Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

[وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal:72]
(Imetafsiriwa)

Kwa muda wa miezi saba, Gaza imeangamizwa kwa mikono ya Mayahudi chini ya macho ya watawala vibaraka na wakoloni wao wa Magharibi, haswa Marekani. Hawakuridhika na Gaza; wakaanza na Rafah, wakiibomoa juu ya vichwa vya watu wake na wale waliohamishwa huko kutoka Gaza na sekta yake. Marekani, anayeitwa mtetezi wa binadamu, anawaunga mkono kwa kusema: “Ipigeni mabomu Rafah, lakini kwanza, waondoeni watu wa kaskazini mwa Gaza na muwarudishe makwao!” Kana kwamba watu wa Rafah na nyumba zao hawatakikani na kana kwamba watu wa kaskazini bado wana nyumba za kuregea!

Katikati ya uharibifu huu na mauaji ya halaiki, bado kuna kundi thabiti huko Gaza, Rafah, na Ukingo wa Magharibi, lenye kuwatia hasara Mayahudi kwa kuwaua na kuwateka. Haya yanatokea licha ya kukabiliana na mashini ya kijeshi iliyo na teknolojia ya kisasa, huku wao - mujahidina - hawana viatu, wakipigana kwa silaha karibu za kibinafsi. Bali wamebeba nyoyoni mwao imani yenye nguvu inayotosha kusukuma milima, ikithibitisha kwa kila mtu mwenye silaha na nguvu katika Ummah huu kwamba suala sio silaha, bali ni nani anayeibeba na anaamini nini. Hili ni funzo ambalo majeshi katika ardhi za Kiislamu, hasa zile zinazoizunguka ardhi iliyobarikiwa ya Palestina nchini Misri na Jordan, zinahitaji kufahamu.

Kazi ya msingi ya watawala vibaraka na vyombo vyao vya usalama ni kuyazuia majeshi na vikosi vya Umma, yanayoonekana tu katika kukandamiza mienendo ya watu au kujaribu kunyamazisha neno la haki lililoamrishwa na Mwenyezi Mungu. Wanayaona maneno yanayochochea majeshi kuwa hatari sawa na risasi, hisia zinazoshirikiwa na tawala zote katika nchi za Kiislamu bila kujali ukubwa wao!

Mambo yote katika nchi za Kiislamu yanasimama na kuharibika, isipokuwa mikutano ya vyombo vya usalama na wizara za mambo ya ndani. Haya si kwa ajili ya kuratibu mapambano dhidi ya maadui wa umma, wale wanaoikalia kimabavu ardhi yake au kukiuka matukufu yake, bali ni kuzuia sauti au harakati zozote zinazochochea majeshi kuwaondoa madarakani watawala na kusimamisha utawala wa Kiislamu katika dola ya Kiislamu, au kuwachochea ili kuwanusuru ndugu zao wanaoshambuliwa huko Gaza, Rafah na Palestina yote. Iwapo baadhi ya askari wa jeshi watatoka kwa bidii kwa ajili ya Dini, heshima, na watu wao huko Gaza, Mayahudi na tawala hubatilisha habari hii ili kuzuia harakati hizi za dhati zisienee kwa majeshi na Umma!

Enyi Waislamu nchini Lebanon:

Tunajua kwamba nyoyo zenu zinawaka kwa hamu ya kuwanusuru watu wenu huko Gaza na Rafah. Mazungumzo yenu yamejaa mada hii, na mumefufua qunoot katika swala zenu, haswa siku za Ijumaa. Matukio ya mauaji na mauaji ya halaiki yanawatia maumivu, kama yanavyomuumiza kila Muislamu mwenye ulinzi kutoka kwa wana wa Ummah huu. Lakini munaishi, kama Waislamu wote wanavyoishi katika nchi zote za Kiislamu, chini ya mamlaka fisadi na vyombo vya usalama ambavyo havifanyi kazi kwa ajili ya usalama wenu bali kwa kukandamiza majaribio yenu ya kusonga, hata kama kutoka kwa vikundi vya wanafunzi vinavyotaka kutoa maoni yao. Pindi Hizb ut Tahrir nchini Lebanon, inayojulikana kwa kuunga mkono mambo ya Ummah na kutaka harakati za majeshi, ilipotaka kukuongozeni katika maandamano mbele ya ubalozi wa Misri na wengineo, vikosi vya usalama viliingiwa na uoga kama mtu aliyetekwa na shetani, bila kutaka harakati au usemi wowote! Licha ya watoaji maamuzi ya kisiasa nchini, wale wanaodhibiti vyombo vya usalama, wakidai uadui dhidi ya Mayahudi, wanaona katika neno la haki na wito wa kusonga kwa vikosi vya Ummah ni tishio kwao. Kinyume chake, hawaoni usaliti wa mipaka ya baharini uliotokea au usaliti wa uwekaji mipaka ya ardhini utakaotokea kuwa ni jambo linalostahiki uingiliaji wao ili kuwatia nguvuni wale waliousaliti Umma na imani yake. Badala yake, wanasonga kunyamazisha neno na sauti ya haki inayoonyesha hisia za kweli za Ummah na hasira yake iliyofichika.

Enyi Waislamu nchini Lebanon:

Tunazichukulia nyakati hizi kuwa muhimu katika maisha ya Ummah, kwani imethibitishwa kwamba kwa rasilimali chache, mengi yanaweza kutimizwa. Imedhihirika kwamba kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu (swt) na Nusrah (Ushindi) wake mbebaji silaha anaweza kuwa mshindi, sio kutokana na aina au teknolojia ya silaha anayoibeba. Adui wa Ummah ni dhaifu na muoga, anapigana tu kama alivyosema Mola wetu Mtukufu:

[لَا يُقَاتِلُونَكُمْ جَمِيعاً إِلَّا فِي قُرًى مُّحَصَّنَةٍ أَوْ مِن وَرَاءِ جُدُرٍ]

“Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipo kuwa katika vijiji vilivyo zatitiwa kwa ngome, au nyuma ya kuta.” [Al-Hashr:14]. Na wanatoa nguvu zao pekee kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyosema:

[ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلَّا بِحَبْلٍ مِنَ اللهِ وَحَبْلٍ مِنَ النَّاسِ]

“Wamepigwa na udhalili popote wanapo kutikana, isipo kuwa wakishika kamba ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu.” [Aal-i-Imran:112]. Lau si tawala za kikhiyana katika ardhi zetu zinazolinda umbile la Mayahudi, na nyuma yao mkoloni, makafiri Magharibi, umbile hili lingekuwepo kwenye jaa la historia muda mrefu uliopita!

Enyi Waislamu nchini Lebanon:

Nyinyi ni sehemu ya Umma mtukufu, Ummah uliotawala dunia kwa zaidi ya karne 13, ukiongoza kwa ubwana na kutangulia kwa mafanikio. Msiruhusu viongozi wa Lebanon wakutengeni na Ummah wenu katika miradi inayomtumikia adui mkoloni pekee. Simameni pamoja na Ummah wenu, mukiinua bendera ya mabadiliko yanayotarajiwa, mabadiliko ambayo yanarudisha fahari na utukufu wa Ummah wenu, na kurudisha uzito wenu muhimu na wa kweli hapa nchini Lebanon. Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon inakunyoosheeni mkono ili kufanya mabadiliko kwa njia ya Utume. Kuweni miongoni mwa waundaji wa mabadiliko haya ambao ishara zao zimeanza kuonekana kwenye upeo wa macho.

Enyi Waislamu nchini Lebanon:

Kafiri mkoloni ameifanya Lebanon kuwa jukwaa la kueneza usekula, na nembo yake katika hali yake ya sasa, umbile dhaifu linalotumikia ajenda za dola kubwa, kimsingi Marekani. Msikubali kwamba ibakie hivi. Irudisheni iwe ni jukwaa la haki na ngome ya Uislamu, nanyi mkiwa walinzi wa Dini, na sio walinzi wa wafisadi. Kuweni kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyosema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا أَنصَارَ اللهِ]

“Enyi mlio amini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu” [As-Saff:14] Ili atimize ahadi Yake kwenu, kama Yeye (swt) alivyosema:

[فَأَيَّدْنَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَى عَدُوِّهِمْ فَأَصْبَحُوا ظَاهِرِينَ]

“Basi tukawaunga mkono walio amini dhidi ya maadui zao, wakawa wenye kushinda.” [As-Saff:14].

H. 23 Dhu al-Qi'dah 1445
M. : Ijumaa, 31 Mei 2024

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Lebanon

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu