Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Enyi Maulamaa Waheshimiwa wa Pakistan! Gaza Inaungua, Huku Watawala wa Pakistan waki ni Watazamaji Wasiochukua Hatua. Lazima Muwanusuru Waislamu wa Gaza, kwa Kutoa Wito wa Jihad kwa Wanajeshi wa Pakistan kwa ajili ya Ukombozi wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

(Imetafsiriwa)

Maulamaa waheshimiwa wa Pakistan! Umbile la Kiyahudi linaijaza anga ya Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina moto na moshi, huku ikinywesheza ardhi yake kwa damu na machozi ya Waislamu. Miezi miwili imepita, ilhali, hakuna jeshi hata moja la Waislamu lililotaharaki kulifukuza jeshi la adui linaloshambulia. Hivyo, tunakuhutubieni kama Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) wanavyotufahamisha lazima uwe. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ]

“Kwa hakika wanao mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni.” [Surah Fatir: 28]. Kutoka kwa Abu Ad-Dardaa’ (ra), Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, العلماء ورثة الأنبياء  “Maulamaa ni warithi wa Mitume.” [Abu Dawud, Tirmidhi] Hivyo, baada ya zama za Mtume wa mwisho (saw) kutumwa kwa wanadamu, na mwisho wa Wahyi, ni lazima muwe kama walivyokuwa Mitume (as), kuchunga mambo ya watu, kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt).

Enyi Warithi wa Mitume (as)! Nyuma ya matukio ya mgogoro wa sasa huko Gaza, vibaraka wa Biden wanataka uungaji mkono wenu katika kuisalimisha Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina kwa umbile linaloikalia kwa mabavu la Mayahudi, kupitia “suluhisho” la Magharibi linalopigiwa debe na watawala wa Waislamu, juu ya Waarabu na Ajami (wasio Waarabu). Wanakuleteeni “suluhisho la dola mbili” kama suluhisho la hali ya sasa, ingawa hilo linaloitwa suluhisho ni udanganyifu tu. “Suluhisho la dola mbili” husababisha kuimarishwa kwa umbile la Mayahudi. Njia za kuishi  kwa Waislamu nchini Palestina zitakuwa kwenye rehema ya umbile katili na lisilo na huruma la Mayahudi. Ulinzi wao utakuwa mikononi mwa umbile la Mayahudi. Zaidi ya hayo, “usuluhisho wa dola mbili” linachochea ujasiri wa umbile la Mayahudi kueneza moto wa Fitnah yake, kutoka kuwa ndani ya eneo pekee, hadi nje yake.

“Suluhisho” la Kimagharibi ni suluhisho la Marekani. Kuunga mkono “suluhisho la dola mbili” ni khiyana kwa Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake (saw) na waumini. Ardhi ya Waislamu ni utakatifu ambao haujuzu kwa Waislamu kuisalimisha. Mwenyezi Mungu (swt) ameharamisha kukubali aina yoyote ya utukufu wa makafiri juu ya Waislamu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt),

[وَلَن يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا]

“wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [Surah An-Nisaa 4:141]. Mwenyezi Mungu (swt) ameifanya kuwa faradhi ya Shariah kumaliza unyakuzi wa makafiri wa ardhi za Waislamu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt),

[وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ]

“na muwatoe popote walipo kutoeni.” [Surah Al-Baqarah 2:191]. Amri ya Mwenyezi Mungu (swt) inahusiana na ardhi yoyote ya Waislamu, huku ardhi ya Palestina ni ardhi ya Msikiti wa Al-Aqsa, Kibla cha Kwanza, Haram iliyotakaswa, eneo la Isra'a na Miraj ya Mtume (saw), ambaye Mwenyezi Mungu (swt) amevibariki viunga vyake mpaka Siku ya Kiyama!

Enyi Maulamaa Waheshimiwa! Watawala wa Pakistan wanaelekea katika kulitambua umbile la Mayahudi, kwa badali ya fedha kutoka kwa watawala wasaliti wa dola za Ghuba, vibaraka wa Magharibi. Wanataka muidhinishe “suluhisho la dola mbili” la Marekani. Kwa hiyo watawala hawa wanatumia hadhi yenu ya kidini ndani ya Ummah kuimarisha misimamo yao ya khiyana. Kwa njia ya kuwaonya dhidi ya udanganyifu wa watawala hawa, tunakukumbusheni kauli ya Umar al-Farooq (ra), kama ilivyosimuliwa na ad-Darami:

هَلْ تَعْرِفُ مَا يَهْدِمُ الإِسْلاَمَ؟ قَالَ قُلْتُ، لاَ. قَالَ يَهْدِمُهُ زَلَّةُ الْعَالِمِ وَجِدَالُ الْمُنَافِقِ بِالْكِتَابِ وَحُكْمُ الأَئِمَّةِ الْمُضِلِّينَ

“Je, unajua ni kitu gani chenye kuvunja Uislamu?” Asema nikasema, “Hapana.” Umar akasema, “Unavunjwa kwa mtelezo wa mwanachuoni (‘Alim), na mjadala wa wanafiki juu ya Kitabu, na utoaji hukmu wa maimamu waliopotoka.”

Hakika, mtelezo wa ‘Aalim ni mbaya zaidi kuliko mtelezo wa mtu wa kawaida. Kwa hiyo, kataeni kwa uwazi aina yoyote ya uungaji mkono kwa watawala, katika kuisaliti kwao Dini na Ummah. Wawajibishe juu ya ni kwa nini bado hawajapeleka jeshi shupavu la Pakistan, licha ya kuwa na nguvu na uwezo wa kufanya hivyo. Tangazeni kwa uwazi wajibu wa kuwatetea Waislamu wanaodhulumiwa wa Gaza, na wajibu wa Jihad kwa majeshi ya Pakistan, kwa ajili ya ukombozi wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Hakika, ni kutokuwepo kwa hatua za kijeshi ndiko kumezuia kadhia ya Palestina kutatuliwa kama inavyopaswa kutatuliwa, ili tu watawala hawa wasaliti waweze kulazimisha “suluhisho la dola mbili” la Marekani. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَتَأْمُرُنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلَتَنْهَوُنَّ عَنْ الْمُنْكَرِ أَوْ لَيُوشِكَنَّ اللَّهُ أَنْ يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عِقَابًا مِنْهُ ثُمَّ تَدْعُونَهُ فَلَا يُسْتَجَابُ لَكُمْ»

“Naapa kwa Yule ambaye kwamba nafsi yangu imo Mikononi mwake! Hamtaacha kuamrisha mema na hamtaacha kukataza maovu, isipokuwa Mwenyezi Mungu atakaribia kushusha adhabu kutoka kwake. Kisha mtamuomba na wala hamtajibiwa.” [Tirmidhi].

Enyi Maulamaa Waheshimiwa! Katika msimamo wenu kwa watawala, lazima mufuate wachamungu waliotangulia ambao walivumilia kila aina ya taabu na mitihani, lakini kamwe msiruhusu Dini yenu kuhujumiwa. Imam Abu Hanifah, Imam Ahmad bin Hanbal na Izzuddin Abdul Salam walikuwa nyota angavu wa Umma, ambao waliwawajibisha watawala, wakistahamili matatizo yote yaliyowajia. Mama yake Imam mchamungu Abu Hanifa Nuuman ibn Thabit Mwenyezi Mungu amrehemu rehema nyingi alimwambia siku moja alipokuwa gerezani يا نعمان، إن هذه المعرفة لم تنفعك إلا لضربك وسجنك، وهذا يكفي لأن تتخلى عنها “Ewe Nu’man, maarifa haya hayatakunufaisha isipokuwa kupigwa na kufungwa, na hii inatosha kwako kuyaacha.” Imam Abu Haniyfah akamjibu, يا أماه, إذا رغبت العالم لكنت حققت ذلك, ولكني أردت أن يعلم الله سبحانه وتعالى أنني أحافظ على الله للجحيم “Ewe mamangu, lau ningetamani ulimwengu ningefanikisha hilo. Hata hivyo, nilitaka Mwenyezi Mungu (swt) ajue kwamba niliilinda elimu ya Kiislamu niliyopewa na sikujisalimisha, licha ya hayo, kwenye moto wa Jahim.”

Enyi Maulamaa Waheshimiwa! Je, hamutamani heshima ya mmoja wa watangulizi wenu wachamungu, Qaadi Muhyiddin az-Zaki, ambaye alitoa hotuba ya kwanza ya Ijumaa katika Msikiti Al-Aqsa, baada ya kukombolewa na majeshi ya Salahudin, ambayo aliisoma mbele ya jeshi la washindi,

[فَقُطِعَ دَابِرُ الْقَوْمِ الَّذِينَ ظَلَمُوا وَالْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ]

“Ikakatwa mizizi ya watu walio dhulumu - na wa kuhimidiwa ni Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.” [Surah Al-Anam 6:45]?! Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt), heshima hii itapeanwa kwa yule ambaye atajiunga na safu ya mbele ya mapambano ya kusimamisha Khilafah. Kwa hakika, ilikuwa ni Khilafah Rashida ya Umar al-Farooq (ra) ambayo iliifungua Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina kwa Uislamu. Alikuwa ni Salahudin Ayyubi chini ya Khilafah ya Abbasiyya ambaye aliisafisha ardhi ya Palestina kutokana na najisi ya kukaliwa kwa mabavu na Wapiganaji wa Kimsalaba. Itakuwa ni Khilafah Rashidah ya Pili kwa Njia ya Utume ambayo itaikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina kwa mara nyingine tena, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt).

Ewe Mwenyezi Mungu (swt) je hatujafikisha?! Ewe Mwenyezi Mungu (swt) shuhudia kwamba tumefikisha! Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[إِنَّ فِي هَذَا لَبَلَاغاً لِّقَوْمٍ عَابِدِينَ]

“Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada.” [Surah Al-Anbiyyah 21:106].

#ArmiesToAqsa

H. 21 Jumada I 1445
M. : Jumanne, 05 Disemba 2023

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu