Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Enyi Ummah wa Muhammad (saw)
Je! Ni Kufa Kifo cha Udhalilifu, au Utukufu, Ushindi na Tamkini?!
(Imetafsiriwa)

Enyi Ummah wa Muhammad (saw)! Watu wa Gaza wako baina ya kifo na kifo zaidi. Ikiwa hawatakufa kutokana na mabomu, watakufa kwa njaa, kiu, au watakufa kwa maradhi. Eneo la Kaskazini la Ukanda wa Gaza liko chini ya mzingiro mkali bila ya chakula, maji, au dawa. Kwa hivyo mutafanya nini, Enyi Waislamu?

Wale waliokasirikiwa na Mwenyezi Mungu (swt), wamevunja misikiti, mahospitali, nyumba, mabirika ya maji, na huduma zote za maisha. Walinyesheza mvua ya kifo kwa watoto wetu na wanawake katika mandhari ya umwagaji damu, ya kutisha, ambayo vyombo vya habari haviripoti. Je! Mnafikiria kwamba chaneli za satelaiti zinakuletea hata nusu, au robo, ya ukweli? Vyombo vya habari vinakutangazieni mashambulizi machache tu, yanayosababisha maumivu yanayovunja moyo na uchungu.

Enyi Ummah wa Muhammad (saw)! Zaidi ya siku sabiini mauaji yamewaangamiza watu wa Gaza. Zaidi ya miaka sabiini ya kunajisi eneo la Isra ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na wale waliokasirikiwa na Mwenyezi Mungu (swt). Mumeona kwa macho yenu wenyewe uoga wa Mayahudi vitani. Sasa je mutafanya nini? Je! mnalia juu yetu, au mumechanganyikiwa na kujiondoa? Je! Mnafikiria kuridhika na hili pekee, itakuokoeni hapa ulimwenguni na kesho Akhera?!

Enyi Ummah wa Muhammad (saw)! Je! Mnajua ni mamilioni mangapi ya Waislamu wameuawa, au kuhamishwa, kwa sababu ya watawala vibaraka, na kukosekana kwa Khilafah kwa Njia ya Utume? Hawa ni wale wa Iraq, Ash-Sham, Libya, Yemen, Burma, Chechnya, Uzbekistan, Afghanistan, Turkestan ... na zaidi. Je! Mnafikiria, Enyi watu wa Jordan, Misri, Hijaz, Pakistan na Uturuki, kwamba kile kilichotokea Gaza au Ash-Sham hakitakutokeeni nyinyi?

Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[أَوَلَا ‌يَرَوْنَ ‌أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُونَ]

“Je! Hawaoni ya kwamba wanatiwa mtihanini kila mwaka mara moja au mara mbili? Kisha hawatubu, wala hawakumbuki.” [Surah At-Tawbah 9:126]. Je! Sio wakati sasa wa nyinyi kuzingatia?! Matatari walivamia ardhi ya Waislamu, wakawauwa Waislamu milioni mbili, kwa sababu ya uhaini, uoga, na mapuuza. Matatari waliikalia kimabavu miji ya Waislamu nchini Iraq na Ash-Sham, hadi walipofika mipaka ya Misri. Uchinjaji wa Waislamu haukusimamishwa isipokuwa kwa uongozi wa dhati, wa Mujahid, ambao uliwashinda Matatari huko Ein Jalut, na kuikomboa miji ya Waislamu, kwa Mujahidina elfu ishirini tu.

Kabla ya hapo, Makruseda waliwachinja Waislamu milioni mbili katika uvamizi wa Makruseda, wakiwemo 70,000 katika Al-Quds kutokana na usaliti, mgawanyiko, na kupuuzwa. Kuchinjwa kwa Waislamu hakutakomeshwa, isipokuwa kwa kuibuka kwa uongozi wa dhati, wa Mujahid. Mshindi Salahudin aliwaangamiza Makruseda huko Hattin, akiwa na Mujahidina elfu ishirini na tano tu.

Je! Sio wakati sasa kwenu, Enyi Waislamu, kugundua kuwa kumwaga damu yenu kunaweza kukomeshwa kwa uwepo tu wa uongozi wenye imani, mkweli kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake pekee? Je! Ni kiasi gani cha damu yenu kinapaswa kumwagwa, mpaka mutambue ukweli huu?! Je! Ni kiasi gani cha hofu na njaa manapaswa kuteseka nacho, mpaka mutambue ukweli huu?! Je! Ni mamilioni mangapi ya Waislamu watauawa chini ya serikali hizi vibaraka, hadi mutambue kuwa kumshinda adui yenu kunaweza kupatikana tu kupitia uongozi wa dhati na wenye imani? Je! Lini  mtagundua kuwa gharama nzito mnayolipia kwa damu yenu, watoto wenu, wanawake wenu, pesa zenu, nyumba zenu, na ardhi yenu, haitalipwa tena, ikiwa mtaelekea kwenye ikulu za marais, kuondoa kikundi cha uhaini na muupe Bayah (ahadi ya utiifu) uongozi ambao ni mwaaminifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake?!

Je! Sio wakati sasa kwenu, Enyi Majeshi ya Waislamu, kutambua kiwango cha hitajio lenu la uongozi wa dhati kwa Mwenyezi Mungu na Mjume wake, ambao utakuongozeni kutoka kwa utukufu hadi utukufu zaidi, na kutoka kwa ushindi hadi ushindi zaidi?!

Je! Sio wakati sasa kwenu, Enyi Majeshi ya Waislamu, kugundua kuwa kikundi cha wasaliti kama As-Sisi, Mfalme wa Jordan, na Bin Salman, na kundi la vibaraka nchini Pakistan, Uturuki, Iraq, na Maghreb ya Kiarabu ... ndio wanaoukandamiza Ummah wenu?! Je! Sio wakati sasa wa nyinyi kugundua kuwa hawatakupeni maisha ya staha, hawatakomboa ardhi yenu, na hawatakuleteeni Nusrah (ushindi)?!

Je! Sio wakati sasa kwenu kuona kwamba watu hawa, na wengine kama wao, ndio viongozi wa usaliti, na ala za makafiri? Je, si ni kwa sababu ya watu kama wao, kwamba Makruseda na Matatari waliwachinja mamilioni ya Waislamu. Wao ndio walioukabidhi Msikiti wa Al-Aqsa kwa Mayahudi. Wao ndio wanaolipa umbile la Kiyahudi njia za kubakia hai. Wao ndio wanaozuia Ummah na majeshi yake kuinusuru Gaza. Wao ndio wanaouchana Ummah na kuzuia umoja wake. Wao ndio wanaowapiga vita watu wenye ikhlasi na kuwazuia kuja madarakani.       

Enyi Ummah wa Muhammad (saw)! Tunakuhutubieni kutoka Ardhi Iliyobarikiwa ya Isra'a ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), Ardhi ya Manabii (as), ardhi ambayo Dawah ya Hizb ut Tahrir ilizinduliwa ili kusimamisha tena Khilafah Rashidah ya pili. Tunakuhutubieni kwa maneno ya Mwenyezi Mungu (swt),

[أَلَمْ ‌يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنْ تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ]

“Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na haki iliyo teremka?” [Surah Al-Hadeed 57:16].

Tunakuhutubieni, Enyi Waislamu, kwa uchungu unaoumiza moyo. Lini mtaitikia wito wa Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ ‌انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]

“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache * Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [Surah At-Tawbah 9:38-39]?!

Tunakuhutubieni, Enyi wanajeshi na maafisa, lini mtamnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kwa kuipa Nusrah Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah Rashida, ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya Mtume wake (saw)? Je! Lini mtawapindua watawala vibaraka, ambao ni wasaliti kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake?

Enyi Ummah wa Muhammad (saw)! Kile kitakachookoa damu yenu, kuyakomboa matukufu, kuleta maisha ya staha kwenu na kwa watoto wenu, na kukupeni utukufu, ushindi, tamkini, huku radhi za Mwenyezi Mungu zikiwa kubwa zaidi, ni uongozi wenye ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, unaokutawaleni kwa yale yote aliyoyateremshwa Mwenyezi Mungu, unaojitahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na husimamisha haki miongoni mwa watu. Hili ndilo ambalo Hizb ut Tahrir anakulinganieni kwalo, mchana na usiku, kuyafikia masikio yenu, na wito kuyataka majeshi ya Waislamu kulifanikisha. Kwa hivyo, ni lini mtajibu wito wa utukufu, wito wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili kutoa Bay’ah kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu Duniani?!

Enyi Ummah wa Muhammad (saw)! Kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu Duniani, kuikomboa Bayt al-Maqdis, na kuwapa Nusrah (kuwasaidia) wanaodhulumiwa ni heshima kubwa ambayo Mwenyezi Mungu hawapi wale ambao ni wasaliti dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Heshima hii kubwa inaweza kufanywa tu na waumini wa kweli. Mwenyezi Mungu haitoi heshima kubwa, isipokuwa kwa waongofu. Kwa hivyo, Enyi wale wenye ruwaza, oneni hili. Kwa hivyo, Enyi watu wenye kuelewa, zingatieni hili!

Kwa kumalizia, tunakulinganieni kwa Ulinganizi wa Mwenyezi Mungu (swt),

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَى تِجَارَةٍ تُنْجِيكُمْ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ * تُؤْمِنُونَ بِاللهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنْفُسِكُمْ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ * يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ * ‌وَأُخْرَى تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِنَ اللهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ * يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا أَنْصَارَ اللهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ لِلْحَوَارِيِّينَ مَنْ أَنْصَارِي إِلَى اللهِ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنْصَارُ اللهِ فَآمَنَتْ طَائِفَةٌ مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَكَفَرَتْ طَائِفَةٌ فَأَيَّدْنَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَى عَدُوِّهِمْ فَأَصْبَحُوا ظَاهِرِينَ]

“Enyi mlio amini! Nikuonyesheni biashara itakayo kuokoeni na adhabu iliyo chungu? Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua. Atakusameheni dhambi zenu, na atakutieni katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani nzuri nzuri katika Bustani za milele. Huko ndio kufuzu kukubwa. Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini! Enyi mlio amini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu, kama alivyo sema Isa bin Mariamu kuwaambia wanafunzi wake: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wakasema wanafunzi: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu! Basi taifa moja la Wana wa Israili liliamini, na taifa jingine lilikufuru. Basi tukawaunga mkono walio amini dhidi ya maadui zao, wakawa wenye kushinda.” [Surah As-Saff 61:10-14].

Ewe Mwenyezi Mungu ifikishe kheri hii kutoka kwetu. Ziangaze nyoyo za Waislamu kwayo na kwa ajili yake. Tupe kutoka Kwako mamlaka na nusra.

Sifa Njema zote ni kwa Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu

H. 8 Jumada II 1445
M. : Alhamisi, 21 Disemba 2023

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu