Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

28 Rajab 1342 H – Kuvunjwa kwa Khilafah: Waislamu Wamefaradhishiwa Kuisimamisha

 (Imetafsiriwa)

Uchaguzi Mkuu wa 14 ambao utafanyika mnamo 9 Mei 2018 utaamua ima Serikali ya Kitaifa ya Barisani itaendelea kutawala au historia itabuniwa ambapo upinzani itaunda serikali mpya. Pia tunaweza kushuhudia kuundwa kwa serikali ya muungano ya pande husika washindani lau Barisan au Pakatan Harapan hawatoweza kushinda wingi wa kura - kila kitu kitajibiwa baada ya uchaguzi. Hali hizi zote ni sehemu ya mchakato wa uchaguzi wa kidemokrasia; serikali mpya itachaguliwa pale ambapo muda wa serikali iliyopita utakapoisha. Wale ambao watakuwa wamechaguliwa wataanza kutekeleza kazi yao ya utungaji sheria ndani ya mchakato wa kisekula wa kidemokrasia.

Kinachotakiwa kufahamika ni kwamba mchakato wa uchaguzi haukuwekwa kama njia ya kubadilisha nidhamu ya kisekula-kidemokrasia au nidhamu nyingine. Kinyume chake ni kuwa uchaguzi upo kuhakikisha muendelezo wa nidhamu ya kisekula-kidemokrasia. Utekelezaji wa nidhamu ni moja ya ushindi mkubwa wa nguvu za Wamagharibi wakoloni katika kuzuia nidhamu ya Uislamu kutosimamishwa tena. Nidhamu ya Khilafah imetoa ulinzi na kuleta ustawi kwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu kwa takribani miaka 1300 kabla ya kuvunjwa na msaliti Mustafa Kemal Ataturk mnamo 28 Rajab 1342 Hijria au 3 Machi 1924 ndani ya Uturuki ya Kiuthmaniyya. Tangu kupoteza mlinzi wao, Waislamu walianza kuwa waathriwa wa mizozo ya kimataifa.

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Hakika Imamu (Khalifah) ni ngao (ulinzi) ambaye nyuma yake munapigana na kujilinda.” [Hadith imesimuliwa na Bukhari, Muslim na Ahmad]

Miongoni mwa majanga ambayo yamewafika Waislamu kutokana na kuvunjwa kwa Khilafah ni mzozo ndani ya ardhi tukufu ya Palestina. Al-Aqsa iliyoshuhudia tukio la Isra' wal Mi'raj la Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) mnamo 27 Rajab ambayo hivi sasa inakoloniwa na utawala wa Kizayuni. Damu nyingi ya Waislamu imemwagwa ndani ya ardhi tukufu na mamilioni wanaishi kama wakimbizi kutokana na mauaji yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni. Kutoka magharibi kwenda mashariki ya dunia, Waislamu ni waathiriwa.

Waislamu ndani ya Arakan wanawindwa na kuuliwa kinyama na utawala wa Myanmar. Waislamu ndani ya Syria wanauliwa pasina huruma, wanalipuliwa na kutiwa gesi na utawala wa Bashar kwa usaidizi wa Urusi na washirika wake. Hali kama hiyo imewatokea Waislamu ndani ya Afghanistan, Iraq, Kashmir, Kusini mwa Thailand, Kusini mwa Ufilipino, Xinjiang na Chechnya.

Enyi Ummah wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), mushafikiria kwa nini majanga haya yanawafika Waislamu? Je wao (Waislamu duniani kote) sio kaka na dada zetu katika Imani?

Kwa uhakika ni kaka na dada zetu tuliofungamana nao kwa kalimah ya tauhid (Mwenyezi Mungu mmoja) Laa Ilaha Illallah, Muhammadur Rasulullah. Lakushangaza, minyororo iliyofunga mipaka ya dola za mataifa iliyobuniwa na Wamagharibi imefutilia mbali fungamano la udugu miongoni mwetu. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ)

“Hakika Waumini ni ndugu” [TMQ al-Hujurat (49):10]

Enyi Waislamu! Tumekuja kutambua kwamba hakuna katika watawala Waislamu wanatulinda kama ilivyokuwa wakati wa Khalifah Al-Mu'tasim. Hakuna Salahuddin Al-Ayubi ambaye atapigana jihad ili kuikomboa ardhi tukufu ya Palestina. Leo, watawala Waislamu pasina aibu na hatia wanafanya uhadaifu kwa kushirikiana na makafiri Wamagharibi ili kuwapiga vita dhidi ya Waislamu wenzao. Mbele ya Waislamu wanatoa hotuba nzito wakijidai kuwa wanaulinda Ummah lakini siku inayofuata, wanawakumbatia na kupeana mikono na maadui wa Uislamu ambayo ni majuzi tu imejaa damu za Waislamu. Hivyo ndivyo ulivyo unafiki na uhadaifu wa watawala Waislamu ambao kiuhalisia ni vikaragosi vya Wamagharibi na hawawezi kuaminika. 

Enyi Waislamu! Juhudi ya kuregesha tena nidhamu ya Khilafah lazima ianze kwa ufahamu kwamba sheria zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt) lazima zipewe nafasi ya juu ndani ya utawala wa taifa. Mwenyezi Mungu ametuletea wahyi kupitia Al-Qur’an na Sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) njia ya kutekeleza hukmu za Mwenyezi Mungu kwa hali nzuri ya ukamilifu.

Hii inaweza kufaulu kwa kusimamisha Dola ambayo inatekeleza nidhamu ya utawala wa Kiislamu kwa ukamilifu ikimaanisha Dola ya Khilafah. Dola ya Khilafah ndio mama wa utekelezaji wa hukmu tofauti tofauti za kiwahyi ndani ya maisha yetu. Dola ya Khilafah ilipovunjwa mnamo 28 Rajab 1342 Hijria sehemu kubwa ya Shari’ah haiwezi kutekelezeka. Ni sehemu ndogo za sheria ya Uislamu kuhusiana na akhlaq, ibada na nyanja iliyofungika ya mahusiano (muamalat) imebakia kutekelezwa. Ni jambo la kusikitisha kiukweli kwamba baada ya kuanguka kwa

Dola ya Khilafah, mama wa faradhi zote, maisha ya Kiislamu ambayo yalikuwepo kwa zaidi ya miaka 1300 yamepotea kutoka ndani ya Ummah.

Kurudisha tena Khilafah ni kazi ya kisiasa iliyo faradh na yenye hadhi pasina Khilafah, Shari’ah haiwezi kutekelezeka kiukamilifu. Hii ni kwa mujibu wa msingi wa kishari’ah unaosema Mâ lâ Yatimmu al-Wâjibu illâ bihi fa Huwa Wâjib (kile ambacho faradhi haiwezi kutekelezeka pasinacho, basi nacho huwa ni faradhi). Mtume (saw) ambaye ndiye mfano wetu wa nuru ametuelezea wazi kuhusu njia ya kusimamisha nidhamu ya utawala wa Khilafah. Ni njia hii ndiyo tunayotakiwa kuifuata katika kusimamisha Dola ya Khilafah. Ni njia hii ndiyo itakayotuletea mabadiliko ya kweli – ambapo sheria za mwanadamu zitaondolewa kabisa kwa sheria za Mwenyezi Mungu (swt). Hakika, chama kitakacho tawala baada ya uchaguzi, lau nidhamu itabakia ile ile - nidhamu ya kisekula-kidemokrasia, kiuhalisia itakuwa bado mabadiliko ya kweli hayajapatikana.

Enyi Waislamu! Hakika heshima, ustawi na mabadiliko ya kweli ndani ya ummah wa Kiislamu yataweza kupatikana kwa kurudisha Dola ya Khilafah, taasisi ya upeo ya kisiasa ya Waislamu. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa vizazi ambavyo viliishi chini ya kivuli cha Khilafah. Na kwa Mwenyezi Mungu akitujaalia, ndivyo tunavyoomba iwe kwa kusimamishwa tena kwa taasisi hii inayowaunganisha Waislamu. Al-Qur’án na Sunnah zitakuwa ndio zinasimamia mambo ya maisha na dola. Utukufu ambao umepotea kwa muda wote huu hakika utarudi kwetu kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu (swt).

Na nuru ya kheri na uzuri itaangaza mionzi yake katika pembe ya dunia. Na dunia yote itafunikwa na baraka na huruma kutoka kwa Mwenyezi Mungu Azza wa Jalla.

Enyi Kaka na Dada, Mwenyezi Mungu Azza wa Jalla ameipa nguvu mikono yenu kumchagua na kumpa baiyah Khalifah ambaye ataongoza dunia hii kwa mujibu wa maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu na hatimaye kuleta ushindi na utukufu kwenu. Hivyo basi, amkeni kaka na dada zangu! Tujifufueni wenyewe - tujiunge na Shabab wa Hizb ut Tahrir katika juhudi za kusimamisha tena Uislamu. Hakika, Hizb ut Tahrir iko miongoni mwenu na pamoja nanyi. Hizb ut Tahrir imemuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kufanyakazi kwa juhudi za juu na kujitolea ili kueneza ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kutafuta nusrah (msaada) ili maisha ya Kiislamu yaweze kuhuishwa kwa kusimamisha Dola ya Khilafah ya ar-Rashidah (Uongofu) kwa njia ya Utume. Kwa Mwenyezi Mungu tunaomba msaada na kutaka ulinzi.

H. 26 Rajab 1439
M. : Ijumaa, 13 Aprili 2018

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu