Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Nussrah Iliyoleta Hijrah Hadi Dar ul-Islam, Al-Madinah Al-Munawwara

(Imetafsiriwa)

Kwa kuanza kalenda ya Hijria katika mwezi mtukufu wa Muharram, Waislamu wanakumbuka tukio ambalo limefafanua kalenda ya Ummah kwa zaidi ya karne kumi na tatu, Hijrah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) hadi Dar ul Islam (Makaazi ya Uislamu), katika al-Madinah al-Munawarrah.

Mwenyezi Mungu (swt) amewapa Waislamu wa mwanzo heshima yake, akapitisha thawabu kwao na akazitaja sifa zao katika Qur'an Tukufu. Yeye (swt) aliyaita makundi mawili ya kindugu, ambayo yalifanikisha dhamira ya kuasisi Dola ya Kiislamu, kama Muhajirin na Ansar. Muhajirin ni wale waliofanya Hijrah kwa ajili ya Dini ya Mwenyezi Mungu na Ansar ni wale waliowapatia Nussrah (Usaidizi wa Kimada) kwa ajili ya Deen hii.

Hijrah ilikuwa tangazo la kuasisiwa kwa Dola ya Kiislamu na uhamiaji kwenda kwenye Makao ya Uislamu (Dar ul-Islam), huku Nussrah ilitolewa kwa ajili ya Hijrah hii yaani kwa ajili ya kusimamisha Dar ul-Islam. Bila Nussrah na Ansar, kusingekuwa na Hijrah wala Muhajirin. Kwa hivyo, ni vipi Muislamu, anayesoma Qur'an mara nyingi na ndani yake kukutana na sifa za Muhajirin na Ansar, anaweza kupuuza thamani ya Hijrah na Nussrah?

Kwa kuwa tunazungumzia Nussrah, ambayo baada ya yake Hijrah ilifanyika, ni lazima kuiregelea Seera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kufuata mfano wake. Juhudi za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) mjini Makka zilielekezwa katika kuasisi Makao ya Uislamu (Dar ul Islam). Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alifuata njia iliyofafanuliwa, na hatua muhimu zilizoelezewa waziwazi, ili hatua hizi ziweze kuigwa na vizazi vya baadaye wakati Dar ul-Islam itakapokuwa hakuna. Kwa kweli kufuata njia hii wazi ni lazima katika kufanya kazi ya kusimamisha Dar ul-Islam.

Katika mwaka wa kumi wa Utume, miaka mitatu kabla ya Hijrah, ammi yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), Abu Talib, alifariki. Abu Talib alitoa kiasi fulani cha Nussrah na ulinzi ambao ulimwezesha Mtume kubeba ulinganizi wa Uislamu kwa salama. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aligundua kuwa jamii mjini Makka haikuathiriwa sana na ulinganizi wa Uislamu, na hakukuwa na rai jumla imara kwa Uislamu na fahamu zake. Ilikuwa katika hali hii ambapo Mwenyezi Mungu (swt) alimwamuru (saw) kutafuta Nussrah. Nussrah inamaanisha Msaada Mzuri, katika kamusi za lugha. Nasr inamaanisha kuwasaidia wahasiriwa wa dhulma, huku Ansar inamaanisha kundi la wale ambao hutoa msaada kwa wanyonge. Ndani ya sura yenye kichwa. "Juhudi za Mtume (saw) kutafuta Nussrah kutoka kabila la 'Thaqeef'" katika Seerat ibn Hisham, imeripotiwa:

قَالَ ابْنُ إسْحَاقَ: وَلَمّا هَلَكَ أَبُو طَالِبٍ، نَالَتْ قُرَيْشٌ مِنْ رَسُولِ اللّهِ (صلى الله عليه وآله وسلم) مِنَ الأَذَى مَا لَمْ تَكُنْ تَنَالُ مِنْهُ فِي حَيَاةِ عَمّهِ أَبِي طَالِبٍ، فَخَرَجَ رَسُولُ اللّهِ (صلى الله عليه وآله وسلم) إلَى الطّائِفِ يَلْتَمِسُ النّصْرَةَ مِنْ ثَقِيفٍ، وَالْمَنَعَةَ بِهِمْ مِنْ قَوْمِهِ، وَرَجَاءَ أَنْ يَقْبَلُوا مِنْهُ مَا جَاءَهُمْ بِهِ مِنْ اللّهِ عَزّ، وَجَلّ فَخَرَجَ إلَيْهِمْ وَحْدَهُ

“Ibn Ishaq asema: Abu Talib alipokufa, Maquraishi walimtesa sana Mtume (saw) ambapo hawakuweza wakati wa zama za ammi yake (saw). Mtume (saw) aliondoka kwenda Taif kwa ajili ya kutafuta nusra na ulinzi na aliwauliza wakubali yale aliyokuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Alikwenda Ta’if peke yake.”

Imesimuliwa kutoka kwa Ibn Abbas (ra) katika Fath ul-Bari ya Ibn Hajar, Tuhaft ul-Ahwadhi na al-Kalam pamoja na Hakim, Abu Nua'im na Baihaqi katika Dala'il kwa riwaya sahih, Ibn Abbas amnukuu Ali ibn Abi Talib ambaye anasema:

لَمَّا أَمَرَ اللَّهُ نَبِيّه أَنْ يَعْرِض نَفْسَه عَلَى قَبَائِل الْعَرَب، خَرَجَ وَأَنَا مِنْهُ وَأَبُو بَكْر إِلَى مِنًى، حَتَّى دَفَعَنَا إِلَى مَجْلِس مِنْ مَجَالِس الْعَرَب

Pindi Mwenyezi Mungu (swt) alipomwamuru Mtume wake (swt) aende kwenye makabila ya Kiarabu, mimi na Abu Bakr tuliandamana na Mtume (saw) hadi Mina hadi kwenye vikao miongoni mwa makabila ya Kiarabu.”

Kwa hivyo imethibitika kuwa amri ya kuyaendea makabila ya Kiarabu na kutafuta nusra yao, pamoja na wakati muwafaka wa kuyaendea huku ilitoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) kama inavyoonekana kutoka kwa riwaya ya Ali ibn Abi Talib (ra) hapo juu. Wakati wa amri hii unasadifiana na kupoteza ulinzi na nusra kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Hakuwa salama tena na kulindwa, Maquraishi hawakumruhusu kubeba ulinganizi wa Mwenyezi Mungu, na wakati huo huo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) hakuwa na matumaini kwamba jamii mjini Makka ingekubali mamlaka yake, kwani rai jumla yenyewe huko Makka haikuupendelea Uislamu. Kwa hivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliamrishwa kutafuta Nussrah wakati huo ili kuimarisha Da’wah na kuufikisha Uislamu katika nafasi inayostahili katika suala la utawala, mamlaka na utekelezaji kamili wa hukmu zake.

Mtume (saw) alianza jukumu la kutafuta Nussrah kutoka Ta'if, ambayo ilihesabiwa kati ya maeneo yenye nguvu zaidi katika Bara Arabu wakati huo. Kihakika ilishindana na Maquraishi kwa nguvu, ufahari na cheo. Hili ndilo lilisisitizwa na Walid ibn Mughairah wakati alipobishana kwa nini wahyi wa Quran ulikuwa uliteremshiwa Muhammad (saw) na sio kwa waheshimiwa wa Makka na Ta’if. Mwenyezi Mungu (swt) kisha akateremsha ayah:

 [وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ هَذَا الْقُرْءانُ عَلَى رَجُلٍ مِنَ الْقَرْيَتَيْنِ عَظِيمٍ]

“And they say: “Why is not this Qur’ân sent down to some great man of the two towns (Makkah and Tâ’if)?” [Surah al Zukhruf 43:31].

Nguvu ya watu wa Ta'if inadhihirishwa na ukweli kwamba hata baada ya dola ya Kiislamu kusimamishwa baadaye, Ta'if haikufunguliwa kwa urahisi. Ilizuia uzingirwaji, na kusababisha majeruhi mazito pande zote mbili, na manati yalilazimika kurushwa ili kuvunja upinzani wao.

Mtume (saw) alisonga mbele hadi Ta’if akiwa na nia ya kukutana na wakuu wao na waheshimiwa. Alikutana na wakuu watatu na akazungumza nao juu ya Uislamu na Nussrah. Alirudi akiwa amevunjika moyo, kwa sababu ya kukataliwa Nussrah na wakuu wa kikabila wa Taif. Huu ulikuwa mwanzo. Mtume alirudi kutoka Ta'if na kukaa na al-Mut'im ibn 'Adai nje kidogo ya Makka na akaanza kuwaendea viongozi wenye nguvu wa makabila mengine ya Kiarabu wakati wa misimu ya Hajj. Viongozi hawa wa makabila walikuwa sawa na wakuu wa serikali katika nyakati zetu. Katika Seerah ya ibn Hisham, ndani ya sura kuhusu Mtume (saw) kuyaendea makabila, Ibn Ishaq asema:

ثُمّ قَدِمَ رَسُولُ اللّهِ (صلى الله عليه وآله وسلم) مَكّةَ، وَقَوْمُهُ أَشَدُّ ...، فَكَانَ رَسُولُ اللّهِ (صلى الله عليه وآله وسلم) يَعْرِضُ نَفْسَهُ فِي الْمَوَاسِمِ إذَا كَانَتْ عَلَى قَبَائِلِ الْعَرَبِ يَدْعُوهُمْ إلَى اللّهِ، وَيُخْبِرُهُمْ أَنّهُ نَبِيّ مُرْسَلٌ، وَيَسْأَلُهُمْ أَنْ يُصَدّقُوهُ وَيَمْنَعُوهُ حَتّى يُبَيّنَ (لَهُمْ) اللّهُ مَا بَعَثَهُ بِه

“Mtume (saw) alikuja Makka lakini watu wake (Maquraishi) walikuwa wakali zaidi dhidi ya dini yake kuliko hapo awali... Mtume (saw) aliyaendea makabila wakati wa msimu wa hajj na akawalingania kwa Mwenyezi Mungu, akiwaambia kwamba ametumwa na Mwenyezi Mungu na kuwahimiza wamuamini yeye na wamlinde mpaka Mwenyezi Mungu (swt) atakapowadhihirishia aliyomtumiliza kwayo.”

Vitabu vya Seerah vinafichua kuwa wakati wa msimu wa Hajj, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) yeyote alikuwa na wadhifa wa heshima na alikuwa na nguvu. Katika Seerah na Ibn Hisham, ndani ya sura "Mtume (saw) aliwaendea Waarabu wakati wa misimu", inasema: "Ibn Ishaq amesema:

وَكَانَ رَسُولُ اللّهِ (صلى الله عليه وآله وسلم) عَلَى ذَلِكَ مِنْ أَمْرِهِ، كُلّمَا اجْتَمَعَ لَهُ النّاسُ بِالْمَوْسِمِ أَتَاهُمْ يَدْعُو الْقَبَائِلَ إلَى اللّهِ وَإِلَى الإِسْلاَمِ، وَيَعْرِضُ عَلَيْهِمْ نَفْسَهُ وَمَا جَاءَ بِهِ مِنْ اللّهِ مِنْ الْهُدَى وَالرّحْمَةِ، وَهُوَ لا يَسْمَعُ بِقَادِمِ يَقْدَمُ مَكّةَ مِنْ الْعَرَبِ لَهُ اسْمٌ وَشَرَفٌ، إلا تَصَدّى لَهُ فَدَعَاهُ إلَى اللّهِ وَعَرَضَ عَلَيْهِ مَا عِنْدَهُ”

“Mtume (saw) aliendelea kufuatilia jambo hili (la Nussrah na ulinzi) kila wakati watu walipokutana naye wakati misimu ya (hajj), aliyalingania makabila kwa Mwenyezi Mungu na kwa Uislamu na akajiwasilisha kwao na pamoja na mwongozo na rehma alizokuja nazo  kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Mtume (saw) hakusikia juu ya mtu yeyote wa maana na heshima aliyetembelea Makka isipokuwa alimlingania kwa Mwenyezi Mungu na akawasilisha wito wake kwake.”

Kwa hivyo Nabii aliwatembelea Bani Kalb na wakakataa kumkubali, akawajia Bani Hanifah wa al-Yamamah mahali pao na walifanya ujeuri sana hakuna kabila jengine la Kiarabu lililofanya kama wao. Mtume aliwalingania Bani ‘Aamer ibn Sa’sa’ ambao walikataa isipokuwa awape mamlaka baada yake. Mtume (saw) alikataa ofa hii ya masharti. Kisha aliwatembelea Bani Kindah wa Yemen kwenye kambi yao na pia walidai mamlaka baada yake na kwa hivyo Mtume alikataa Nussrah yao. Aliwalingania Bakr bin Wa’il katika kambi zao; walikataa kumlinda Mtume (saw) kwa sababu walikuwa karibu na Uajemi. Wakati Mtume (saw) alipotembelea kambi ya Bani Rabee’ah, hawakujibu. Mtume (saw) aliwalingania Bani Shaiban katika kambi zao ambazo pia zilikuwa karibu na Uajemi. Bani Shaiban walijitolea kumlinda Mtume (saw) kutoka kwa Waarabu lakini sio Waajemi, kwa hivyo Mtume (saw) akawajibu:

«ما أسأتم الرد إذ أفصحتم بالصدق، إنه لا يقوم بدين الله إلا من حاطه من جميع جوانبه»

“Ufafanuzi wenu katika jibu ni wa kukataliwa. Hakuna anayesimama na Dini ya Mwenyezi Mungu isipokuwa yule anayeshughulikia mambo yake yote.”

Mtume (saw) aliendelea kutafuta Nussrah licha ya kabila kadhaa kukataa; hakuteteleka, wala hakukata tamaa wala hakubadilisha mwendo wake. 'Zaad al Ma'ad' anaripoti kutoka kwa al-Waqidi ambaye anasema:

وَكَانَ مِمّنْ يُسَمّى لَنَا مِنْ الْقَبَائِلِ الّذِينَ أَتَاهُمْ رَسُولُ اللّهِ (صلى الله عليه وآله وسلم) وَدَعَاهُمْ وَعَرَضَ نَفْسَهُ عَلَيْهِمْ بَنُو عَامِرِ بْنِ صَعْصَعَة، وَمُحَارِبُ بْنُ حصفة، وَفَزَارَةُ، وَغَسّانُ، وَمُرّةُ، وَحَنِيفَةُ، وَسُلَيْمٌ، وَعَبْسُ، وَبَنُو النّضْر،ِ وَبَنُو الْبَكّاءِ، وَكِنْدَةُ، وَكَلْبٌ، وَالْحَارِثُ بْنُ كَعْبٍ، وَعُذْرَةُ، وَالْحَضَارِمَةُ، فَلَمْ يَسْتَجِبْ مِنْهُمْ أَحَد

“Makabila tunayoyajua ambao Mtume (saw) aliyaendea na kuwalingania ni Banu 'Aamer ibn Sa'sa', Muharib ibn Hafsah, Fazarah, Ghassan, Murrah, Haneefah, Sulaym, 'Abs, Banu Nadhar, Banu Bika', Kindah , Kalb, Harith ibn Ka'ab, 'Udrah na Mahadhrami. Hakuna hata mmoja wao aliyejibu kwa njia chanya.”

Mtume (saw) aliendelea kutafuta Nussrah mpaka Mwenyezi Mungu (swt) akaibariki dini yake na Nussrah. Ibn Ishaq amenukuliwa katika Seerah ya ibn Hisham:

فَلَمّا أَرَادَ اللّهُ عَزّ وَجَلّ إظْهَارَ دِينِهِ وَإِعْزَازَ نَبِيّهِ (صلى الله عليه وآله وسلم) وَإِنْجَازَ مَوْعِدِهِ لَهُ خَرَجَ رَسُولُ اللّهِ (صلى الله عليه وآله وسلم) فِي الْمَوْسِمِ الّذِي لَقِيَهُ فِيهِ النّفَرُ مِنْ الأَنْصَارِ، فَعَرَضَ نَفْسَهُ عَلَى قَبَائِلِ الْعَرَبِ، كَمَا كَانَ يَصْنَعُ فِي كُلّ مَوْسِمٍ. فَبَيْنَمَا هُوَ عِنْدَ الْعَقَبَةِ لَقِيَ رَهْطًا مِنْ الْخَزْرَجِ أَرَادَ اللّهُ بِهِمْ خَيْرا

“Wakati Mwenyezi Mungu (swt) alipoamuru kutawala kwa Dini Yake na kumkirimu Mtume wake (saw) na kutimiza ahadi Yake, Mtume (saw) alitoka nje katika msimu wa hajj alipokutana na watu wa Ansar. Alijiwasilisha kwa makabila hayo ya Kiarabu kama alivyokuwa akifanya wakati wa misimu ya hajj. Kwa hivyo wakati alipokuwa yuko al-‘Aqabah, alikutana na watu kutoka kabila la Khazraj ambao Mwenyezi Mungu (swt) alitaka kuwabariki.”

Watu hao kutoka Khazraj walikubali wito wake na wakaenda kupatanisha mzozo wao na kabila la Aws. Walirudi mwaka uliofuata wakiwa na watu kumi na wawili na walikutana na Mtume (saw) huko al-‘Aqabah. Hii ilikuwa Bay’ah ya kwanza ya ‘Aqabah. Halafu baadaye, jamii ya Madina iliandaliwa na Mus'ab ibn 'Umair (ra), wakuu wa mji huo walimtembelea Mtume (saw) kumpa ulinzi na nusra yao. Walikutana na Mtume (saw) tena huko al-‘Aqabah na wakatoa ahadi ya utiifu ambayo ilikuwa ahadi ya kupigana pamoja na Mtume (saw). Seerat ibn Hisham inasimulia kutoka kwa Mtume (saw) wakati wa Bay'a hii (Ahadi):

ثُمّ قَال: أُبَايِعُكُمْ عَلَى أَنْ تَمْنَعُونِي مِمّا تَمْنَعُونَ مِنْهُ نِسَاءَكُمْ وَأَبْنَاءَكُمْ. قَالَ: فَأَخَذَ الْبَرَاءُ بْنُ مَعْرُورٍ بِيَدِهِ ثُمّ قَالَ: نَعَمْ وَاَلّذِي بَعَثَك بِالْحَقّ (نَبِيّاً) لَنَمْنَعَنّك مِمّا نَمْنَعُ مِنْهُ أُزُرَنَا، فَبَايِعْنَا يَا رَسُولَ اللّهِ، فَنَحْنُ وَاَللّهِ أَبْنَاءُ الْحُرُوبِ وَأَهْلُ الْحَلْقَةِ وَرِثْنَاهَا (كَابِرًا عَنْ كَابِرٍ)

Nachukua ahadi yenu kwamba mtanilinda kama vile mnavyowalinda wake na watoto wenu.” Al Bara 'ibn Ma'roor alimshika mkono Mtume (saw) na akasema: "Hakika, naapa kwa yule aliyekutumiliza kwa haki kama Mtume, tutakulinda kama vile tunavyowalinda watoto wetu kwa hivyo, chukua ahadi yetu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, naapa kwa Mwenyezi Mungu hakika sisi ni watoto wa vita na silaha za vita ni kama vidude vya kuchezea kwetu, haya ni urithi wetu tangu zama za baba zetu.”

Kwa hili, ahadi ya Mwenyezi Mungu ilitimizwa na dola ya Uislamu ikaasisiwa.

Enyi Waislamu wa Pakistan! Enyi Wanachuoni wa Waislamu wa Pakistan!

Na kwa hivyo Nussrah kwa Uislamu kama hukmu ilipatikana kwa njia ya Utume, ikabadilisha Yathrib iliyochanika na kugawanyika kuwa mwenge wa nguvu kwa Uislamu, Madinah Al-Manawwarah.

Hizb ut Tahrir inafanya kazi sasa na kati yetu kwa ajili ya kurudisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Hivyo basi Mashababu wake wanatuonya kuhusu ukafiri na kutulingania kuunga mkono Uislamu na Khilafah yake. Na Amiri Hizb ut Tahrir, mwanachuoni wa  fiqh mkubwa na mwana dola, Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, anafanya kazi mchana na usiku, akihatarisha maisha na viungo, ili kupata Nussrah kutoka kwa majeshi ya Dini hii. Ni juu yetu, kila mmoja wetu, kujiunga na Hizb ut Tahrir na kutia hisa yetu katika kumaliza utawala huu wa mabavu wa sasa, kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Ahmed amesimulia kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«ثُمَّ تَکُونُ مُلْکاً جَبْرِیَّةً، فَتَکُونُ مَا شَاءَ اللّٰہُ اَنْ تَکُونَ، ثُمَّ یَرْفَعُھَا اِذَا شَاءَ اَنْ یَرْفَعَھَا، ثُمَّ تَکُونُ خِلَافَةً عَلَی مِنْھَاجِ النُّبُوَّة ثُمَّ سَکَتَ»

“Kisha utakuwepo utawala wa kimabavu, utakuwepo kwa muda apendao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa anapotaka kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa Njia ya Utume.” Kisha akanyamaza.

Enyi Waislamu wa Majeshi ya Pakistan! Enyi Watu wa Nussrah! Enyi Maanswari wa leo!

Njia ya Utume ya kusimamisha Uislamu inataka Nussrah kutoka kwa watu wake, ambao ni kila mmoja wenu. Watoto, binti, kaka, dada, baba na mama zenu wanakuiteni, wakitarajia mutimize wajibu wenu. Suala la Nussrah ni suala lenu, na wakati huu ni wenu, kwa hivyo timizeni jukumu lenu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) na mtafanikiwa. Jihadharini na kuusaliti Umma wenu na kuvunja viapo vyenu kwa kuunga mkono demokrasia ya kikafiri inayoanguka, ambayo haina msaada wa watu. Jihadharini kupoteza Akhera yenu kwa maisha ya kidunia ya wavunaji kiapo, ambayo huchafua safu ya uongozi wetu! Rudisheni Khilafah kwa Njia ya Utume kwa kutoa Nussrah kwa Hizb ut Tahrir. Kwa kufanya hivyo, mkishinda na mkaushinda ukafiri na watu wake, mtafurahi na waumini pia.

 [إِنْ يَنْصُرْكُمُ اللَّهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ وَإِنْ يَخْذُلْكُمْ فَمَنْ ذَا الَّذِي يَنْصُرُكُمْ مِنْ بَعْدِهِ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ]

“Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” [Surah Aali-Imran 3: 160]

H. 1 Muharram 1443
M. : Jumatatu, 09 Agosti 2021

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu