?

Jambo ni kwamba mamlaka hii inayauza maisha ya watu hawa kutoka kwa watu wa Lebanon, Palestina na Syria, na kuwafanya kama kadi ya kutafuta msaada wa nchi wafadhili. Vyenginevyo, kauli ya Waziri wa Mazingira katika Mamlaka ya Lebanon, Nasser Yassin, kwenye Idhaa ya Al-Jazeera mnamo tarehe 24/09/2022 ina maanisha nini kwamba suluhisho ni kufungua mlango wa uhamiaji wa mara kwa mara wa nchi za Ulaya kwa wanaotafuta uhamiaji? Je, Waziri wa Masuala ya Kijamii, Hector Al-Hajjar, anaiambia nini mamlaka ya Lebanon, katika taarifa ya habari kwa Al-Jazeera siku hiyo hiyo, kwamba waliionya jumuiya ya kimataifa juu ya Lebanon kutokuwa na uwezo wa kubeba idadi kubwa ya wakimbizi wa Syria?! Hii ni pamoja na kauli za Waziri Mkuu mteule Najib Mikati kuhusu wakimbizi, na kauli za Baba wa Taifa za kutokea kwa vita kwa sababu ya kuwepo wakimbizi!

Kauli hizi za juu kuhusu wajibu wa serikali na mamlaka wa utunzaji, na upuuzaji wa mamlaka na vyombo vyake wa uchungu wa walanguzi hawa wa watu, ina maana moja pekee: Enyi nchi wafadhili, ima mtulipe pesa, au tutayatupa maisha ya wakimbizi hawa usoni mwenu!

Kwa mukhtasari, hakuna chakula na usalama nchini Lebanon, huku kikundi kidogo cha watu wake kikichanganya nguvu na pesa, ambazo kina baba wanawarithisha watoto! Matajiri hawa wababe wa madaraka hukusanya vilabu vyao na pesa zao, huku wakiwashughulisha watu kuhangaika kutafuta chakula chao, na hata kuhangaika huku ni kwa mujibu wa madhehebu yao! Wanauana wao kwa wao, na kujiweka hatarini ili kuondoka nchini kwa sababu ya utovu wa uslama na kukata tamaa na mamlaka na vyombo vyake.

Ama nyinyi, watu wetu, hatusemi kuwa mnahusika na hali hii mbaya, kwani nyinyi ndio mnaohisi moto wake, bali tunasema, tukiwakumbusha:

Kinachotutokea sisi na nyinyi ni mabadiliko dhidi ya hawa wafisadi, na sio kuendelea na kimya cha kukubali matukio ya kifo cha kila siku mitaani na baharini, na hata kujiua; Ni juu ya kila mheshimiwa kwa jumla nchini Lebanon kupitia mchakato wa mabadiliko na kukataa tabaka hili fisadi la kisiasa.

Hapa, tunawakumbusha wananchi kuhusu wale waliowachagua muda si mrefu kuwawakilisha bungeni, hivi matokeo yalikuwaje?! Wamekuwa manaibu, na masuala yakaongezeka pamoja nao! Na hii hapa miji yenu, bali miji mikuu ya pwani ya Mediterania na Ash-Sham, Tiro, Sidon, Beirut na Tripoli, ambayo wawakilishi hawa na wale waliowachagua kuwawakilisha wanadai kuzama ndani ya giza na kiu, kuzama ndani ya umaskini, na kuzamisha watoto wao baharini! Hivi ziko wapi ahadi za jana za mabadiliko ndani ya mfumo?!

Hawana masuluhisho isipokuwa kutoka kwa aina ile ile ya mfumo! Mfumo fisadi unaobeba adhabu ndani yake, na ni bure kabisa kujaribu suluhisho kupitia mfumo huo, jambo ambalo Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Lebanon ilionya juu yake katika machapisho yake ya maandishi na ya video wakati wa uchaguzi wa Mei 2022, ambayo ilitoa wakati huo ikionya dhidi ya kushiriki katika mchakato wa uchaguzi, ikiwemo chapisho lenye kichwa "Hairuhusiwi kugombea au kupiga kura katika uchaguzi wa ubunge..." na jengine lenye kichwa "Katika milango ya uchaguzi na utoaji wito wa kuzidisha ushiriki katika dhambi zao".

Na sisi hawa hapa tena, tunawahutubia watu wote wa Lebanon, ndio, watu wote wa Lebanon, sio tu Waislamu pekee, kwa usemi wa kweli, ambao lazima ueleweke, kukubalika na kufanyiwa kazi na kila mtu huru, mwenye akili timamu na mwenye uwezo.

Aidha, ni wajibu kwa Muislamu mwenye uwezo, kama kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika yale aliyoyasimulia Al-Tirmidhi kutoka kwa Hudhaifah, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«والَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَتَأْمُرُنَّ بالْمَعْرُوفِ، ولَتَنْهَوُنَّ عَنِ المُنْكَرِ، أَوْ لَيُوشِكَنَّ اللَّه أَنْ يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عِقَاباً مِنْهُ، ثُمَّ تَدْعُونَهُ فَلا يُسْتَجابُ لَكُمْ»

“Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake! Hamtaacha kuamrisha mema na hamtaacha kukataza maovu, isipokuwa Mwenyezi Mungu atakaribia kuteremsha adhabu juu yenu kutoka kwake, kisha mutamuomba wala hamtajibiwa.” Na amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kama ilivyopokelewa na Abu Dawud na Al-Tirmidhi kwa kutoka kwa Ibn Masoud Mwenyezi Mungu amuwiye radhi:

«واللَّه لَتَأْمُرُنَّ بِالْمَعْرُوفِ، وَلَتَنْهَوُنَّ عَنِ الْمُنْكَرِ، ولتَأْخُذُنَّ عَلَى يَدِ الظَّالِمِ، ولَتَأْطرُنَّهُ عَلَى الْحَقِّ أَطْراً، ولَتَقْصُرُنَّهُ عَلَى الْحَقِّ قَصْراً، أَوْ لَيَضْرِبَنَّ اللَّه بقُلُوبِ بَعْضِكُمْ عَلَى بَعْضٍ، ثُمَّ ليَلْعَنكُمْ كَمَا لَعَنَهُمْ - أي بني إسرائيل»

“Naapa kwa Mwenyezi Mungu, hataacha kuamrisha mema na hamtaacha kukataza maovu, na hamtaacha kumzuia dhalimu, na hamtaacha kumpinda katika haki, na hamtaacha kumfunga katika haki. Isipokuwa Mwenyezi Mungu atazingonganisha nyoyo zenu wenyewe kwa wenyewe, kisha atawalaani kama alivyo walaani wao - yaani wana wa Israili”

Kuchunga mambo ni jukumu la dola na mamlaka, na kumhisabu mtawala dhalimu na fisadi ni jukumu la watu. Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika yale aliyoyasimulia Al-Nasa’i kutoka kwa Abu Bakr Al-Siddiq, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema:

«إِنَّ النَّاسَ إِذَا رَأَوا الظَّالِمَ فَلَمْ يَأْخُذُوا عَلَى يَدَيْهِ أَوْشَكَ أَنْ يَعُمَّهُمُ اللَّه بِعِقَابٍ مِنْهُ»

“Hakika watu pindi wanapomuona dhalimu (anadhulumu) na wasimzuie, Mwenyezi Mungu atakaribia kuwachanga katika adhabu itokayo kwake.”

Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon inakualikeni kufanya kazi nayo katika njia ya mabadiliko inayoifuata kwa njia iliyo wazi na iliyounganishwa ya kuunda dola. Sio dola yoyote, bali ni dola inayotakwa na Mjuzi wa yote, Mwingi wa hekima, dola inayoeleza uhalisia wa ukhalifa ardhini ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu anautaka sio tu kwa Waislamu bali kwa wanadamu, Dola ya Kiislamu; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

H. 30 Safar 1444
M. : Jumatatu, 26 Septemba 2022

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Lebanon

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu