Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hotuba ya Maandamano ya Hashem Gaza, Nyuma ya Matukio ya Al-Quds na Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa.  
Mashambulizi ya Kiyahudi dhidi ya Al-Aqsa Yayalazimu Majeshi ya Kiislamu Kutangaza Vita Kuling'oa Umbile Lao

(Imetafsiriwa)

Enyi Waislamu: Je, haujafika wakati kwenu kuzinyenyekesha nyoyo zenu kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na yale yaliyoteremshwa kwa haki, na musonge katika kuinusuru Al-Aqsa, kabla ya kugawanya kwake kupitia wakati na nafasi kuwa kweli, kisha majuto hatamfaidi mtu?!

Kutoka katikati mwa Hashem Gaza, tunaelekeza miito hii kwa Ummah, majeshi yake, na wanazuoni wake:

Enyi Umma wa Kiislamu: Lindeni Kibla chenu cha kwanza na Masra ya Mtume wenu, inukeni kwenye utukufu wa dunia hii na Akhera, wakomesheni watawala wenu madhalimu, milikini uamuzi wenu wa kumsimamisha Khalifa ambaye: Ataunganisha safu zenu na neno lenu, atajisalimisha kwa Mwenyezi Mungu na kukuongozeni nyinyi mnaopigana katika njia ya Mwenyezi Mungu ili kuukomboa msikiti wenu na ardhi yenu, ndiye Khalifa, kama alivyosema Mtume wetu (saw): «جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Imam ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujihami kwake.”

Enyi Wanajeshi Mashujaa: Mnawezaje kuutelekeza Msikiti wenu wa Al-Aqsa na kuuacha kuwa windo jepesi la umbile la Kiyahudi, linalotaka kuugawanya na kufanya uharibifu ndani yake? Kwa nini mnawaacha watu wa Palestina peke kukabiliana na umbile la Kiyahudi wakati muna nyenzo na zana? Umefika wakati wa nyinyi kuyakusanya majeshi yenu na kuinisuru Palestina na watu wake na Aqsa yake, na kuling'oa umbile la Kiyahudi. Endapo mtawala dhalimu atasimama kati yenu na harakati hii, musimtii, simameni dhidi yake na musimsikilize, kwa sababu mababu zetu mashujaa waliwasagasaga Watatari huko Ain Jalut kwenye ardhi ya Palestina, na waliwaangamiza Makruseda huko Hattin kwenye ardhi ya Al-Aqsa. Wakati umewadia wa kuliangamiza umbile la Kiyahudi nchini Palestina. Je, mutaitikia?

Enyi Jeshi la Misri, Jeshi la Jordan, Jeshi la Hijaz, Jeshi la Uturuki, Jeshi la Pakistan... Enyi Majeshi ya Kiislamu: Mayahudi wameuvunjia heshima, wameuharibu na kuunajisi Msikiti wa Al-Aqsa, na sasa wanataka kuugawanya. Kuondolewa kwa umbile la Kiyahudi kunategemea uamuzi wa jeshi moja la Ummah, Ummah wote hivi karibuni utalifuata, na kuondoa tezi hii yenye saratani kutoka kwenye mwili wa Ummah.

Enyi Watu wa Palestina na Mujahidina wake: Kadhia ya Palestina ni kadhia ya jihad ya kiitikadi kwa Umma wa Kiislamu, sio kadhia ya makundi au mazungumzo kwa upande wowote. Na sisi tulio ndani Palestina hebu na tuwe ndio sababu ya kushajiisha, na wachochezi katika kuuhamisha Ummah na majeshi yake, na tuwasaidie kutekeleza wajibu wao wa jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kupigana vita vya kina vitakavyo ling'oa umbile la Kiyahudi kutoka kwenye mizizi yake na kutoridhika na duru ndogo ndogo za mapigano.

Enyi Wanazuoni wa Kiislamu: Timizeni ahadi ya Mwenyezi Mungu, na muyachochee majeshi ya Kiislamu kufanya jihad. Leo, hakuna lawama wala shutuma zitakazofaidisha. Waelezeni watu ukweli wala musiufiche, na wala musiwaogope watawala wala manufaa ya dunia yasikuzuieni kusema ukweli.

 [فَاللَّهُ أَحَقُّ أَنْ تَخْشَوْهُ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ]

“Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mumwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini.” [At-Tawba: 13].

Kwa hayo, mutairudia historia ya wanazuoni wa Mwenyezi Mungu.

Enyi Waislamu: Ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli, na Mayahudi wote wataangamia, na nyinyi mtashinda, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hebu mtu mwenye heshima na ajitokeze na kuanzisha cheche za jihad pana dhidi ya umbile hili lenye chuki. Basi ni nani atakaye pata heshima ya dunia hii na Akhera?

 [إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7]

[وَفِي ذَلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ]

“Na katika hayo washindanie wenye kushindana.” [Al-Mutaffifin: 26].

H. 29 Shawwal 1443
M. : Jumapili, 29 Mei 2022

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu